Imeandikwa na ULY CLINIC
Vyakula vinavyoondoa saratani
Saratani ni aina ya uvimbe unaotokea kwa binadamu na viumbe wengine. Janga hili limekuwa likiwadhuru watu wengi duniani na mpaka sasa hakuna tiba yake ingawa kuna aina za matibabu yapo kurejesha nyuma uvimbe au kufanya saratani isikue na kusambaa. Wagonjwa wengi hutambuliwa kuwa na saratani wakiwa kwenye hatua za mbaya ambapo wataalamu wa afya hupata changamoto katika matibabu. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kuna vihatarishi Fulani ambavyo mtu akiwa navyo anakuwa anajiweka kwenye hatari ya kupata saratani kwa mfano kuvuta sigara, kula vibaya n.k naam baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa kula vema husaidia katika kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya saratani.
Visa vya saratani vimekuwa vikiongezeka miaka na miaka, miaka ya hivi karibuni kumekuwa na visa vya saratani vingi sana. Tafiti zilizofanywa na WHO mwaka 2018 na mashirika mengine ya kiafya zinaonyesha taarifa za Kidunia kwamba, kati ya wanawake sita(6), mwanamke mmoja(1) huwa na saratani mmoja saratani na kati ya wanaume watano (5) mwanaume mmoja(1) huwa na saratani. Mwanaume mmoja kati ya wanaume 8, na mwanamke mmoja kati ya wanawake 11 hufa kwa saratani.
Baadhi ya watu wanaoishi katika mazingira Fulani duniani, wanaokula vyakula asilia na kutokuwa kwenye vihatarishi wameonekana kutopata saratani. Hata hivyo watu hao wakihama mazingira waliyopo na kujiweka kwenye vihatarishi hupata saratani.
Makala hii ni mahususi kukuelimisha kuhusu saratani, namna ya kujikinga na saratani na namna ya kutibu saratani kutokana na tafiti ambazo zimefanyika.
Saratani ni nini?
Ili kuelewa kwa urahisi kuhusu saratani ni vema tukajifunza kuhusu namna mwili unavyofanya ukarabati endapo kuna shida imetokea;
Kwa kawaida mwili wa binadamu na wanyama wenngine huwa na uwezo wa kujitibu na kujiponya wenyewe mara kunapotokea udhaifu wowote ule mwilini. Mfano mzuri, endapo mtu amejikata na kitu, sehemu iliyokatwa hutoa taarifa zinazosafiri kwa mfumo wa umeme kupitia kwenye damu na mishipa ya fahamu kwenda kwenye chembe asilia (stem cell) kuziambia chembe hizo kuna shida imetokea na hivyo ziende kwenye eneo la tukio ili kufanya ukarabati. Chembe asilia zinapofika katika eneo la tukio huwa na uwezo wa kubadilika kuwa nyenzo yoyote inayohitajika katika uponyaji, kwa mfano endapo mshipa wa damu umepasuka, chembe hizo zitabadilika na kutengeneza kuta za mshipa wa damu na endapo ngozi imepasuka, chembe hizo zitabadilika na kutengeneza seli za ngozi ili kufanya ukarabati kwenye eneo lenye shida. Mara baada ya ukarabati kukamilika, taarifa maalumu hutolewa tena katika mfumo wa umeme kuamuru kusimama kwa tukio la ukarabati.
Endapo ukarabati haujasimama ni nini kitatokea
Endapo ukarabati haujasimamishwa, tukio la ukarabati huwa linaendelea,kutoka katika mfano wa hapo juu, endapo ukarabati wa kuweka kiraka kwenye ngozi iliyokatwa unaendelea, kiraka hicho kitaendelea kukua siku hadi siku na hivyo kuleta uvimbe katika eneo hilo linalofanyiwa ukarabati. mfano uvimbe wa keloidi n.k. uvimbe unaotengenezwa katika eneo hili mara nyingi hufanana na tishu katika eneo uliopo. Uvimbe unaofanana na eneo uliopo huitwa uvimbe wa kawaida(uvimbe usio saratani) kwa kitiba huitwa benign tumor, wakati uvimbe ambao haufanani na chembe asilia katika eneo hilo huitwa uvimbe wa saratani unaofahamika kitiba kama malignant tumor.
Kwanini uvimbe wa saratani huwa tofauti na vimbe zingine?
Vimbe za saratani huwa tofauti na tishu zingine kwa kuwa huwa na tabia ya kuzalisha chembe(tishu) zilizo tofauti na mazingira zilizopo na pia uzalishaji wake huwa hausikii amri ya kusimamisha uzalishaji na ukuzaji au kutofuata utaratibu asilia wa kufa kwa chembe zilizozalishwa.
Chembe za saratani huwa na ukuta nje ambao umetengenezwa kwa chaji hasi, na chembe za ulinzi ambazo huweza fanya kazi ya kula chembe za saratani huwa na chaji chanya pia. Kama inavyofahamika chaji zinazofanana huwa haziwezi kugusana, hii ndio sababu kwanini chembe za saratani huwa haziwezi kukua
Vyakula vya kukukinga na kuponya saratani
Vyakula gani vina vitamin B17 kwa wingi?
Mbegu za
-
Apricot
-
Tufaa(apple)
-
Matunda damu (Plum)
-
Peasi
-
Matunda madogomadogo
-
Mtama
-
Chia
-
Buckwheat
-
Almond
Mboga na viubgo kama
-
Karoti
-
Celery
-
Mbaazi
-
Maharagwe aina nyingi isipokuwa maharagwe ya soya
Endapo unataka kutumia vyakula hivi kama kinga, ni vema ukavitumia kila siku. Ili kuweza kutumia kama dawa au tiba, ni vema ukatumia vidonge au dawa ya maji ya kuchoma. Dawa zilizotengenezwa huwa na kiwango cha dawa kinachofaa, endapo utazitumia hautapata maudhi madogo ambayo huonekana sana kwa watu wanaotumia kiini cha dawa kutoka kwenye chakula(mbegu) au kunywa dawa ya kidonge.
Mfano matumizi ya mbegu za tufaa kwa wingi huweza kuleta sumu mwilini. Matumizi kwa kiwango kianchotakiwa huwa hakidhuru mwili.
Namna gani vyakula hivi huyeyusha saratani
-
Mwili huvunja kemikali ya latrine kuwa hydrogen cyanide, benzaldehyde na prusin
-
Kampaundi ya hydrogen cyanide ni kampaundi mahususi inayopambana na saratani.
-
Vimeng’enya mbalimbali ndani ya mwili hubadili kampaundi ya hydrogen cyanide kuwa molecule inayoitwa thiocyanate, ambayo ina uwezo wa kutibu shinikizo la damu na kufyonza saratani.
Imeboreshwa 14.01.2021
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri zaidi na tiba kabla ya kuchuku a hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii.
Rejea za mada hii;
-
National cancer institute .https://www.cancer.gov/about-cancer/understanding/what-is-cancer. Imechukuliwa 12.01.2020
-
Latest global cancer data. Cancer burden rises to 18.1 million new cases and 9.6 million cancer deaths in 2018.https://www.who.int/cancer/PRGlobocanFinal.pdf. Imechukuliwa 12.01.2020
-
Shwayta Kukreti, PhD etal. Characterization of Metabolic Differences between Benign and Malignant Tumors: High-Spectral-Resolution Diffuse Optical Spectroscopy1. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2797652/. Imechukuliwa 12.01.2020
-
Global cancer statistics 2018: GLOBOCAN estimates of incidence and mortality worldwide for 36 cancers in 185 countries. https://acsjournals.onlinelibrary.wiley.com/doi/10.3322/caac.21492. https://www.who.int/cancer/resources/incidences/en/. Imechukuliwa 12.01.2020
-
Cancer Statistics. https://www.cancer.gov/about-cancer/understanding/statistics. Imechukuliwa 12.01.2020
-
Cancer Prevalence. https://www.cdc.gov/cancer/uscs/technical_notes/stat_methods/prevalence.htm. Imechukuliwa 12.01.2020
-
Cancer cell morphology. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK9553/. Imechukuliwa 12.01.20201
-
Kim U, Baumler A, Carruthers C, Bichat K. Proc. Natl. Acad. Sci. U.S. 1975;72:1012–1018.
-
TUMOR CELL MORPHOLOGY. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK9553/#ch3.r100. Imechukuliwa 12.01.2020