top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter B, M

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

kirusi mumps-ulyclinic

Meropenem ni antibayotiki yenye uwanja mpana wa kuua bakteria wa gramu hasi na chanya iliyo kwenye kundi la carbapenem.


Meropenem hufanya kazi kwa kujipenyeza haraka kwenye kuta za bakteria na hivyo kuingilia uzalishaji wa vijenzi muhimu vya bakteria kitendo kinachopelekea kifo chake.


Bakteria wanaouliwa na dawa

Hutumika yenyewe katika matibabu ya maradhi yanayosababishwa na bakteria wafuatao wanaodhuriwa na dawa:

 

Fomu ya dawa


Hupatikana kama chumvi ya soiam kloride ambayo huchanganywa na maji na kutumika kwa kuchoma na sindano.


Maambukizi tata bakteria kwenye ngozi

Kutokana na Bakteria

 • Staphylococcus aureus (wanaozalisha na wasiozaisha b-lactamase na wale wanaodhuriwa tu na methicillin-Streptococcus pyogenes

 • Streptococcus agalactiae

 • Streptococci kundi la viridans

 • Enterococcus faecalis isipokuwa waliosugu kwenye vancomycin

 • Pseudomonas aeruginosa

 • Escherichia coli

 • Proteus mirabilis

 • Bacteroides fragilis

 • Spishi za Peptostreptococcus


Homa ya kidole tumbo na peritoniamu

Kutokana na bakteria

 • Streptococci kundi la Viridans

 • Escherichia coli

 • Klebsiella pneumoniae

 • Pseudomonas aeruginosa

 • Bacteroides fragilis

 • Thetaiotaomicron

 • Spishi za Peptostreptococcus

 

Kutibu homa ya uti wa mgongo
 • Kutokana na bakteria

 • Streptococcus pneumoniae

 • Haemophilus influenzae (wanaozalisha na wasiozalisha b-lactamase

 • Neisseria meningitidis.

 

Maambukizi tata ya UTI

Hutumika katika matibabu hayo ikiwa imeungana na dawa nyingine ya Vaborbactam  na muunganiko huo hufahamika kwa jina la vabomere.

  

Namna inavyofanya kazi

Uwezo wa kitiba wa meropenem hutokana na uwezo wake wa kuzuia ujenzi wa kuta ya bakteria. Dawa hii hupenya haraka na kuingia ndani ya kuta za bakteria jamii ya gramu hasi na chanya na kuzuia ujenzi wa vijenzi vya ukuta huo na hivyo bakteria kufa.

 

Ufyonzaji wa dawa

Dawa hii hutumika kwa kuchoma, hivyo asilimia 100 hupatikana kwenye damu kwa ajili ya kufanya kazi.

 

Nusu maisha ya dawa

 • Ni saa 1 kwa watu wazima na watoto wa miaka 2 na kuendelea na wenye figo zinavyofanya kazi kawaida.

 • Ni saa 1.5 kwa watoto wa miezi 3 hadi miaka 2

 

Utoaji wa dawa mwilini

Asilimia 70 ya dawa iliyochomwa hutolewa kwa njia ya mkojo ikiwa haijafanyiwa umetaboli katika kipindi cha masaa 12 na baada ya hapo kiwango chake kwenye mkojo huwa kidogo.

 

Usumu wa dawa

Katika tafiti, matumizi ya dawa hii kwa kiasi kikubwa kinachozidi miligramu kwa kilo 2200-4000 huambatana na madhara/maudhi yafuatayo:

 •  Kupotea usawia wakati wa mwendo

 • Kuishiwa pumzi

 • Degedege

 • Kifo

 

Dawa zenye mwingiliano na meropenem

 • Chanjo hai ya BCG

 • Chanjo ya Kipindupindu

 • Divalproex sodium

 • Microbiota oral

 • Probenecid

 • typhoid vaccine live

 • valproic acid

 

Uangalizi wa karibu unatakiwa kufanyika endapo zitatumika na dawa hizi
 • bazedoxifene/conjugated estrogens

 • conjugated estrogens

 • conjugated estrogens, vaginal

 • dienogest/estradiol valerate

 • digoxin

 • estradiol

 • estrogens conjugated synthetic

 • estrogens esterified

 • estropipate

 • mestranol

 • sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid

 

Dawa zenye mwingiliano mdogo sana
 • balsalazide

 • biotin

 • niacin

 • pantothenic acid

 • pyridoxine

 • pyridoxine (Antidote)

 • thiamine

 • vitamin K1 (phytonadione)

 

Meropenem na pombe

Meropenem hapaswi kutumika pamoja na pombe kwa kuwa pombe huongeza maudhi yake na kudhuru utendaji kazi wa akili na kuweza kusabaisha usingizi wa kupindukia.

 

Maudhi ya dawa

 

Maudhi yanayotokea sana
 • Maumivu ya kichwa

 • Homa ya michomo kwenye mshipa wa damu uliochomwa dawa

 • Kuhara

 • Aleji

 • Kichefuchefu

 • Ongezeko la vimeng’enya vya ini ALT, AST

 • Homa

 • Kushuka kwa kiwango cha potasiamu kwenye damu

 

Maudhi yanayotokea kwa nadra
 • Upungufu wa chembe nyeupe za damu

 • Homa ya koo

 • Maumivu ya kifuLeukopenia

 • Fangasi ukeni

 • Fangasi kwenye koo

 • Ongezeko la kimeng’enya creatinine phosphokinase

 • Kukosa hamu ya kula

 • Ongezeko la potasiamu kwenye damu

 • Kupungua kwa glukosi kwenye damu

 • Kizunguzungu

 • Kutetemeka

 • Ganzi

 • Weweseko

 • Uchovu wa kupindukia

 • Kukosa usingizi

 • Azotemia

 • Kuferi kwa figo

 • Kuganda kwa damu mishipa ya ndnai ya vena

 • Kushuka kwa shinikizo la damu

 • Maumivu ya mshipa wa damu

 

13 Juni 2023 19:18:46

Dawa Meropenem

Imeboreshwa,

13 Juni 2023 19:18:46

Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.

Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.

Rejea za mada hii:

 1. Bäck SE, et al. Age dependence of renal function: clearance of iohexol and p-amino hippurate in healthy males. Scand J Clin Lab Invest. 1989 Nov;49(7):641–646.

 2. Bax RP, et al. The pharmacokinetics of meropenem in volunteers. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):311–320.

 3. Burman LA, et al. Pharmacokinetics of meropenem and its metabolite ICI 213,689 in healthy subjects with known renal metabolism of imipenem. J Antimicrob Chemother. 1991 Feb;27(2):219–224.

 4. Christensson BA, et al. Pharmacokinetics of meropenem in subjects with various degrees of renal impairment. Antimicrob Agents Chemother. 1992 Jul;36(7):1532–1537. 

 5. DAVIES DF, SHOCK NW. Age changes in glomerular filtration rate, effective renal plasma flow, and tubular excretory capacity in adult males. J Clin Invest. 1950 May;29(5):496–507.

 6. Douglas JG, et al. The pharmacokinetics of cefuroxime in the elderly. J Antimicrob Chemother. 1980 Jul;6(4):543–549.

 7. Granerus G, et al. Reference values for 51Cr-EDTA clearance as a measure of glomerular filtration rate. Scand J Clin Lab Invest. 1981 Oct;41(6):611–616.

 8. Harrison MP, et al. The disposition and metabolism of meropenem in laboratory animals and man. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):265–277. 

 9. Jones RN, et al. In-vitro studies of meropenem. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):9–29. 

 10. Krutzén E, et al. Plasma clearance of a new contrast agent, iohexol: a method for the assessment of glomerular filtration rate. J Lab Clin Med. 1984 Dec;104(6):955–961.

 11. Ljungberg B, et al. Pharmacokinetics of antimicrobial agents in the elderly. Rev Infect Dis. 1987 Mar-Apr;9(2):250–264.

bottom of page