Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 26 Novemba 2020
Kipimo cha peripheral blood film
Kipimo hiki hutumia hadubini kutazama chembe nyekundu za damu zilizotiwa rangi (stain) ili kuona vema chembe nyekundu, nyeupe na chembe sahani za damu.
Kipimo hiki pia huweza kutambua vimelea kama malaria, trypanosomes walio kwenye damu au chembe za damu zilizo na maumbo tofauti na zingine.
Kipimo hiki ni nini?
Peripheral blood firm ni kipimo cha kuangalia picha ya chembe nyekundu za damu kwa kutumia hadubini
Umuhimu wa kipimo
Kipimo hiki huagiziwa kufanyika endapo kipimo cha FBP kimeonesha kuwepo kwa shida kwenye chembe nyeupe za damu mfano endapo umeshuku kuwepo kwa madhaifu ya chembe za damu.
Maabara zinazoruhusiwa kufanya kipimo hiki
​
Mgonjwa gani anapaswa kufanya kipimo hiki?
Kipimo hiki hufanyika ili kugundua matatizo yafuatayo;
Kuumwa manjano isiyofahamika kisababishi
Kuishiwa damu pasipo bila kisababishi kufahamika
Kupata michubuko kirahisi
Kupata dalili endelevu za mafua
Kupoteza uzito ghafla
Maumivu ya mifupa
Harara kwenye ngozi
Maambukizi makali au yasiyo na sababu
Aina ya sampuli inayotakiwa
Sampuli inaochukuliwa ni damu kutoka kwenye mishipa mikubwa ya damu haswa kwenye maungio ya mikono.
Namna ya kukusanya sampuli
Mtaalamu wa maabara atakufunga kifaa maalumu kwenye mkono ili kufanya mishipa ya damu ivimbe, baada ya kuona mishipa atatumia gozi iliyochovywa kwenye spirit ili kusafisha eneo hilo kabla ya kuingiza sindano kwenye kuvuta damu. Baada ya hapo mtaalamu atavuta damu kiasi kinachotosha na kuhifadhi wkenye chupa maalumu ya kukusanya sampuli. Utapata maumivu kiasi lakini yataisha baada ya muda.
Kwa wanawake
Ukusanyaji wa sampuli kwa ajili ya kipimo hiki hautegemei jinsia, hufanana kwa wanawake na wanaume
Kwa wanaume
Ukusanyaji wa sampuli kwa ajili ya kipimo hiki hautegemei jinsia, hufanana kwa wanawake na wanaume
Ukusanyaji wa sampuli kwa njia zingine
Sampuli inayotakiwa ni damu hivyo hukusanywa kutokakwenye mishipa ya vein
Utunzaji wa sampuli
Damu huhifadhiwa kwenye kichupa cha sampuli chenye EDTA
Muda wa sampuli kuwa hai
Baada ya kukusanya sampuli ya damu na kuweka kwenye kichupa cha sampuli, sampuli inatakiwa kupimwa ndnai ya masaa mawili ili kuleta majibu ya kweli. Kuchelewa kufanyia kazi sampuli kunaweza kuleta majibu ya uongo kuhusu kwamba una upungufu wa chembe sahani za damu(thrombocytopenia)
Muda wa kupata majibu ya kipimo chako
Inategemea aina ya hospitali na wingi wa wagonjwa, majibu unaweza kuyapata ndani ya lisaa moja
Usomaji wa majbu
Daktari atasoma majibu yako kuona sifa za chembe mbalimbali za damu na endapo kuna uwepo wa vimelea kwenye damu yako. Magonjwa yanayoweza kutambuliwa kwa kipimo hiki yameorodheshwa hapo chini.
Majibu chanya
Kipimo chanya kinaweza kutambua madhaifu ya chembe nyekundu za damu na madhaifu mengine mwilini kama;
Upungufu wa damu kutokana na upungufu wa madini chuma- iron deficiency anemia
Ugonjwa wa selli mundu- Sickle cell anemia
Hemolytic uremic syndrome
Ugonjwa wa Polycythemia rubra vera
Saratani ya damu
Saratani ya lymphoma
Maambukizi ya HIV
Maambukizi ya vimelea kama minyoo
Maambukizi ya fangasi
Ugonjwa wa Multiple myeloma
Upungufu wa chembe sahani za damu
Magonjwa ya figo, ini na tezi ya thyroid
Ushauri wa msingi kwa mgonjwa
Kipimo hiki kinaweza kutoa majibu yasiyo sahihi endapo unatumia dawa jamii ya NSAID, baadhi ya antibayotiki, dawa jamii ya glucocorticoid na vitamin. Hivyo hakikisha unamshirikisha daktari kwamba unatumia dawa hizi kabla ya kufanya kipimo hiki.
Endapo pia una ugonjwa wa hemophilia, huwa unaongezewa damu mara kwa mara na una saratani aina fulani usisite kutoa taarifa pia ili kusaidia mtaalamu wa afya kufanya kipimo na kukupa majibu sahihi.
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
Imeboreshwa,
8 Novemba 2021 10:55:38
Rejea za mada hii
1. Blood smear. (2015, February 24). labtestsonline.org/understanding/analytes/blood smear/tab/test/Imechukuliwa 24.11.2020
Blood smear. (n.d.)urmc.rochester.edu/encyclopedia/content.aspx ContentTypeID=167&ContentID=blood_smear. Imechukuliwa 24.11.2020
Peripheral blood smear - a review. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4415389/.Imechukuliwa 24.11.2020