Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 26 Novemba 2020
Kipimo cha Urine microscopy
Kipimo cha hadubini ya mkojo (Urine microscopy) ni kipimo cha uhakika, rahisi, cha gharama nafuu na kinatumika chini ya kiwango katika utambuzi wa maambukizi ya UTI. Kipimo cha biopsy ya mkojo pia kinaweza kufanyika kwa njia hii ya hadubini.
Kipimo hiki ni nini?
Mkojo wa katikati ya kukojoa, wa asubuhi, msafi na wa hivi punde uliokusanywa kwenye kopo la sampuli hufanyiwa centrifugation kabla ya kipimo kufanyika. Kwa majibu ya kipomo jinsi kinavyosomwa muulizie daktari wako au toa maoni kuhusu kuandika majibu hayo na yataandikwa hapa kwa jinsi utakavyohitaji kutumia.
Umuhimu wa kipimo
Kipimo hiki huwa na umuhimu kwa mtaalamu wa afya kuangalia matatizo mbalimbali ya figo na njia ya mkojo.
Mgonjwa gani anapaswa kufanya kipimo hiki?
Kwa mtu anayesemekana kuwa ana UTI
Kuhisiwa kuwa na acute glomerulonephritis
Kuhisiwa kuwa na ugonjwa wa kuferi figo kwa ghafla au tatizo sugu (acute or chronic renal failure
Kukojoa mkojo wenye damu (hematuria) pamoja au bila protini (proteinuria)
Kuhisiwa kuwa na saratani ya njia ya mkojo
Aina ya sampuli inayotakiwa
Sampuli inayokusanywa ni ile ya mkojo wa kati
Namna ya kukusanya sampuli
Ili kukusanya sampuli ya mkojo, chukua mkojo wa kati. Anza kukojoa kwanza na unapokuwa katikati ya kukojoa kinga mkojo huo kwenye kikopo kisha malizia kukojoa mkojo uliobaki.
Kwa wanawake
Ukusanyaji wa sampuli kwa mwanamke na mwanaume unafanana.
Kwa wanaume
Ukusanyaji wa sampuli kwa mwanaume na mwanamke unafanana.
Ukusanyaji wa sampuli kwa njia zingine
Kipimo hiki hutumia sampuli ya mkojo tu, hakuna sampuli mbadala wake
Utunzaji wa sampuli
Sampuli inapaswa kutunza kwenye kopo maalumu la kutunzia mkojo ambalo utapewa na mtaalamu wa afya
Muda wa sampuli kuwa hai
Baada ya kukusanya sampuli kwenye kopo, inatakiwa kufanyiwa kazi ndani ya saa moja ili kuepuka kupata majibu yasiyo sahihi.
Muda wa kupata majibu ya kipimo chako
Unaweza kupata majibu baada ya dakika 15 hadi 30, hata hivyo inategemea wingi wa wagonjwa na taratibu za hospitali
Usomaji wa majbu
Majibu yapo ya aina mbalimbali kutegemea ni nini kimeonekana kwenye mkojo wako
Majibu chanya
Majibu chanya hutokea pale edapo alichokifikiria daktari kimeonekana kwenye mkojo
Majibu hasi
Majibu hasi hutokea pale kama kilichofikiriwa na daktari hakijaonekana
Ushauri wa msingi kwa mgonjwa
Ni muhimu kuzingatia aina ya mkojo unaokusanya ili kupata majibu sahihi
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyte ile ya kiafya.
Imeboreshwa,
8 Novemba 2021 10:33:07
Rejea za mada hii
1.Oxford Handbook of Clinical and Laboratory Investigation, 4th edition. 2018. By Drew Provan. ISBN 978–0–19–876653–7.
http://www.bbc.co.uk/health/talking/tests/blood_full_blood_count.shtml