Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Ijumaa, 27 Novemba 2020
Kipimo cha antijeni za H. pylori
Kipimo cha kutambua antijeni za H. pylori hutumika kuchunguza uwepo wa protini za bakteria Helicobacter pylori kwenye kinyesi. Uchunguzi huu humwezesha daktari kufahamu kama vidonda vya tumbo vimesababishwa na bakteria huyu au sababu zingine.
Maambukizi ya H.pylori ni maambukizi yanayotokana na bakteria maarufu kwa jina la helicobacter pylori. Maambukizi haya hutokea utotoni, hali ya maambukizi ni kubwa duniani kote hata kwenye nchi zilizoendelea ambapo maambukizi yamekuwa yakipungua kwa kasi.
Kipimo hiki ni nini?
Kipimo hiki huitwa H.pylori antigen test kwa sababu hupima uwepo wa protini za bakteria huyu zinazoitwa H.Pylori antigeni kwenye kinyesi. Antigen za H.Pylori huzalishwa na bakteria huyu kisha kutolewa kupitia kinyesi. Uwepo wa antigen kwenye kinyesi huashiria kuna uwepo wa bakteria huyu kwa wakati huo.
Umuhimu wa kipimo
Kipimo cha antibodies hufanyika sana na huweza tambua uwepo wa maambukizi kwenye damu, hata hivyo antibodies hukaa kwa muda wa miezi mpaka miaka kadhaa hata kama mtu ametumia dawa na kupona kabisa. Kipimo cha antigen ni kipimo pekee kinachoweza kutambua maambukizi yanayoendelea kwa sababu hutambua uwepo wa protini zinazozalisha na bakteria huyu kasha kutolewa kwenye kinyesi. Antigen hizi hupotea kwenye kinyesi mara tu baada ya matibabu kufanya kazi. Kipimo hiki pia huwa si kipimo vamizi kwa mwili kama kilivyo kipimo cha endoscopy na antibodies
Mgonjwa gani anapaswa kufanya kipimo hiki?
Watu wafuatao wanapaswa kupima kipimo hiki;
Wenye historia ya kuwa na vidonda vya tumbo na wamekuja na vidonda vya tumbo, isipokuwa endapo walithibitika kupona kabisa
Kuhisi gesi tumboni
Wagonjwa wenye vidonda vya tumbo ambao wanapata dalili za maumivu ya tumbo, kuhisi kushiba, kupungua uzito bila sababu, kichefuchefu/kutapika
Wagonjwa waliomaliza matibabu ya vidonda vya tumbo ili kuangalia kama maambukizi yameisha kwenye damu. Kipimo kitafanyika wiki 4 hadi 6 baada ya kuanza matibabu
Wagonjwa wenye ugonjwa wa MALT lymphoma
Wenye hatua za awali za saratani ya tumbo
Aina ya sampuli inayotakiwa
Sampuli inayotakiwa ni kinyesi kikavu cha asubuhi au kinyesi cha kwanza kabisa kama itawezekana.
Namna ya kukusanya sampuli
Utapewa kontaina safi ya kutunzia sampuli ili kuweka kiasi kidogo cha kinyesi kwa ajili ya kipimo.
Kila mtu anayekutwa na maambukizi anatakiwa huewa tiba, baada ya kumaliza tiba anatakiwa kupima tena ili kuthibitisha maambukizi yameisha
Kutokana na bakteria H.pyrol kuwa na usugu kwenye dawa nyingi, inashauriwa baada ya dozi kuisha upime kipimo hiki tena ili kuangalia kama mfumo wako wa tumbo umesasafishwa dhidi ya maambukizi haya.
Kwa wanawake
Ukusanyaji wa sampuli hautegemei jinsia
Kwa wanaume
Ukusanyaji wa sampuli hautegemei jinsia
Ukusanyaji wa sampuli kwa njia zingine
Hakuna mbadala wa sampuli hii
Utunzaji wa sampuli
Endapo sampuli inahitajika kutunzwa, itatunzwa kwenye kontena safi na kisha kuwekwa kwene jokofu katika joto linaloshauriwa ili isiharibibe. Utunzaji wa sampuli utafanyika pale endapo kipimo hakifanyiku muda huo.
Muda wa sampuli kuwa hai
Sampuli endapo imetunzwa kweye konteina na kuwekwa kwenye jokofu katika joto la mazingira (joto kati ya nyuzi joto 28-32) inaweza kudumu kwa muda wa siku 10-14 kabla ya kupimwa.
Kipimo hiki huwa na uwezo wa kuwa sahihi kwa asilimia 97 na husoma kwamba
Muda wa kupata majibu ya kipimo chako
Majibu hutoka ndani ya dakika 15 endapo umetumia kipimo cha haraka cha H.pylori.
Usomaji wa majbu
Kuna majibu aina mbili
Majibu chanya
Majibu chanya yataonyesha uwepo wa antigen za H.Pylori kwa kusoma mistari miwili kwenye sehemu ya control na sehemu ya test
Majibu hasi
Majibu hasi au negative yanaatikana pale endapo mstari mmoja tu wa control ndo umeonekana kwenye kipimo.
Ushauri wa msingi kwa mgonjwa
Endapo mgonjwa anatumia dawa jamii ya PPI kama omeprazole, lansoprazole au esomeprazole., antibayotiki na kampaundi zenye bismuth mjibu yake yanaweza kusoma negative ambapo kipimo kitakuwa ni cha uongo.
Utashauriwa na daktari wako au mtaalamu wa maabara kuzingatia mambo yafuatayo;
Kuacha kutumia dawa za antibayotiki na zenye kampaundi ya bismuth angalau kwa mwezi mmoja
Kuacha kutumia dawa jamii ya PPI angalau kwa wiki mbili
Kuacha kunywa maji au kula angalau saa moja kabla ya kipimo
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
Imeboreshwa,
8 Novemba 2021 10:35:49
Rejea za mada hii
1.MSD MANUAL Consumer Version. Helicobacter pylori (H. pylori) Testing. https://www.msdmanuals.com/home/multimedia/lab-tests/v42968411. Imechukuliwa 17.11.2020
Techlab. H. pylori Stool Antigen Testing. https://www.techlab.com/blog/techlab-publications/h-pylori/h-pylori-stool-antigen-testing/. Imechukuliwa 17.11.2020
Healthlinkbc. Helicobacter pylori test. https://www.healthlinkbc.ca/medical-tests/hw1531. Imechukuliwa 17.11.2020
Zeki Calik etal. Investigation of Helicobacter pylori antigen in stool samples of patients with upper gastrointestinal complaints. https://www.scielo.br/scielo.php?pid=S1517-83822016000100167&script=sci_arttext. Imechukuliwa 17.11.2020
Biopanda reagents. H. pylori Rapid Tests. https://www.biopanda.co.uk/php/products/rapid/infectious_diseases/h-pylori.php#. Imechukuliwa 17.11.2020
Helicobacter pylori Stool Antigen Test. https://www.clinicallabs.com.au/functional-pathology-old/practitioners/functional-tests-arterial/helicobacter-pylori-stool-antigen-test/. Imechukuliwa 17.11.2020
Tadashi Shimoyama. Stool antigen tests for the management of Helicobacter pylori infection. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3857440/. Imechukuliwa 17.11.2020
Geisinger Medical Laboratories/Geisinger Proven Diagnostics Test Catalog. H PYLORI AG STOOL. https://www.geisingermedicallabs.com/catalog/details.cfm?tid=61. Imechukuliwa 17.11.2020