Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Helen L, M.D
Ijumaa, 29 Januari 2021
Usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa
Matumizi yasiyo sahihi ya dawa jamii ya ‘antibiotic’ na ‘antifungal’ zinazotibu magonjwa mbalimbali kama kisonono, TB, UTI, tonses, nimonia, homa ya matumbo, fangasi ukeni n.k, husababisha vimelea kuwa sugu na kutotibika na dawa hizo. Tumia dawa kama ulivyoandikiwa na daktari wako.
Hali ya usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa
Tafiti nyingi zimefanyika kuangalia ukubwa wa tatizo la usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa. Tafiti hizo zinaonyesha kuwepo na ongezeko kubwa la usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa za kutibu maambukizi ya bakteria na fangasi. Tatizo hili linaweza kudhuru watu wa umri wowote na taifa lolote lile na huongeza gharama kwa wagonjwa na kukaa hospitali kwa muda mrefu.
Sababu za vimelea kuwa sugu
Sababu kuu zinazochangia kutokea kwa tatizo hili ni;
Kutokuwepo kwa mwongozo wa matumizi ya dawa kwa wataalamu wa afya inayofanya mtaalamu kujichagulia dawa bila kujali ni daraja gani la dawa lianze kutumika kwanza kabla ya kwenda daraja kubwa zaidi
Matumizi ya dawa bila kuandikiwa na daktari mwenye leseni na weledi wa dawa hizo
Matumizi ya dawa bila kufanyiwa vipimo kuonyesha ugonjwa uliopo
Kuandikiwa dawa na mtu ambaye si mtaalamu wa afya
Kutumia dawa bila kukamilisha dozi nzima uliyoandikiwa na mtaalamu wa afya
Nini ufanye ili kuepuka usugu wa vimelea kwenye dawa?
Tumia dawa endapo tu umeandikiwa na daktari aliyesajiliwa
Usinunue au kutumia dawa za 'antibiotic' au 'antifungal' endapo mtaalamu amekwambia huhitaji tumia dawa hizo
Usitumie mabaki ya dawa za 'antibiotic' au 'antifungal' au kutumia kwa pamoja dozi ya mtu mwingine
Tumia dozi ya dawa kwa masaa na siku ulizopangiwa na mtaalamu wa afya
Jikinge na maradhi mbalimbali kwa kufuata kanuni za kiafya mfano, Kunywa maji safi na salama, nawa mikono kabla ya kula, andaa chakula kwa usafi, fanya ngono salama na pata chanjo kwa wakati ili uepuke matumizi ya dawa
Usitumie mazao ya wanyama au ndege waliokuzwa kwa dawa za 'antibiotic' au kutumia dawa hizo kama kinga ya maradhi ya magonjwa, isipokuwa endapo walikuwa wanaumwa. Hii itasaidia kuepuka kupata vimelea sugu kutoka kwa mazao hayo
Penda kujisomea kuhusu mada za kiafya ili kufahamu matibabu ya nyumbani, dawa, magonjwa na kinga mbalimbali za maradhi
Kumbuka;
Matumizi ya dawa yasiyo sahihi hujumuisha matumizi kwa binadamu au wanyama wengine wa kufungwa
Unaweza kupata maambukizi ya vimelea sugu wa dawa aina fulani kutoka kwa mtu mwingine au mnyama, kisha ukashindwa kutibika kwa dawa inayofahamika kutibu vimelea au ugonjwa ulionao.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:41:55
Rejea za mada hii:
1. Antibiotic-resistance in Tanzania is an environmental problem. https://www.sciencedaily.com/releases/2020/01/200130081627.htm. Imechukuliwa 29.01.2021
2. Pius G. Horumpende, et al. Point prevalence survey of antimicrobial use in three hospitals in North-Eastern Tanzania. https://aricjournal.biomedcentral.com/articles/10.1186/s13756-020-00809-3. Imechukuliwa 29.01.2021
3. Nyambura Moremi, et al. Antimicrobial resistance pattern: a report of microbiological cultures at a tertiary hospital in Tanzania. https://bmcinfectdis.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12879-016-2082-1. Imechukuliwa 29.01.2021
4. Vijay B. Arumugham, et al. Third Generation Cephalosporins. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK549881/#. Imechukuliwa 29.01.2021
5. Diana Faini, et al. Burden of serious fungal infections in Tanzania. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/full/10.1111/myc.12390. Imechukuliwa 29.01.2021
6. CDC. About Antibiotic Resistance. https://www.cdc.gov/drugresistance/about.html#. Imechukuliwa 29.01.2021
7. WHO. Antibiotic resistance. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/antibiotic-resistance. Imechukuliwa 29.01.2021
8. OO Komolafe. Antibiotic resistance in bacteria - an emerging public health problem . https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3345436/. Imechukuliwa 29.01.2021
9. Vachon M. A report presented by George Soros Open Society Institute. New York: 1999. Harvard Medical School Report Warns of World Health Threat. https://www.researchgate.net/profile/Alasdair_Macgowan/publication/275402285_Surveillance_of_antimicrobial_resistance/links/56b9b89408ae3b658a8a055f/Surveillance-of-antimicrobial-resistance.pdf. Imechukuliwa 29.01.2021
10. Antimicrobials and Antibiotic-Resistant Bacteria: A Risk to the Environment and to Public Health. https://www.mdpi.com/2073-4441/12/12/3313/pdf. Imechukuliwa 29.01.2021
11. Lewis Marquez, et al. Prevalence and Therapeutic Challenges of Fungal Drug Resistance: Role for Plants in Drug Discovery. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7235788/. Imechukuliwa 29.01.2021
12. Michael A. Pfaller, MD. Antifungal Drug Resistance: Mechanisms, Epidemiology, and Consequences for Treatment. https://www.amjmed.com/article/S0002-9343%2811%2900913-2/fulltext. Imechukuliwa 29.01.2021
13. Dhara N. Shah, et al. Impact of Prior Inappropriate Fluconazole Dosing on Isolation of Fluconazole-Nonsusceptible Candida Species in Hospitalized Patients with Candidemia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3370796/. Imechukuliwa 29.01.2021
14. Ronen Ben-Ami, et al. Antibiotic Exposure as a Risk Factor for Fluconazole-Resistant Candida Bloodstream Infection. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3346668/. Imechukuliwa 29.01.2021
15. Thomas F. Patterson, et al. Practice Guidelines for the Diagnosis and Management of Aspergillosis: 2016 Update by the Infectious Diseases Society of America. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4967602/. Imechukuliwa 29.01.2021
16. David S. Perlin, et al. Update on Antifungal Drug Resistance. https://link.springer.com/article/10.1007/s40588-015-0015-1. Imechukuliwa 29.01.2021
17. MARTHA F. MUSHI, et all. Prevalence and factors associated with over-the-counter use of antifungal agents in Mwanza City, Tanzania. https://www.researchgate.net/publication/312667730_Prevalence_and_factor_associated_with_over-the-counter_use_of_antifungal_agents'_in_Mwanza_City_Tanzania. Imechukuliwa 29.01.2021
18. Diana Faini, et al. Burden of serious fungal infections in Tanzania. https://core.ac.uk/download/pdf/77101878.pdf. Imechukuliwa 29.01.2021