top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumatatu, 24 Julai 2023

Mimba ya miezi mitatu

Mimba ya miezi mitatu

Mimba ya miezi mitatu ni sawa na mimba ya wiki 9 hadi 12. Katika makala hii utajifunza kuhusu nini kinatokea kwenye wiki ya 9 hadi ya 12 ya ujauzito.


Mimba ya wiki tisa (9)


Nini kinatokea mwilini mwako

  • Mzunguko wa kiuno chako huongezeka taratibu wakati huu

  • Utaanza kuona ongezeko la uzito kutokana na ongezeko la maji mwilini

  • Utapata hisia za tumbo kujaa na uchovu

  • Utapata mabadiliko makali ya hisia kutokana na mabadiliko ya homon progesterone mwilini


Nini kinatokea kwa mtoto tumboni

Mwanao huwa na urefu wa sentimita 2.3 sawa na ukubwa wa zabibu na uzito wa gramu 2 tu.


  • Wakati huu pia viungo muhimu vya mtoto huwa vimeshatengenezwa.

  • Vyumba vya moyo pamoja na milango yake huanza kutengenezwa pia.

  • Macho ya mtoto huwa yameshatengenezwa kikamilifu pamoja na meno, masikio ya nje, midomo, pua na matundu ya pua.

  • Mkia wa mtoto hupotea kabisa na kutoonekana kipindi hiki

  • Kondo la nyuma pia huwa limeshatengenezwa vya kutosha kuweza kufanya kazi muhimu ya kuzalisha homoni.

  • Kwa sababu mtoto anakuwa ameshatengenezwa viungo vingi vya awali kwenye hatua hii, huanza kuongezeka uzito kwa kasi kubwa.


Nini unapaswa kuzingatia kipindi hiki?

Unapaswa kuanza kuungana na mwanao kwa kufanya tafakuri.


Mima ya wiki kumi (10)


Nini kinatokea mwilini mwako?

  • Kijusi hukua kutoka kwenye ukubwa wa mbegu ya mbaazi hadi ukubwa wa zabibu.


  • Mazoezi ni muhimu wakati huu kwa kuwa yatasaidia kuuandaa mwili wako na msongo, kubeba uzito wa ziada pamoja na uchungu. Hata hivyo pia yatasaidia kupunguza maumivu ya mgongo wakati wa ujauzito na kufanya mwili wako urejee kwenye hali ya kawaida baada ya kujifungua.

  • Unaweza kufanya mazoezi ya kutembea au mengine unayoweza kwa miezi tisa yote. Unapaswa kuwasiliana na daktari kuhusu mazoezi gani yanakufaa wiki kwa wiki katika ujauzito.


Nini kinatokea kwa mtoto?
  • Wiki hii hutia alama ya kuanza kipindi cha ukuaji wa mtoto na wakati huu viungo mbalimbali vya mtoto hukua haraka.

  • Kipindi hiki mapigo ya moyo ya mtoto yanaweza kutambuliwa kwa kifaa maalumu kinachowekwa kwenye ukuta wa tumbo kinachoitwa Doppler stethoscope. Mtaalamu wa afya anaweza kukusikilizisha mapigo ya mwanao utakapotembelea kliniki

  • Mtoto hupata uwezo wa kunywa maji yaliyo ndani ya chupa ya uzazi na pia huweza kujikunja na kunyoosha miguu yake.

  • Viungo mbalimbali vya mtoto huanza kufanya kazi vema na kwa kujitegemea.

  • Mwonekano wa nje wa uti wamgongo huonekana na pia mishipa ya fahamu ya uti wa mgongo hukua kutoka kwenye uti wa mgongo.


Mimba ya wiki kumi na moja (11)


Nini hutokea kwa mtoto
  • Kijusi hukua na kupata taswira ya binadamu

  • Kichwa huwa cha mviringo na chenye mabonde

  • Jicho huwa limefungwa kwa kigubiko cha jicho

  • Matundu ya vinyweleo huanza kutengenezwa kwenye ngozi

  • Matumbo huwa yamedumbukia katika kitovu cha mtoto

  • Sehemu za nje za siri huwepo lakini huwa hazijatengenezwa vizuri hivyo kushindwa kujua jinsia ya mtoto


Nini hutokea kwa mama
  • Hakuna mabadiliko makubwa ukilinganisha na wiki za awali

  • Mama huendelea kuhisi dalili za ujauzito kama kuvimba matiti, kubagua chakula, kichefuchefu na kutapika nk.


Mimba ya wiki kumi na mbili (12)


Nini hutokea kwa mtoto
  • Umbo na sura halisi ya binadamu huonekana lakini masikio huwa hayajakua vizuri

  • Vidole vya miguu na mikono huwa na umbo linaloeleweka na kucha huanza kutokea

  • Ngozi ya mtoto huwa nyembamba kiasi cha kuonyesha vilivyomo ndani ya mwili wake kama vile mishipa ya damu

  • Nyusi na nywele za kichwa huota, na mwili huwa na vinyweleo vichanga vilivyotawanyika (lanugo)

  • Katika kipindi hiki sehemu za siri za nje huanza kuonesha tofauti kati ya jinsia ME na jinsia KE

  • Matumbo huhama kutoka katika kitovu cha mtoto na kuwa katika eneo la wazi linalounganisha kifua na kiwamba tumbo

  • Misuli hupata huwa na mjongeo (primitive reflexes)

  • Mtoto huanza kucheza tumboni lakini si rahisi kwa mama kuhisi


Nini hutokea kwa mama
  • Kizazi hutanuka kiasi cha kuweza kupapaswa juu ya kinena

  • Dalili za kichefuchefu na kutapika huanza kupungua hata hivyo dalili nyingine za ujauzito kama vile kuhisi kuchoka, kukojoa mara kwa mara, kutokwa na ute ute ukeni nk. huendelea kuonekana

Imeboreshwa:

Jumatatu, 24 Julai 2023 21:02:57 UTC

Rejea za mada hii:

  1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

  2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

  3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

  4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

  5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

  6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

  7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

  8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

  9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page