top of page

Mwandishi:

Dkt. SAlome A, MD

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Jumanne, 19 Aprili 2022

Mlo wa kutibu pumu ya ngozi

Mlo wa kutibu pumu ya ngozi

Tafiti nyingi zimefanyika kuangalia uhusiano wa chakula na ugonjwa wa pumu ya ngozi, aina tofauti za vyakula vimeonekana kupunguza na kuficha kabisa dalili za ugonjwa huu lakini si kutibu. Tafiti nyingi zinaendelea na zinaleta matumaini mazuri.


Mlo wa kupunguza michomo kinga kwa pumu ya ngozi


Mlo wa aina hii huwa na umuhimu mkubwa kama vile kupunguza maumivu ikiwa pamoja na maumivu ya misuli. Aina hii ya chakula ni muhimu sana kwa wagonjwa wa pumu ya ngozi haswa inayoamshwa na msongo, mwitikio mkubwa wa kinga ya mwili kwenye viamsha mzio na vichokoza ngozi vya kwenye mazingira.


Mlo huu msingi wake ni kuwa na kiwango kidogo au kukosa maziwa na mazao yatokanayo na maziwa, nyama nyekundu, sukari na vyakula vya nafaka zisizokobolewa na hushamiri kwa mazao ya mimea, matunda na samaki.


Mfano vyakula vinavyojenga mlo huu ni

 • Matunda

 • Mboga za majani

 • Nafaka zisizokobolewa

 • Mafuta ya kiafya kutoka kwa mzeituni au ufuta

 • Samaki wenye mafuta ya omega 3 kwa wingi


Mlo wa ki-mediterania kwaajili ya pumu ya ngozi


Watalaalamu wa tiba kwa muda mrefu wamekuwa wakisifia chakula cha kimediterania ambacho hushamiri vyakula kutoka mboga za majani, matunda, nafaka zisizokobolewa, mimea jamii ya kunde, samaki, mafuta ya omega 3 na mzeituni/ aina hii ya chakula huwa na kiwango kikubwa cha chakula kutoka kwenye mimea na chanzo cha protini ni mimea.


Mlo wa ki-ayuveidik kwa pumu ya ngozi


Kama kilivyo chakula cha kimediterania, chakula cha ki-ayuviedik msingi wake ni vyakula kutoka kwenye mimea na ambavyo hazijasindikwa.


Mfano wa vyakula kwenye aina hii yay a mlo ni;

 • Viungo kama tangawizi, mdalasini na manjano

 • Kunde na mimea jamii yake

 • Nafaka zisizokobolewa


Aina zote za vyakula vinavyotumika huwa na uwezo wa kuzuia mwitikio wa kinga ya mwili na kuzimua sumu za umetaboli mwilini.


Mlo wa kutokomeza pumu ya ngozi


Ili kutimiza malengo ya mlo aina hii, mtumiaji huanza kuacha kula chakula kimoja baada ya kingine (amgalau kwa muda wa siku tatu) kutoka kwenye vyakula anavyokula kisha kuongeza kimoja baada ya kingine kwenye mlo wake. Hii husaidia kuchunguza ni chakula gani ambacho kikitumika hupunguza au huzidisha mzio na kuonekana kwa dalili zaidi za pumu ya ngozi.


Baadhi ya wataalamu hawashauri mpango wa aina hii kutumika hasa kwa watoto.


Mlo wa pumu ya ngozi ya ki-dishaidrotiki


Kwa bahati mbaya, hakuna mlo hata mmoja ambao ni maalumu kwa pumu ya ngozi yak i-dishaidrotiki. Aina hii ya pumu hutokea mara nyingi mikononi na husababishwa na kukauka kwa ngozi na kukosa unyevu kurokana na kujianika juani na matumizi ya kemikali kama vile vitakasa mikono.


Matibabu yake mara nyingi huhusisha matumizi ya steroidi, hata hivyo kutokana na aina hii ya pumu kusababisha malenge madogo na kupasuka kwa ngozi, wagonjwa hushauriwa kuepuka vyaku vyenye tindikali kwa wingi kama vile matunda jamii ya citrus ambayo husabaisha uchokozi wa ziada kwenye ngozi pia kuepuka madini kama nickel na cobalt yanayopatika kwa wingi kwenye vyakula vilivyotajwa hapa chini kama;


 • Ngano isiyokobolewa

 • Shayiri

 • Kokoa

 • Rai

 • Magadi soda

 • Vyakula vyenye soya

 • Matunda yaliyokaushwa

 • Mbaazi

 • Vyakula vilivyosindikwa


Mgonjwa wa pumu ya ki-dishaidrotiki akitaka kuandaa chakula au kitu chochote chenye tindikali kwa wingi anashauriwa kuvaa glavu zinavyozuia kuguswa na tindikali hii.


Mlo unaokosa Gluten


Gluteni ni kemikali inayopatikana kwenye vyakula aina mbalimbali kama vule mkate, viazi mviringo, vyakula vilivyookwa, soya na vyakula vilivyotiwa soya, na aina Fulani ya mchanganyiko wa matunda

Gluteni ni kemikali inayopatikana kwenye vyakula aina mbalimbali kama vule mkate, viazi mviringo, vyakula vilivyookwa, soya na vyakula vilivyotiwa soya, na aina fulani ya mchanganyiko wa matunda

Kwa baadhi ya watu, wanapoacha mlo wenye gluten dalili za pumu ya ngozi hupungua na wengine hupata nafuu kidogo au kutopata mabadiliko yoyote.


Majina mengine ya makala hii


Makala hii inafahamika pia kwa jina la chakula wagonjwa wa eczema na mlo kwa ajili ya wagonjwa wa eczema.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Aprili 2022 15:30:21

Rejea za mada hii:

1. An overview of the different types of eczema. (n.d.).nationaleczema.org/eczema/types-of-eczema/. Imechukuliwa 19.04.2022

2. Bath-Hextall FJ, et al. (2012). Dietary supplements for established atopic eczema in adults and children. ncbi.nlm.nih.gov/pubmedhealth/PMH0033946/. Imechukuliwa 19.04.2022

3. Caproni M, et al. (2012). Celiac disease and dermatologic manifestations: Many skin clue to unfold gluten-sensitive enteropathy. DOI:dx.doi.org/10.1155/2012/952753. Imechukuliwa 19.04.2022

4. Dietary guidelines for Americans 2010. (2010).health.gov/dietaryguidelines/dga2010/dietaryguidelines2010.pdf. Imechukuliwa 19.04.2022

5. Eczema (atopic dermatitis). (2015). allergy.org.au/patients/skin-allergy/eczema

6. Katta R, et al. (2014). Diet and dermatitis: Food triggers. ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3970830/

7. Lien TY, et al. (2011). Breastfeeding and maternal diet in atopic dermatitis. ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3237513/. Imechukuliwa 19.04.2022

8. Maroon JC, et al. (2006). Omega-3 fatty acids (fish oil) as an anti-inflammatory: An alternative to nonsteroidal anti-inflammatory drugs for discogenic pain.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/16531187

9. Mayo Clinic Staff. (2017). Fish oil. mayoclinic.org/drugs-supplements-fish-oil/art-20364810. Imechukuliwa 19.04.2022

10. Sharma AD. (2013). Low nickel diet in dermatology. ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3667300/

11. Skin care for eczema. (2017). ncbi.nlm.nih.gov/pubmedhealth/PMH0072582/. Imechukuliwa 19.04.2022

12. Stukert J, et al. (2008). Low-cobalt diet for dyshidrotic eczema patients. DOI: doi.org/10.1111/j.1600-0536.2008.01469.x. Imechukuliwa 19.04.2022

bottom of page