top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

1 Machi 2021 09:44:50

Kutomeng'enywa kwa chakula- Dyspepsia

Kutomeng'enywa kwa chakula- Dyspepsia

Dispepsia ni hali ya kutomeng’enywa kwa chakula tumboni kinachopelekea hisia za tumbo kujaa gesi, kichefu chefu, kiungulia, kupotea kwa hamu ya kula maumivu ya tumbo ya kunyonga, na hisia za tumbo kujaa.


Mara nyingi huamshwa na vyakula vyenye viungo kwa wingi, vyenye nyuzilishe kwa wingi na kafeine. Endapo unapata dispepsia isiyotokana na sababu ya kipatholojia, hii humaanisha kuna shida kwenye mfumo wa umeng’enyaji wa chakula.


Dispepsia huweza kusabaishwa na matatizo ya mfumo wat umbo, mapafu, moyo na matumizi ya baadhi ya dawa au hali ya akili, kula sana na kula haraka haraka. Kutokea kwa dyspepsia hutokana na kubadilika kwa uzalishaji wa tindikali tumboni unaopelekea dalili hii.


Neno dispepsia kilatini hufahamika kama dyspepsia


Visababishi


  • Ugonjwa wa cholelithiasis au mawe kweney kibofu cha nyongo

  • Ugonjwa wa kusinyaa kwa ini (cirrhosis)

  • Vidonda vya tumbo

  • Kuvurugika kwa tumbo

  • Henia ya hiatal

  • Embolism ya pulmonary

  • Yuremia

  • Kifua kikuu

  • Ugonjwa wa homa ya ini

  • Saratani katika mfumo wa chakula

  • Kupanuliwa kwa tumbo

  • Kufeli kwa moyo

  • Upasuaji unaohusisha mfumo wa chakula

  • Matumizi ya dawa za NSAIDS kama aspirini, dawa jamii ya diuretics, antibayotiki, dawa za kushusha presha, dawa za corticosteroid na zngine

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

7 Februari 2022 19:29:36

Rejea za mada hii

bottom of page