top of page

Mwandishi:

Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Jumanne, 21 Septemba 2021

Madhara ya vidonge vya majira

Madhara ya vidonge vya majira

Matumizi ya vidonge vya majira ni njia nyepesi ya uzazi wa mpango inayopendwa na wanawake wengi. Licha ya kuwa na faida nyingi, tafiti zimeonyesha vidonge hivi huongeza hatari ya kupata magonjwa ya fizi na meno, saratani ya titi na shingo ya kizazi, kuganda kwa damu, kuamka kwa kipanda uso na shinikizo la juu la damu. Kama una vihatarishi vingine vya magonjwa haya, ongea na daktari wako akushauri njia nzuri zaidi ya kutumia.


Dawa za majira ni nini?


Dawa za majira kwa jina jingine dawa za uzazi wa mpango, ni dawa za kunywa zenye homon zinazozuia kushika ujauzito. Dawa hizi hufanya kazi ya kuzuia ovari kuzalisha mayai na manii kuingia ndani ya mfuko wa kizazi.


Dawa nyingi za uzazi wa mpango zinazotumika huwa na mchanganyiko wa homon mbili (progesterone na estrogen) zinazofanana na zile za binadabu lakini zimetengenezwa kwa kusanisi. Vidonge vyenye homoni mbili huitwa ‘vidonge mchaganyiko vya majira’, au ‘majira mchanganyiko’. Baadhi ya vidonge vya majira pia hutengenezwa kwa homon moja tu ya kusanisi haswa progesterone na huitwa ‘kidonge cha progestin’


Maudhi madogo


Matumizi ya vidonge vya majira huwa na maudhi yafuatayo;


 • Kutokwa na matone ya damu ukeni

 • Kutokwa damu bila mpangilio (hali hii hupungua baada ya miezi mitatu ya kwanza ya matumizi)

 • Maumivu ya matiti yakiguswa

 • Tumbo kujaa gesi

 • Kichefuchefu

 • Ongezeko kiasi la uzito


Nani asiyepaswa kutumia vidonge vya majira?


Wanawake mwenye umri zaidi ya miaka 35 na mwenye shinikizo la juu a damu, kipanda uso chenye aura, matatizo ya ini, kiwango cha juu cha lehemu kwenye damu, historia ya kuganda damu, kiharusi, saratani ya titi na watumiaji wa wa sigara hawapaswi kutumia vidonge hivi.


Madhara ya majira


 • Huamsha magonjwa ya fizi na meno kuoza

 • Huongeza hatari ya saratani ya titi

 • Huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi

 • Huongeza hatari ya damu kuganda

 • Huamsha kipanda uso

 • Huongeza shinikizo la juu la damu

 • Huongeza hatari ya magonjwa ya moyo


Maelezo zaidi yanapatikana chini yanapatikana aya zinazofuata.


Huamsha magonjwa ya fizi na meno kuoza


Tafiti mbalimbali zilizofuatiliwa wanawake waliokuwa wanatumia vidonge vya majira na kufananisha na wale ambao hawatumii zimeonyesha kuwa wanawake waliotumia vidonge hivi kwa muda mrefu meno yao yalipata matundu yenye kina kirefu nan a magonjwa ya fizi kama vile fizi kutoa damu.


Huongeza hatari ya saratani ya titi


Licha ya tafiti nyingi zilizofanyika kutumia njia ya kuangalia madhara kwa watumiaji wa dawa hizi, tafiti 54 zilizoangalia wanawake 150,000 zimeonyesha kuwa;


Watumiaji wa nadra wa majira wana ongezeko zaidi la asilimia 7 kupata saratani ya titi

Wanawake waliokuwa wanaendelea kutumia hatari yao ya kupata saratani ilikuwa asilimia 24 zaidi.


Huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi


Wanawake waliotumia dawa za uzazi wa mpango kwa muda wa miaka mitano au zaidi wana hatari zaidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kuliko wanawake ambao hawakuwahi tumia dawa hizi. Kutumia dawa za majira kwa muda mrefu, huongeza hatari zaidi kuliko mtumiaji wa muda mfupi.Tafiti mbalimbali zimeonyesha mambo yafuatayo; • Watumiaji wa chini ya miaka mitano ongezeko la hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi ni mara 10 zaidi

 • Watumiaji wa miaka 5 hadi 9 ongezeko la hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi ni mara 60 zaidi

 • Watumiaji wa zaidi ya miaka 10 ongezeko la hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi ni mara 120 zaidi


Mbali na hivyo tafiti zimeonyesha kuwa hatairi ya saratani ya shingo ya kizazi hupungua mtumiaji anapoacha kutumia dawa hizo.


Huongeaza hatari ya damu kunganda, shinikizo la juu la damu na magonjwa ya moyo


Huongeza hatari ya damu kuganda


Matumizi ya dawa za majira huongeza hatari ya kutengenezwa kwa mabonge ya damu ndani ya mishipa ya damu haswa kwenye miguu. Mabonge ya damu yana hatari ya kunyofoka na kusafiri kwenye mishipa ya damu na huweza kuziba mizipa midogo ya damu kwenye mapafu na kusababisha embolizim ya palmonari. Tafiti zinaonyesha hatari hii huongezeka mara nyingi zaidi kama mtumiaji ana vihatarishi vingine vya;


Maagonjwa ya kurithi na hali

 • Kuwa na factor V Leiden

 • Kubadilika kwa jeni ya Prothrombin

 • Upungufu wa protini asili za kuzuia ugandishaji damu kama (antithrombin, protin C naprotein S)

 • Kuzidi kwa kiwango cha homocysteine

 • Kuwa na kiwango cha juu au kushindwa kufanya kazi kwa fibrinogen

 • Kuwa na kiwango kikubwa cha factor VIII, IX na XI

 • Ugonjwa wa hypoplasminogenemia

 • Ugonjwa wa dysplasminogenemia

 • Kuwa na kiwango cha juu cha kizuizi cha kiamsha plasminogen (PAI-1)


Hali na magonjwa ya kutorithiwa

 • Saratani

 • Matumizi ya dawa za kutibu saratani tamoxifen, bevacizumab, thalidomide na lenalidomide

 • Kufanyiwa upasuaji au kupata jeraha hivi karibuni

 • Kuingiziwa mrija kwenye mishipa mikuu ya damu

 • Obeziti

 • Ujauzito

 • Kukaa kwa muda mrefu bila kutembea au kufanya mazoezi

 • Mshituko wa moyo

 • Kuferi kwa moyo

 • Kiharusi

 • Upungufu wa chembe sahani za damu kutokana na matumizi ya heparin

 • Kusafiri kwa muda mrefu kwenye ndege au gari

 • Kuwa na antibodi dhidi ya fosfolipid

 • Historia iliyopita ya kuganda kwa damu kwenye mishipa ya ndani

 • Embolism ya mapafu

 • Ugonjwa wa damu nyingi

 • Thrombosatosis

 • Paroxysmal nocturnal hemoglobinuria

 • Sindromu ya inflamatori bowel

 • UKIMWI

 • Sindromu ya Nephrotik

 • Kuvuta sigara


Huongeza shinikizo la juu la damu


Matumizi ya vidonge vya majira huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Hatari pia huongezeka zaidi kama mtumiaji ana vihatarishi vingine ambavyo ni;


 • Obeziti

 • Historia ya shinikizo la damu kwa wazazi au ndugu wa tumbo moja

 • Kuvuta sigara


Kama una shinikizo la juu la damu, ni vema ukawasiliana na daktari kuhusu uchaguzi wa njia nzuri ya uzazi wa mpango.


Huongeza hatari ya magonjwa ya moyoKwa wanawake walio zaidi ya miaka 35, wanaovuta sigara sana na kutumia dawa za uzazi wa mpango, huwa na ongezeko la hatari ya kupata mshituko wa moyo na kiharusi. Hatari huongezeka mara nyingi zaidi kama kuna vihatarishi vingine ambavyo ni;


 • Historia ya magonjwa ya moyo kwa ndugu wa damu moja

 • Kuwa na kiwango cha juu cha lehemu kwenye damu(kolestro)

 • Shinikizo la juu la damu


Huamsha kipanda uso


Vidonge vya majira haswa vile vyenye homon estrogen vimeonekana kuamsha kipanda uso kwa watumiaji wenye kipanda uso. Unapaswa kuongea na daktari wako kuhusu njia gani ya kutumia kam una kipanda uso.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021 16:12:56

Rejea za mada hii:

Jin J. Oral Contraceptives. JAMA. 2014;311(3):321. doi:10.1001/jama.2013.283505. inapatikana. https://jamanetwork.com/journals/jama/fullarticle/1814214. Imechukuliwa 21/09/2021

Collaborative Group on Hormonal Factors in Breast Cancer. Breast cancer and hormonal contraceptives: collaborative reanalysis of individual data on 53,297 women with breast cancer and 100,239 women without breast cancer from 54 epidemiological studies. Lancet 1996; 347(9017):1713–1727

Mørch LS et al. Contemporary hormonal contraception and the risk of breast cancer. New England Journal of Medicine 2017; 377(23):2228-2239.

Smith JS et al. Cervical cancer and use of hormonal contraceptives: a systematic review. Lancet 2003; 361(9364):1159-1167.

International Collaboration of Epidemiological Studies of Cervical Cancer, Appleby P, Beral V, et al. Cervical cancer and hormonal contraceptives: collaborative reanalysis of individual data for 16,573 women with cervical cancer and 35,509 women without cervical cancer from 24 epidemiological studies. Lancet 2007; 370(9599):1609–1621.

Roura E et al. The influence of hormonal factors on the risk of developing cervical cancer and pre-cancer: Results from the EPIC Cohort. PLoS One 2016; 11(1):e0147029.

NCI. Oral Contraceptives and Cancer Risk. https://www.cancer.gov/about-cancer/causes-prevention/risk/hormones/oral-contraceptives-fact-sheet. Imechukuliwa 20/09/2021

Prachi, Sharma et al. “Impact of oral contraceptives on periodontal health.” African health sciences vol. 19,1 (2019): 1795-1800. doi:10.4314/ahs.v19i1.56

bottom of page