Imeandikwa na daktari wa ulyclinic
Vipele mshikizo kwenye Ngozi (skin Tag)
Vipele mshikizo kwenye Ngozi ni vipele vidogo vinavyoning’inia kwenye Ngozi.
Vipele hivi huwa havina shida yoyote, hupatikana kwenye maeneo ya shingo, kufuani, mgongoni, na kwapani. Hutokea sana kwa wanawake haswa wanaoongezeka uzito sana na watu wazima.
Vipele mshikozo huwa havisababishi maumivu mara nyingi, hata hivyo huweza kubadilika na kuleta maumivu endapo vimegusana na kitu chochote kama kidani, Mafuta, kupata msuguano n.k
Hutibiwaje?
Daktari wa Ngozi anaweza kutibu vipele mshikizo kwenye Ngozi kwa kufanya upasuaji mdogo wa kukata na kisu cha upasuaji au kutumia kisu cha umeme au njia ya kugandisha kipele au dawa.
Pata tiba kutoka kwa daktari wa ulyclinic kwa kubonyeza hapa, au kupiga nambaza simu chini ya tovuti hii.