Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Peter A, MD
Jumatatu, 1 Novemba 2021
Sharubati ya Kutibu U.T.I
Sharubati ya beri ya bluu pamoja na tui la nazi hutibu na kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya U.T.I kwa kuua na kudhoofisha uwezo wa bakteria wanaosababisha U.T.I kuingia kwenye mfumo wa mkojo.
Bakteria eschelician coli anayeongoza kusababisha U.T.I husafiri katika mfumo wa mkojo kwa kutumua miguu maalumu inayomwezesha kujishikiza kwenye mfumo wa mkojo, matumizi ya sharubati ya tui la nazi pamoja na beri ya bluu hudhoofisha miguu ya bakteria na hivyo kufanya wasafishwe kirahisi wakati wa kukojoa na hivyo kupunguza idadi ya bakteria wanaoingia kwenye kibofu cha mkojo.
Kupungua kwa vimelea wanaoingia kwenye kibofu cha mkojo hupunguza vipindi vya kuugua U.T.I kwa wanawake, wanaume na watoto.
Uwezo wa tui la nazi
Tuia la nazi pia huwa na viuaji vya viini vya maradhi kama bakteria wanaosababisha U.T.I, hivyo kutumia sharubati hii kutakufanya upone U.T.I na kupunguza vipindi vya kuugua U.T.I.
Kazi zingine za sharubati ya beri ya bluu na tui la nazi
Huua vimelea vya U.T.I
Huimarisha kinga ya mwili
Huondoa sumu mwilini
Vitamin na madini katika unavyopata kwenye sharubati hii
Vitamin C
Chuma
Magnesium
Potasium
Zink
Vitamin B1
Vitamin B6
Folate
Nishati
Sukari
Mafuta
Sodium
Protini
Nyuzilishe
Kufahamu namna ya kuandaa, kiasi gani utumie na kiasi gani cha madini na vitamin unapata kwa kila glasi unayokunywa ingia kwenye makala ya sharubati ya beri ya bluu na tui la nazi.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Novemba 2021 20:38:05
Rejea za mada hii:
1. Kim HW, et al. Synergistic cranberry juice combinations with natural-borne antimicrobials for the eradication of uropathogenic Escherichia coli biofilm within a short time. Lett Appl Microbiol. 2019 Apr;68(4):321-328. doi: 10.1111/lam.13140. Epub 2019 Mar 13. PMID: 30801748.
2. Hisano, Marcelo et al. “Cranberries and lower urinary tract infection prevention.” Clinics (Sao Paulo, Brazil) vol. 67,6 (2012): 661-8. doi:10.6061/clinics/2012(06)18.
3. Jackson, Courtney B et al. “Complementary and alternative therapies for urinary symptoms: use in a diverse population sample qualitative study.” Urologic nursing vol. 32,3 (2012): 149-57.