top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

Jumatano, 3 Machi 2021

Kipimo cha homoni HCG kwenye mkojo

beta HCG ni homoni inayozalishwa na chembe zinazozunguka yai lililotungishwa. Homoni hii hupatikana kwenye damu na mkojo, hata hivyo hutambulika chini ya wiki mbili kwa kipimo cha damu na takribani wiki mbili au zaidi baada ya kupata mimba kwa kipimo cha mkojo.


Kipimo hiki ni nini?


Ni kipimo ambacho huweza kufanyika nyumbani kuchunguza kwa upimaji wa kiwango cha homoni HCG kwenye mkojo. Kipimo hiki hufanyika siku za awali kipindi mwanamke anapokosa hedhi.


Kipimo cha HCG hupima kiwango cha hormoni HCG kwenye mkojo au kwenye damu, homoni HCG hutengenezwa kwanye mwili wa mwanamke baada yai lililorutubishwa kujipandikiza katika sehemu ya ukuta wa mji wa mimba. Uzalishaji wa HCG hutokea siku sita baada ya kurutubishwa kwa yai. Kiwango hicho cha hormone huongezeka kila baada ya siku 2 au 3 kwa haraka zaidi.


Umuhimu wa kipimo


Umuhimu wa kipimo hiki ni rahisi kutumika ambacho kinaweza kufanyika nyumbani au maabara pia. HCG ni kipimo cha haraka zaidi katika upimaji wa ujauzito. Unaweza ukanunua stripu kwa ajili ya kupima ujauzito kwenye duka la dawa bila ya kuandikiwa na daktari. Gharama ya kipimo inategemea ubora wa kipimo chenyewe. Vipimo vya aina nyingi huwa siyo ghali.


Kama uko nyumbani unataka kupima kipimo hiki fanya yafuatayo;


Andaa mkojo wako kwenye chombo kisafi, unashauriwa zaidi kutumia mkojo wa asubuhi.

Zamisha sehemu ya kupimia kwenye chombo chenye mkojo kama mshare wa kipimo unavyoelekeza

Baada ya kufanya hivyo subiri kwa muda wa dakika chache ili kupata majibu (angalau dakika tano)


Maabara zinazoruhusiwa kufanya kipimo hiki


Maabara yoyote inaweza kupima kipimo hiki. Unashauriwa kupima hata nyumbani kwako kwa sababu ni kipimo rahisi na unaweza kukifanya mwenyewe


Mgonjwa gani anapaswa kufanya kipimo hiki?


Watu ambao wanaweza fanya kipimo hiki ni wafuatao;


  • Mwanamke aliepitisha siku moja baada ya kukosa kuona damu ya hedhi

  • Mwanamke mwenye kupata Maumivu ya tumbo la uzazi pamoja na kutokuona hedhi

  • Mwanamke mwenye kutokwa na matone ya damu ukeni

  • Mwanamke mwenye Uchovu bila sababu na huku anashiriki ngono

  • Mwanamke mwenye Mabadiliko katika matiti yanayoambatana na kutoona hedhi

  • Kichefuchefu, Kukojoa mara kwa mara, Kukosa choo, Mababdiriko katika uchangamfu, Maumivu ya kichwa na mgongo, Kizunguzungu pamoja na kutokuona damu ya hedhi


Aina ya sampuli inayotakiwa


Sampuli inayotakiwa ni mkojo. Mkojo mzuri zaidi ni ule mkojo wa kwanza wa asubuhi


Namna ya kukusanya sampuli


Ukusanyaji wa sampuli hufanyika kwa wanawake wenye dalili hizi za ujauzito ambapo hufanyika kwa kuchukua mkojo wa asubuhi wa nwanamke au hata mchana na kukusanya kwenye chombo kisafi kisicho na kemikali au uchafu.


Kwa wanawake

Kojolea kwenye chombo chako mkojo wa kwanza wa asubuhi kisha funika au pima


Kwa wanaume

Wanaume huwa hawafanyi kipimo hiki, isipokuwa endapo wanaweza kushika ujauzito kwa wale wenye jinsia mbili. Ukusanyaji wa sampuli endapo utahitajika, utakuwa sawa na kwa wanawake


Ukusanyaji wa sampuli kwa njia zingine

Hakuna sampuli mbadala inayoweza kukusanywa ili kufanya kipimo cha homoni HCG kwenye mkojo


Utunzaji wa sampuli


Sampuli inapaswa kutunzwa kwenye chombo safi chenye mfuniko


Muda wa sampuli kuwa hai


Sampuli ya mkojo endapo imetuzwa zaidi ya masaa 24 inaweza kupunguza ufanisi wa upimaji wa kipimo hiki cha ujauzito na kutoa majibu yasiyo sahihi


Muda wa kupata majibu ya kipimo chako


Majibu unaweza kuyapata ndani ya dakika 5 hadi 15 toka umepima. Endapo umepima kwenye maabara, muda utategemea foleni ya wagonjwa wanaosubiria majibu.


Usomaji wa majbu


Baada ya kufanya hivyo kusubiri kwa muda wa dakika 5 hadi 10 ili kuona majibu. Kwa msomaji wa Endapo kipimo hakionyeshi mstari wowote ule basi ujue kipimo hiko kinashida na utahitajika kurudia fanya kipimo au wasiliana na aliyekuuzia kipimo


Majibu chanya

mimba huonekana ipo endapo imetokea mistari miwili yenye rangi au alama ya chanya (+). Angalia kwenye pima kwa maelezo zaidi


Majibu hasi

Majibu, Mimba husemekana haipo endapo mstari umetokea mmoja kwenye alama C au endapo itasoma hasi (-). Angalia kwenye pima kwa maelezo zaidi


Ushauri wa msingi kwa mgonjwa


Unashauriwa kuwasiliana na daktari wako au mtaalamu wa maabara kwa ushauri zaidi endapo una maswali yoyote yale kuhusu vipimo hivi. Endapo umejikuta una mimba, mshirikishe mpenzi wako na hudhuria kliniki kwa ushauri zaidi na kufanyiwa vipimo muhimu.

ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.

ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.

Imeboreshwa,

8 Novemba 2021 10:41:11

Rejea za mada hii

  1. 1.Danielle Betz, et la. Human Chorionic Gonadotropin. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK532950/. Imechukuliwa 28.02.2021

  2. Jackie Anderson, et al. Early Pregnancy Diagnosis. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK556135/. Imechukuliwa 28.02.2021

  3. C. Gnoth, et al. Strips of Hope: Accuracy of Home Pregnancy Tests and New Developments. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4119102/. Imechukuliwa 28.02.2021

bottom of page