Matamshi (noo-troe-PEE-nee-uh)
Imeandikwa namadaktari wa uly clinic
Utangulizi
Ni kuwa na kiwango cha chini kuliko cha kawaida cha chembe za neutrophil- neutrophili ni seli zilizo mwilini zinazopambana na maradhi ya maambukizi ya bacteria.
Kwa watu wazima ili aweze semekana ana kiwango cha chini cha seli za neutrophili kiwango hicho kinatakiwa kuwa chini ya 1,500 kwa kila micro lita ya damu. Kwa watoto inategemea na umri wake.
Baadhi ya watu wamezaliwa na kukua wakiwa na chembe nyeupe za neutrophil kwa kiwango cha chini sana lakini hawapo katika hatari ya kupata mambukizi. Kwa watu kama hao upungufu huo/kiwangi hiki huwa hakina tatizo. Kiwango chini ya 1,000 ama chini cell 500 kwa kila micro lita siku zote huitwa Upungufu wa neutrophili, ambapo bacteria rafiki walio kwenye kinywa ama mfumo wa chakula wanaweza kukusabababishia maambukizi makali.
Dalili
-
Kuhisi mwili umechoka
-
Kuishiwa pumzi haraka wakati unaamka, au kufanya kazi
-
mapigo ya moyo kwenda kasi ama kupiga kusiko kawaida
-
Kufifia kwa rangi ya ngozi kuwa nyeupe(kwenye macho) ama viganya,na nyayo
-
maambukizi ya mara kwa mara, ama kutopona haraka
-
Kuchubuka kwa haraka au kusikoelezeka
-
Kutokwa damu puani ama kwenye fizi
-
Kutokwa damu kwa muda mrefu ukijikata
-
Harara kwenye ngozi
-
Kizunguzungu