top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

Ni  wakati gani utarajie maziwa kutoka baada ya kujifungua?

Unajua umuhimu wa kunyonyesha? Maziwa ya mama huwa na kiwango sawia cha virutubisho na chakula anavyotakiwa kupata mtoto. Maziwa ya mama ni rahisi kumengenywa kuliko maziwa mengine. Na maziwa ya mama huwa na kinga ya mwili kwa ajili ya kupambana na maradhi na hivyo huimarisha kinga ya mwili ya mtoto.  Hata hiyo kunyonyesha kunaweza kukufanya upungue uzito na kupata faida nyingi, tumia vidokezo hivi kujua uanzie wapi.

 

 

Kama wewe umejifungua mtoto kwa mara ya kwanza inachukua siku 3 hadi nne ili maziwa yaanze kutoka, lakini kama umejifungua zaidi ya mara moja basi huweza kuchukua siku chache zaidi.

 

Siku zako za mwisho wa ujauzito yaani siku kadhaa kabla ya kujifungua,  utahisi kuwa matiti yako yamejaa ikiwa ni dalili ya kuonyesha maziwa yanazalishwa.

Kiwango cha Homoni inayotoa taarifa kwamba maziwa yaanze kuzalishwa(prolactine) huongezeka kila sikukipindi chote cha ujauzito na hata hivyo huzuia kufanya kazi ipasavyo kutokana na homoni pingamizi zilizo katika kondo. Mara baada ya kujifungua homoni hii ya prolactin hufanya kazi ipasavyo na kuyaambia maziwa yatoke.

Maziwa ya kwanza ya mama huwa mazito nay a njano huitwa kwa jina jingine colostrums, maziwa haya huwa na kiwango kikubwa cha madini , protini, mafuta ambaya na kinga ya mwili.

Mara baada ya mtoto kuzaliwa anatakiwa kuwekwa kwenye ziwa ili apate kunyonya, labda uwe na tatizo ambalo umeshauriwa na daktari wako usimnyonyeshe.

 

Sababu zinazoweza kufanya maziwa yakachelewa kutoka mara baada ya upasuaji ni;

 

  • Mtoto alizaliwa kwa shida au ulifanyiwa upasuaji. Wakati huu inaweza kusababisha maziwa yakatoka siku ya 4 hadi 5 ili maziwa yatoke.

  • Una kisukari kinachohitaji matibabu ya homoni ya insulin au ulipata kisukari  cha ujauzito. Matiti huhitaji homoni hii ili kuzalisha maziwa, hivyo hupambana na mwili kutumia kiwango kidogo kilichopo na kusababisha uzalishaji mdogo wa maziwa.

  • Kipande cha kondo kimebaki kwenye kizazi. Kumbuka kondo la nyuma huwa linatoa homoni inayopingana na prolactine kuzalisha maziwa. Hata hivyo utaendelea kutokwa na damu kama ishala ya kwamba kizazi chako hakiko safi. Unaweza kupimwa na ultrasound ili kuangalia ndani ya kizazi na kujua kilichopo ndani. Baada ya hapo utatibiwa matibabu sahihi.

 

Omba msaada mara moja

Kusoma kuhusu makala hii ni jambo la kwanza la kufanya, na kutenda ni jambo linalofuata- saa la kwanza unapoanza kunyonyesha lazima uombe msaada wa kuelekezwa

 

Nesi wa kinamama wajawazito au mtaalamu wa hospitali anayejua mambo ya kunyonyesha huweza kukupa vidokezo vya namna ya kunyonyesha. Atakuonyesha namna gani ya kumweka  mtoto wakati wa kunyonya na kuhakikisha ananyonya vizuri.

 

Daktari wako ama daktari wa mtoto anaweza kukupa vidokezo vya namna gani ya kumnyonyesha mtoto.

 

Endapo unataka kumkatisha m toto asiendelee kunyonya basi weka kidole kisafi kwenye kona yam domo wake wakati ananyonya na kisha ataendelea kunyonya kidole. Kwa kufanya hivyo unazuia mtoto akiumize chuchu zako.

                                                                                                                                              

Mwache mtoto anyonye itoshavyo

Wiki za kwanza , vichanga hunyonya kila baada ya masaa 2 hadi 3, mtazame mtoto anapoonyesha dalili za awali za kupata njaa kama kupigwa butwaa, kuchoka, kujinyonya na kuonyesha miendo ya kutaka kunyonya

Mwache mtoto anyonye sana mpaka uhisi titi limekuwa laini na hili huchukua dakika 15 hadi 20 kwenye ziwa moja.

 

Pia kumbuka hakuna muda maalumu.

Mtoto anapomaliza mda huo mbadilishe kwenda ziwa jingine, kama ameshiba atashindwa kunyonya  na kama ana njaa atanyonya sana. Kama kashiba basi mwache na wakati ukifika wa kunyonya muweke katika ziwa la pili ambalo hakunyonya awali. Kama mtoto hanyonyi ziwa la pili basi hakikisha unakamua ziwa hilo ili kupunguza maziwa na uzito ndani na kulinda uzalishaji maziwa.

Achana na chupa ya kunyonyeshea

Baadhi ya watoto hufurahia kunyonya  maziwa kwenye chupa. Unaweza kutumia chupa hizi lakini usizitumie mapema sana kwani huweza kufanya zoezi la unyonyeshaji kuwa gumu kwa sababu kunyonya kwenye ziwa ni tofauti na kunyonya kwenye chupa.

Chagua kuishi maisha ya kiafya

 

Maisha ya kiafya wakati wa kunyonyesha yanatakiwa yaendelee kama vile ilivyokuwa katika kipindi cha ujauzito. Mfano;

 

  • Kula chakula bora. Ili kupata nguvu, jikite katika kula vyakula vyenye  maji kwa wingi kama matunda kwa wingi, mboga za majani na nafaka zisizokobolewa. Unaweza kushauriwa kutumia virutubisho dawa na mtaalamu wako wa afya.

  • Kunywa maji ya kutosha . maji, juisi, maziwa huweza kuufanya mwili ukawa na maji ya kutosha. Kiasi kidogo cha kahawa kinaweza kutumiwa kipindi hiki-lakini chunguza kama kiwango cha kahawa unayotumia kinaingilia usingizi wa kichanga. Kama umekunywa pombe basi usimnyonyeshe mtoto kwa mda wa masaa 2 tangu ulipokunywa.

  • Pumzika muda mrefu iwezekanavyo. Kama unaweza, lala mtoto anapolala.

  • Usivute tumbaku/sigara. Kuvuta tumbaku wakati wa kunyonyesha humweka mtoto hatarini kwenye kemikali ya nicotine ambayo inaweza kusababisha matatizo ya usingizi kwa mtoto. Pia kuvuta sigara karibu na mtoto huongeza hatari ya mtoto kufa ghafla, na magonjwa ya mfumo wa hewa.

  • Kuwa makini na madawa. Madawa mengi huwa salama kunywa endapo unanyonyesha, lakini ni jambo la msingi kumuuliza mtaalamu wako wa afya kuhusu usalama wa dawa hizo wakati wa kunyonyesha ili akuhakikishie usalama kwanza

Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020

bottom of page