top of page

Mwandishi:

Dkt. Sima D, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Acarbose ni dawa inayotumika kushusha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wa kisukari aina ya pili. Dawa hii hutumika kuzuia ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu mara baada ya kula. Acarbose hutumika pamoja na mazoezi na lishe sahihi kwa wagonjwa wa kisukari ili kudhibiti ongezeko la sukari kwenye damu.


Upekee wa dawa hii ni kutosababishi kushuka kwa sukari kupita kiasi kama itatumika yenyewe.


Majina ya kibiashara ya acarbose

Acarbose hufahamika kwa majina mengine ya kibiashara kama;

  • Precose

  • Miglitol(Glyset)

  • Voglibose

  • Glucobay

  • Glucor

  • Glumida

  • Prandase


Fomula ya kikemikali

C25H43NO18


Muonekano

Ni dawa ya kidonge. Umbo na rangi vinaweza kutofautiana kutegemeana na kiwanda kinachozaliza.


Dozi zinazopatikana

Hupatikana kwa vidonge vya:-

  • Miligramu 25

  • Miligramu 50

  • Miligramu 100


Namna ya kutumia

  • Meza kama utakavyo elekezwa na daktari wako.

  • Unashauriwa kumeza dakika 30 kabla ya kula chakula.


Namna inavyofanya kazi mwilini

Acarbose ni aina ya oligosaccharide inayofanya kazi ya mashindano kwa kuzuia vimeng’enya vya alpha-glucosidase kuvunja wanga kuwa monosaccharides, kupunguza ufyonzwaji wa kabohaidreti na hivyo kupunguza kiwango cha homon insulin baada ya kula. Acarbose hutakiwa kutumika pamoja na wanga ili iweze kufanya kazi vema, hivyo mtumiaji anapaswa kutumia baada ya kula chakula mara tatu kwa siku.


Umetaboli wa dawa

  • Dawa hii huchakatwa na mwili ndani ya utumbo mdogo wa chakula

  • Huanza kufanya kazi baada ya saa 1

  • Taka mwili ya mabaki ya dawa ya acarbose hutolewa kwenye kinyesi (asilimia 51) na mkojo(asilimia 34)


Wagonjwa wasiopaswa kutumia dawa hii

  • Wagonjwa walioferi figo

  • Wagonjwa wenye mzio na dawa ya acarbose

  • Wagonjwa waliowahi kupata dayabetiki ketoasidosisi

  • Wagonjwa waliopata tatizo la kuziba utumbo

  • Wagonjwa wenye vidonda vya tumbo

  • Wagonjwa wenye figo iliyoferi


Tahadhari wakati wa kutumia dawa ya acarbose

  • Bado hakuna tafiti za kutosha kuelezea uhusiano wa dawa ya acarbose na hatari zake katika mfumo wa moyo na mishipa ya damu.

  • Kama ikitumiwa na insulin au sulfonylurea inaweza kushusha sukari kupita kiasi.

  • Inaweza kushindwa kufanya kazi vizuri kwa wagonjwa wenye maambbukizi au homa, upasuaji mkubwa au majeraha makubwa.


Dawa zenye muingiliano na acarbose

Dawa zisizopaswa kutumika kwa pamoja


Hakuna orodha ya dawa zisizopaswa kutumika kwa pamoja na acarbose


Dawa zenye muingiliano mkali


Dawa zifuatazo hazipaswi kutumika pamoja na acarbose, unawezakutumia mbadala wa dawa ambazo hazina mwingiliano;


  • Ethanol

  • Pramlintide


Dawa zenye muingiliano na acarbose ambazo zikitumika pamoja mgonjwa anapaswa kuwa kwenye uchunguzi wa karibu wa daktari;


  • Albiglutide

  • Aripiprazole

  • Asenapine

  • Atazanavir

  • Bitter melon

  • Cinnamon

  • Ciprofloxacin

  • Clozapine

  • Darunavir

  • Digoxin

  • Dulaglutide

  • Exenatide kimiminika cha kuchoma

  • Exenatide kimiminika cha kuchoma

  • Fleroxacin

  • Fosamprenavir

  • Gemifloxacin

  • Iloperidone

  • Indinavir

  • Insulin aspart

  • Insulin aspart protamine/insulin aspart

  • Insulin degludec

  • Insulin degludec/insulin aspart

  • Insulin detemir

  • Insulin glargine

  • Insulin glulisine

  • Insulin inhaled

  • Insulin isophane human/insulin regular human

  • Insulin lispro

  • Insulin lispro protamine/insulin lispro

  • Insulin nph

  • Insulin regular human

  • Ketotifen, ya macho

  • Letermovir

  • Levofloxacin

  • Liraglutide

  • Lopinavir

  • Lurasidone

  • Marijuana

  • Mecasermin

  • Mipomersen

  • Moxifloxacin

  • Nelfinavir

  • Ofloxacin

  • Olanzapine

  • Opuntia ficus indica

  • Paliperidone

  • Pancrelipase

  • Quetiapine

  • Risperidone

  • Ritonavir

  • Saquinavir

  • Shark cartilage

  • Somapacitan

  • Sulfamethoxypyridazine

  • Tipranavir

  • Triamcinolone acetonide kimiminika cha kuchoma

  • Xipamide

  • Ziprasidone


Dawa zenye muingilian mdogo usio na mashiko


  • Activated charcoal

  • Agrimony

  • American ginseng

  • Amitriptyline

  • Amoxapine

  • Anamu

  • Bendroflumethiazide

  • Budesonide

  • Chlorothiazide

  • Chlorthalidone

  • Chromium

  • Clomipramine

  • Clonidine

  • Cornsilk

  • Cortisone

  • Cyclopenthiazide

  • Damiana

  • Danazol

  • Deflazacort

  • Desipramine

  • Devil's claw

  • Dexamethasone

  • Doxepin

  • Elderberry

  • Eucalyptus

  • Fludrocortisone

  • Fluoxymesterone

  • Forskolin

  • Fo-ti

  • Gotu kola

  • Guanfacine

  • Gymnema

  • Horse chestnut seed

  • Hydrochlorothiazide

  • Hydrocortisone

  • Imipramine

  • Indapamide

  • Isoniazid

  • Juniper

  • Lofepramine

  • Lycopus

  • Maitake

  • Maprotiline

  • Mesterolone

  • Methyclothiazide

  • Methylprednisolone

  • Methyltestosterone

  • Metolazone

  • Nettle

  • Nortriptyline

  • Ofloxacin

  • Oxandrolone

  • Oxymetholone

  • Pegvisomant

  • Potassium acid phosphate

  • Potassium chloride

  • Potassium citrate

  • Prednisolone

  • Prednisone

  • Protriptyline

  • Sage

  • Stevia

  • Testosterone

  • Testosterone ya kupaka

  • Testosterone ya kuweka kinywani

  • Tongkat ali

  • Trazodone

  • Trimipramine

  • Vanadium


Matumizi wakati wa ujauzito

Inaweza kutumiwa kwa mama mjamzito ila hakuna tafiti za kutosha kuhusu mdahara yake.


Matumizi wakati wa kunyonyesha

Epuka kwa kipindi cha kunyonyesha.


Maudhi ya dawa

  • Maumivu ya tumbo

  • Tumbo kujaa gesi

  • Kujamba

  • Kuharisha

  • Kuwashwa ngozi

  • Ongezeko la vimeng'enya vya ini kwenye damu

  • Huweza kusababisha kuferi kwa ini

  • Kuvimba

  • Thrombocytopenia

  • Pneumatosis cystoides intestinalis


17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Acarbose

Imeboreshwa,

25 Septemba 2021, 06:46:40

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page