Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 26 Novemba 2020
Kipimo cha Full blood picture- FBP
Kipimo cha picha nzima ya damu-FBP hufahamika kwa jina jingine la complete blood count-CBC huwa ni kipimo muhimu sana kwa dunia ya sasa kwani husaidia wataalamu wa afya kupata fununu za nini kinaendelea ndani ya mwili pamoja na kutambua magonjwa mbalimbali.
Toka kugunduliwa kwa kipimo cha FBP na matumizi ya kompyuta katika katika vipimo, kipimo hiki kimeboreshwa kwa kiasi kikubwa zaidi. Kwa sasa kipimo cha FBP huwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuchunguza na kutafsiri taarifa nyingi Zaidi kuhusu chembe za damu kuliko wakati wa zamani ambapo kilikuwa na uwezo wa kuangalia na kuona baadhi ya vitu.
Kipimo hiki ni nini?
Kipimo cha FBP hupima vitu vitu vifuatavyo;
Wingi wa HB
RCC
MCV
MCH
MCHC
Haematocrit (Hct) or PCV
Red cell distribution width (RDW)
Kiwango cha chembe nyeupe za damu-WBC
WBC differential
Kiwango cha chembe sahani za damu(Platelet count)
Kiwango cha Reticulocyte
Umuhimu wa kipimo
Je kipimo hiki kina msaada gani kwenye matibabu ya mgonjwa?
Kama ilivyoelezewa hapo juu, kipimo cha FBP kina uwezo wa kutambua vitu vingi kwenye damu na kwa namna hiyo huweza kutoa taarifa muhimu na kutambua aina tofauti ya madhaifu yaliyopo ndani ya mwili wa binadamu haswa yale yanaoonekana kwenye damu.
Kiwango cha chembe nyekundu za damu kitaonyesha kama mtu ana upungufu wa damu au la, kama upungufu wa damu upo, MCV itasaidia kutoa siri ya nini kinachosababisha upungufu wa damu.
Chembe nyeupe za damu huzidi kiwango cha kawaida mar azote endapo mtu ana maambukizi, diferential za chembe nyeupe za damu husaidia kusema pia ni nini kinachosababsha kuongezeka kwa chembe hizo nyeupe za damu. Mfano mtu akiwa na neutrophilia maanake ana maambukizi ya bakteria kwenye damu, akiwa na lymphocytosis itashuku kuwa ana maambukizi ya virusi kwenye damu lakini hata hivyo si mara zote.
Kiwango na umbo la chembe sahani za damu huweza kumaanisha madhara yanayotokea kwa sababu ya ugonjwa unaoendelea au kuwepo kwa ugonjwa unaosababisha madhaifu ya uzalishaji wa chembe hizo.
Ukusanyaji wa sampuli kwa njia zingine
Hakuna sampuli zingine zinazokusanywa kama mbadala wa damu kutoka kenye mishipa ya damu
Utunzaji wa sampuli
Damu hukusanywa kwenye chupa ya EDTA
Muda wa sampuli kuwa hai
Damu inatakiwa kufanyiwa kipimo ndani ya masaa manne (4) kama inawezekana ili kupata majibu sahihi.
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
Imeboreshwa,
8 Novemba 2021 11:57:58
Rejea za mada hii
Oxford Handbook of Clinical and Laboratory Investigation, 4th edition. 2018. By Drew Provan. ISBN 978–0–19–876653–7.
Full blood count. http://www.bbc.co.uk/health/talking/tests/blood_full_blood_count.shtml. Imechukuliwa 25.11.2020
Full blood count.http://www.rcpa.edu.au/pathman/full_blo.htm. Imechukuliwa 25.11.2020