top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumatatu, 24 Julai 2023

Mimba ya miezi mitano

Mimba ya miezi mitano

Mimba ya miezi mitano ni sawa na mimba ya wiki 17 hadi 20, katika kipindi hiki mabadiliko mbalimbali hutokea mwilini katika kila wiki. Makala hii imeelezea kuhusu mabadiliko yanayotokea katika lila wiki ya mimba ya miezi mitano.


Mimba ya wiki kumi na saba(17)


Nini hutokea kwa mtoto
 • Mtoto huendelea kungezeka uzito na urefu

 • Mafuta hutengenewa katika Ngozi yake ili kumpa joto

 • Nywele za kichwa, kope na nyusi hujaa

 • Mifumo yake ya mwili huendele kuimarika Zaidi

 • Mtoto huanza kuazalisha maji ya chupa ya uzazi(amniotiki) kupitia mapafu


Nini hutokea kwa mama
 • Huongezeka uzito

 • Hamu ya kula huongezeka

 • Huwa na nguvu zaidi

 • Hushindwa lala vizuri kutokana na mimba kuwa kubwa


Mimba ya wiki kumi na nane (18)


Nini hutokea kwa mtoto?
 • Mtoto huendelea kuongezeka kimo na uzito

 • Mtoto huwa na ukubwa wa hoho

 • Mifumo ya mwili huendelea kuimarika

 • Mtoto huanza kupiga miayo na kwikiNini hutokea kwa mama?
 • Tumbo huendelea kukua kwa kasi

 • Matumizi ya damu huongezeka hivyo mama anaweza kuhisi kizunguzungu hasa akisimama kwa haraka baada ya kukaa. Hali hii husababishwa pia na mgandamizo wa mishipa ya damu kutokana na mimba kuwa kubwa

 • Mgandamizo huo husababisha pia maumivu ya mgongo na kiuno


Mambo ya kuzingatia
 • Epuka kulala chali

 • Kunywa maji ya kutosha

 • Endelea kutumia virutubishi vya madini chuma, pamoja na vyakula vyenye madini chuma

 • Fanya mazoezi ya viungoMimba ya wiki kumi na tisa (19)


Nini hutokea kwa mtoto

 • Figo za mtoto huanza kutengeneza mkojo

 • Uwezo wa kusikia sauti kutoka mazingira ya nje y a mama huongezeka

 • Mfumo wa ndani wa uzazi wa mtoto wa kike hukamilika na ovari zake huanza kuzalisha mayai

 • Via vya uzazi vya nje kwa mtoto wa kiume huonekana vema

 • Mtoto huwa na umbo lenye ukubwa wa embe
Nini hutokea kwa mama
 • Kuendelea kuhisi maumivu ya kiuno na mgongo

 • Kuendelea kuhisi mgandamizo kwenye nyongaMimba ya wiki 20


Humaanisha miezi mitano ya ujauzito, ambapo ni nusu ya safari ya ujauzito.


Nini hutokea kwa mtoto?


 • Huwa na urefu wa takribani inchi 11

 • Kichwa huwa na nywele zilizokuwa vema, na mwili wote hufunikwa na vinyweleo laini

 • Ngozi yake huwa na utando mweupe unaozuia isijikunje

 • Mifupa laini hubadilika kuwa migumu kiasi

 • Korodani ambazo zilikuwa pamoja na matumbo huanza kushuka kuelekea kwenye mifuko yakeNini hutokea kwa mama?


 • Kuanza kuhisi mtoto akicheza tumboni hasa kwa wanawake ambao ni ujauzito wa kwanza

 • Kuvimba miguu kutokana na kuongezeka kwa maji katika damu

 • Kupata kiungulia na chakula kutomeng’enywa vema

 • Kushindwa kulala vema kutokana na mgandamizo wa mimba

 • Matiti hujaa na Sehemu ya chuchu huwa nyeusi Zaidi na kuwa na vitu kama vipele, na wakati mwingine kutoa maziwa

 • Katika kipindi hiki mimba huendelea kukua kwa kasi na kuwa usawa wa kitovu, na kuongezeka kwa takribani inchi moja na nusu kwa wiki zinazofuata

 • Mstari mweusi chini ya kitovu hutokea na ngozi ya tumbo huanza kuwa na michirizi

Imeboreshwa:

Jumatatu, 24 Julai 2023 20:30:58 UTC

Rejea za mada hii:

 1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

 2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

 3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

 4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

 5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

 6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

 7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

 8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

 9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page