top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

Jumatatu, 19 Julai 2021

Aflatoksin

Aflatoksin

Aflatoksin ni aina ya sumu inayosababisha saratani ya ini, mwili huathiriwa na sumu kwa kuvuta hewa au kula mazao yaliyoathiriwa na fangasi. Jikinge kwa kutambua na kula mazao ya shamba ambayo hayajaathiriwa.


Aflatoksini ni nini?


Aflatoksin ni aina ya sumu inayozalishwa sana na fangasi Aspergillus flavus, Aspergillus parasiticus na Aspergillus nomius wanaopatika kwenye mazao mengi ya shamba. Sumu hii huwa kihatarishi kikubwa cha saratani ya ini kwa binadamu.


Kuna aina 20 za aflatoksin zinazofahamika, aina kuu nne ni aflatoksin B1 (AFB1), aflatoksin B2 (AFB2), aflatoksin G1 (AFG1), aflatoksin G2


Majina mengine ya Aflatoksin hufahamika kama 'sumu ya karanga' sumu ya aflatoksini' 'sumu ya aflatoxin' au 'aflatoxin'


Ni mazao yapi ya shamba huweza kuwa na sumu na aflatoksin?


Mazao ya shamba yenye sumu ya aflatoksini ni;

 • Shayiri

 • Maindi

 • Karanga

 • Njugu

 • Mbegu za pamba


Mazao mengine ya karanga ni kama;

 • Lozi

 • Korosho

 • Nazi

 • Pine

 • Pekani


Mazao mengine mapya yalioonekana kwenye tafitikuwa naaflatoksin ni;

 • Mtama

 • Ufuta

 • Mchele

 • Viungo mbalimbali

 • Kokoa

 • Ngano


Ni mazingira gani husababisha kuota kwa fangasi wanaozalisha aflatoksin?


Fangasi wanaozalisha aflatoksin hupatikana sana maeneo yenye unyevu na joto duniani na huathiri mazao yakiwa shamba au wakati wa kuhifadhi.


Sumu ya aflatoksini inawezaje kuingia mwilini?


Aflatoksin inaweza kuingia mwilini kwa kula vyakula au mazao ya vyakula vilivyo na sumu au kwa kula nyama na maziwa ya wanyama waliokula mazao yenye sumu hii.


Wakulima na wafanyakazi wa shamba wanaweza kupata sumu hii kwa kuvuta hewa ya mazao wakati wanavuna au kusafisha mazao au mimea yenye sumu.


Namna gani ya kupunguza uwezekano wa kudhurika na aflatoksin?


Unaweza kupunguza hatari ya kula au kuvuta hewa yenye aflatoksin kwa;

 • Kutumia karanga na siagi ya karanga zenye ubora tu

 • Chambua karanga ili kutoa zile zinazoonekana kuwa na fangasi, rangi iliyo tofauti na kawaida au zilizosinyaa

 • Kununua siagi ya kawanga zilizopimwa na kuthibitishwa kuwa hazina sumu hii

 • Kuvaa barakoa wakati unavuna au unahudumia mazao haswa endapo yameoza

 • Kutunza mazao kwenye njia zinazotakiwa ili yasiliwe na fangasi

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:40:35

Rejea za mada hii:

1. Aflatoxins. https://www.cancer.gov/about-cancer/causes-prevention/risk/substances/aflatoxins. Imechukuliwa 19.07.2021

2. World Health Organization. Aflatoxinshttps://www.who.int/foodsafety/FSDigest_Aflatoxins_EN.pdf

3. Pradeep Kumar, et al. Aflatoxins: A Global Concern for Food Safety, Human Health and Their Management. https://www.frontiersin.org/articles/10.3389/fmicb.2016.02170/full. Imechukuliwa 19.07.2021

4. Aflatoxin. https://www.sciencedirect.com/topics/earth-and-planetary-sciences/aflatoxin. Imechukuliwa 19.07.2021

5. Dipendra K. Mahato, et al. Aflatoxins in Food and Feed: An Overview on Prevalence, Detection and Control Strategies. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6787635/#. Imechukuliwa 19.07.2021

6. Pradeep Kumar, et al. Aflatoxins: A Global Concern for Food Safety, Human Health and Their Management. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5240007/. Imechukuliwa 19.07.2021

bottom of page