top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Ibandronate ni dawa kizazi cha tatu cha bisphosphonate yenye nitrogen inayotumika kukinga na kutibu magonjwa ya mifupa dhaifu kwa wanawake walio kwenye komahedhi.



Majina ya kibiashara ya Ibandronate

Majina mengine ya Ibandronate ni;


  • Bovina

  • Bondronat

  • Boniva

  • Iasibon


Ibandronate hufahamika pia kama;

  • Ibandronate monosodium monohydrate

  • Ibandronate sodium

  • Ibandronate sodium hydrate

  • Ibandronate sodium monohydrate

  • Ibandronic acid (as sodium ibandronate)

  • Ibandronic acid sodium salt

  • Ibandronic acid sodium salt monohydrate

  • Ibandronic sodium monohydrate

  • Sodium ibandronate


Dawa zilizo kundi moja na Ibandronate

Dawa zilizo kundi moja na Ibandronate ni ;

  • Risedronate

  • Etidronate

  • Alendronate

  • Pamidronate

  • Zoledronate



Fomu na uzito wa Ibandronate

Ibandronate ina uzito ufuatao;

  • Kidonge chenye uzito wa 150mg

  • Kimiminika cha kuchoma kwa sindano chenye uzito wa 1mg/1ml (3ml)


Ibandronate hutibu nini?

  • Hutumika kutibu udhaifu wa mifupa kwa wanawake walio koma hedhi

  • Hutumika kukinga udhaifu wa mifupa kwa wanawake walio koma hedhi



Namna Ibandronate inavyoweza kufanya kazi

Mara baada ya kuingia kwenye damu ibandronate acid hujishikiza kwenye hydroxyapatite ya mifupa. Ufyonzwaji kalisiamu kwenye mifupa hutengeneza mazingira ya utindikali katika mifupa na kupelekea kuachiwa kwa ibandronate acid kutoka kwenye mifupa. Ibandronate acid hufyonzwa na chembe osteoclasts kisha kuachiwa kwenye saitosol ya osteoclasts inayofanya kazi ya kufyonza mifupa. Kuzuiwa ufanyaji kazi wa osteoclasts husababisha kupungua kwa ufyonzwaji wa kalisiiamu ndani ya mifupa na hivyo kufanya mifupa iwe imara kutokana na kutopoteza madini hayo.



Ufyonzwaji wa dawa

Asilimia 0.63 ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye damu kama ikitumika kwa kunywa.


Mwingiliano wa Ibandronate na chakula

Ili kutopunguza ufyonzwaji wa dawa hii, kunywa kwa kutumia maji tu na si vimiminika vya aina nyingine au juisi. Tumia pasipo chakula maana chakula pia hupunguza ufyonzwaji wake



Wagonjwa wasiopaswa kutumia Ibandronate

  • Wagonjwa wenye mzio wa Ibandronate.

  • Wagonjwa wenye mzio wa dawa jamii ya bisphosphonate derivatives.



Utoaji taka wa Ibandronate mwilini

Asilimia hamsini hadi sitini (50%-60%) hutolewa kwa njia ya mkojo, dawa ambayo haijafyonzwa hutolewa mwilini kupitia kinyesi.


Matumizi ya Ibandronate kwa mama mjamzito

Dawa hii hairuhusiwi kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa. Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa kwa mama mjamzito na kwa mtoto aliye tumboni hivyo hairuhusiwi kwa mama mjamzito.




Matumizi ya Ibandronate mama anayenyonyesha

Dawa hii hairuhusiwi kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa. Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo hairuhusiwi kutumiwa na mama anayenyonysha.



Dawa zenye muingiliano na Ibandronate

Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Ibandronate;


  • Hakuna Orodha ya dawa yenye muingiliano mkali na Ibandronate.


Dawa zinazoweza kutumika na Ibandronate chini ya uangalizi;


  • Aluminum hydroxide

  • Calcium acetate

  • Calcium carbonate

  • Calcium chloride

  • Calcium citrate

  • Calcium gluconate

  • Carbonyl iron

  • Deferasirox

  • Ferric maltol

  • Ferrous fumarate

  • Ferrous gluconate

  • Ferrous sulfate

  • Iron dextran complex

  • Iron sucrose

  • Magnesium supplement

  • Polysaccharide iron

  • Rose hips

  • Selenium

  • Sodium bicarbonate

  • Sodium citrate/citric acid

  • Sodium sulfate/?magnesium sulfate/potassium chloride

  • Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate

  • Voclosporin

  • Zinc


Dawa zenye mwingiliano mdogo na Ibandronate;


  • Entecavir

  • Foscarnet

  • Magnesium chloride

  • Magnesium citrate

  • Magnesium hydroxide

  • Magnesium oxide

  • Magnesium sulfate

  • Teriparatide


Maudhi ya Ibandronate

  • Maumivu ya tumbo

  • Maumivu ya kichwa

  • Maumivu ya mifupa, misuli na viungio vya mwili

  • Degedege

  • Homa

  • Mgongo kuuma

  • Kizunguzungu

  • Nimonia

  • Kuharisha

  • Bronchaitiz

  • Maambukizi kwenye mfumo wa juu wa hewa

Ufanye nini endapo utasahau kutumia dozi yako?

Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi kwa wakati sahihi wasiliana na daktari ili aweze kukupangia muda sahihi wa kutumia dozi inayofata.

17 Januari 2026, 15:31:06

Dawa Ibandronate

Imeboreshwa,

24 Septemba 2021, 18:15:33

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

  1. Brunton LL, Hilal-Dandan R, Knollmann BC. Goodman & Gilman's: The Pharmacological Basis of Therapeutics. 14th ed. New York: McGraw-Hill; 2023. Antihypertensive agents.

  2. Sweetman SC, editor. Martindale: The Complete Drug Reference. 40th ed. London: Pharmaceutical Press; 2020. Methyldopa.

  3. McEvoy GK, editor. AHFS Drug Information 2024. Bethesda (MD): ASHP; 2024. Methyldopa.

  4. World Health Organization. WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. Geneva: WHO; 2023.

  5. Drugs.com. Methyldopa [Internet]. 2024 [cited 2025 Jun 5].

  6. Micromedex (IBM Watson). Methyldopa Drug Monograph. 2024.

bottom of page