top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumatatu, 24 Julai 2023

Mimba ya mwezi mmoja

Mimba ya mwezi mmoja

Utangulizi


Ujauzito wa mwezi mmoja ni sawa na ujauzito wa wiki nne. Mambo yanayotokea katika ujauzito wa wiki hizi ni kama ifuatavyo katika kila wiki.


Ujauzito wa wiki moja (1)

Dalili za ujauzito wa wiki 1 huwa tofauti kwa kila mwanamke na ujauzito mmoja na mwingine. Dalili kuu inayotokea ni kukosa hedhi na wakati huu mwili unakuwa unajiandaa kupokea kijusi kitakachotungishwa katika wiki zinazofuata za ujauzito. Dalili zingine zinazoweza kutokea ni pamoja na:

 • Kichefuchefu bila kutapika

 • Mabadiliko kwenye chuchu

 • Kukojoa mara kwa mara

 • Maumivu ya kichwa

 • Ongezeko la joto la mwili

 • Hisia za gesi tumboni

 • Maumivu ya wastani ya nyonga

 • Uchovu mkal

 • Kubadilika hali ya moyo

 • Kupendelea chakula aina fulani tu

 • Ongezeko la hisia kwenye harufu

 • Kuhisi umetali kwenye ulimi


Mara nyingi dalili hizi huwa hazitambuliki na wengi, na njia pekee ya kufahamu kuwa una ujauzito ni kupima.


Ujauzito wa wiki mbili (2)

Katika ovari, mayai hukomaa na uovuleshaji hufanyika mwishoni mwa wiki ya pili. Hii ina maana kwamba, moja ya ovari itaruhusu yai moja kutolewa kisha kuingia kwenye mrija wa falopio tayari kwa urutubishwaji.


Ukuta wa mji wa mimba wakati huu hukua ili kujiandaa na uchavushaji na upandikizaji wa yai kwenye kuta zake kama uchavushaji utatokea.


Ujauzito wa wiki tatu (3)

Hii ni wiki ambayo uchavushaji wa yai na utungishaji mimba hufanyika. Yai litarutubishwa na moja ya manii iliyomwagwa ukeni wakati wa ngono na kufanikiwa kupita kwenye shingo ya kizazi hadi kwenye mrija wa falopio ili kukutana na yai kisha kuingia ndani yake.


Mabadiliko yanayotokea

Mara baada ya yai kuchavushwa na manii, chembe mithiri ya mpira huanza kukua kwa nje huku ikigawanyika ndani kuwa chembe nyingi ndani yake. Katika hatua hii, matokeo ya uchavushaji yai hutengeneza blastosait, ambayo huwa na shemu mbili, sehemu ya nje ambayo itakuwa kondo la nyuma na sehemu ya ndani ambayo itakuwa kiini tete.

Wiki ya 3 ya ujauzito


Jinsia ya mtoto wako huamriwa wakati huu wa uchavushaji. Kwenye hatua hii Mtoto hufahamika kama kiinitete ambacho huwa na takribani chembe 150 zitakazokuwa kwenye matabaka mbalimbali yaliyoelezewa hapa chini.


Tabaka la ndani

Tabaka la ndani hufahamika kama endodem au endoblasti, hubadilika mbeleni na kutengeneza;


 • Njia ya hewa ya mfumo wa upumuaji

 • Mfumo wa umeng’enyaji chakula

 • Kongosho

 • Thyroid

 • Ini

 • Thymus


Tabaka la kati

Tabaka la kati hufahamika kama mesoderm, tabaka hili hukua na kutengeneza viungo vifuatavyo;

 • Mifupa

 • Misuli

 • Moyo na mishipa ya damu

 • Mfumo wa utoaji taka mwilini

 • Maumbile ya kike na kiume


Tabaka la nje

Tabaka la nje hufahamika pia kama ektodem au ektoblast. Hukua na kuengeneza viungo vifuatavyo;

 • Ubongo

 • Ngozi

 • Kucha

 • Nywele


Wakati kiinitete kinapata mabadiliko haya, huwa kinaelea ndani ya tumbo la uzazi kikiwa kinalindwa na ute ute unaozalishwa na kizazi.


Ujauzito wa wiki nne (4)

Nini hutokea mwilini mwako?

Mwili wako unapitia mabadiliko makubwa huku kitufe kidogo cha chembe ambacho kitakuwa kijusi cha mtoto wako hubadilika kuwa kiinitete chenye tabaka nyingi.

Wiki ya 4 ya ujauzito


Mabadiliko haya yanaweza kusababisha dalili kama vile;


 • Maumivu ya tumbo la chini ya kubana

 • Hisia za kuvimbiwa

 • Hisia za juu na kushuka moyo


Dalili hizo hufanana kama dalili za kabla ya kuingia hedhi.


Wakati huu pia kifuko cha mimba na kifuko cha kiini hutengenezwa. Kifuko cha mimba na kiini hujazwa na maji ambayo hufanya kazi ya ulinda kiinitete kianchotengenezwa.


Kifuko cha kiini huzalisha damu na husaidia kukilisha kiinitete mpaka pale kitovu na kondo la nyuma litakapotengenezwa ili kufanya kazi hiyo.


Nini hutokea kwa mtoto tumboni?


Mfumo wa mishipa ya damu ya mtoto ( arteri, vena na kapilari) hukua na husaidia kusafirisha damu, oksijeni na virutubisho vingine kutoka mwilini mwako kwenda kwa mtoto kupitia kitovu cha mtoto.


Moyo wa mtoto pia huanza kufanya kazi na damu huanza kusukumwa. Ogani nyingine pia huanza kutengenezwa.


Hatua hii pia kiinitete huanza kuzalisha kichocheo human chorloric gonadotropin (hCG), kinachozalishwa baada ya kujipandikiza kwa yai lililochavushwa. Kuonekana kwa kichocheo hiki kwenye kipimo cha mkojo au damu hutumika kuthibitisha kuwa una ujauzito kama una ujauzito.


Mambo unayotakiwa fahamu


Kama ukijipima na kujikuta na ujauzito kwa kipimo hiki, unapaswa kuwasiliana na daktari kwa ushauri zaidi wa kulea ujauzito wako.


Majina mengine ya makala hii

MImba ya mwezi mmoja (1) huwa na maana pia ya

 • Ujauzito wa mwezi mmoja

 • Ujauzito wa mwezi 1

 • Mimba ya wiki 1 hadi 4

Imeboreshwa:

Jumatatu, 24 Julai 2023 21:01:33 UTC

Rejea za mada hii:

 1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

 2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

 3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

 4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

 5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

 6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

 7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

 8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

 9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page