Mwandishi:
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD

Risedronic acid ni dawa kizazi cha tatu cha bisphosphonate inayotumika katika matibabu ya baadhi ya matatizo ya udhaifu wa mifupa pamoja na ugonjwa wa paget. Hufanya kazi kwa kuzuia ufyozwaji wa madini kutoka kewnye mifupa.
Majina mengine ya Risedronate
Majina mengine ya Risedronate ni;
Actonel
Atelvia
Actonel with calcium
Risedronate ipo kundi gani la dawa?
Risedronate ni dawa iliyo katika kundi la Calcium metabolism modifiers; Bisphosphonate Derivatives.
Dawa zilizo kundi moja na Risedronate
Dawa zilizo kundi moja na Risedronate ni;
Alendronate
Ibandronate
Etidronate
Pamidronate
Zoledronate
Fomu ya dawa ya Risedronate
Dawa hii ipo katika fomu ya;
Kidonge
Uzito wa dawa ya Risedronate
Risedronate ina uzito ufuatao;
Vidonge
5mg
30mg
35mg
150mg
Risedronate hutibu nini?
Hutumika kutibu madhaifu ya mifupa kwa wanawake walio koma hedhi
Hutumika kutibu madhaifu ya mifupa yaliyoamshwa na dawa za glucocorticoid
Hutumika kukinga madhaifu ya mifupa kwa wanaotumia dawa jamii ya Glucocorticoid
Hutumika kutibu magonjwa ya Paget
Hutumika kutibu magonjwa ya mifupa kwa wanaume
Hutumika kutibu Osteogenesis imperfecta
Namna Risedronate inavyoweza kufanya kazi
Dawa jamii ya Bisphosphonates kama ikiwa pamoja na Risedronate hufyonzwa na chembe na mifupa kisha kujishikiza kwenye hydroxyapatite. Kujishikiza huku husababisha kutengeneza mazingira ya utindikali na kuzalishwa kwa bisphosphonate inayosaidia chembe za osteoclast kuzuia kufyonzwa kwa kwa madini kalisiamu yaliyo kwenye mifupa.
Ufozwaji wa dawa
Ufozwaji wa dawa hii hufanyika vizuri ikiingia kwenye mfumo wa chakula mtu akiwa hajala.
Mwingiliano wa Risedronate na chakula
Unapotumia dawa hii unapasa kutumia pia vitamin D
Zuia kutumia pamoja na ayani za multivalent
Dawa au vyakuka kama kalisiamu, dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali na zile zenye Iyani za divalent huingilia ufyonzwaji wa dawa hii
Tumia bila chakula
Kunywa kwa kutumia maji tu
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Risedronate
Wagonjwa wenye mzio wa Risedronate.
Wagonjwa ambao calcium ipo chini (Hypocalcemia).
Utoaji taka za Risedronate mwilini
Asilimia themanini na tano (85%) ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na dawa ambayo haijafozwa hutolewa kwa haja kubwa.
Matumizi ya Risedronate kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii ina madhara kwa mama na mtoto aliyeko tumboni hivyo haitakiwi kutumika wakati wa ujauzito.
Matumizi ya Risedronate mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo hairuhusiwi kwa mama anayenyonyesha.
Dawa zenye muingiliano na Risedronate
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Risedronate;
Cimetidine
Famotidine
Ibuprofen/famotidine
Nizatidine
Dawa zinazoweza kutumika na Risedronate chini ya uangalizi;
Aluminum hydroxide
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Deferasirox
Magnesium supplement
Selenium
Sodium bicarbonate
Sodium citrate/citric acid
Sodium sulfate/?magnesium sulfate/potassium chloride
Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate
Sodium zirconium cyclosilicate
Voclosporin
Zinc
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Risedronate;
Dexlansoprazole
Entecavir
Food
Foscarnet
Teriparatide
Maudhi ya Risedronate;
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya mifupa, misuli na viungio vya mwili
Shinikizo la dawa kuwa juu
Vipele
Kichefuchefu
Haja kubwa kuwa ngumu
Kuharisha
Mafua
Kutapika
Kupata msongo wa mawazo
Kifua kuuma
Kizunguzungu
Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi yako ulipoamka usitumie baadae kama umesahau kutumia dozi na dozi ya mwezi unaofata ni zaidi ya siku saba tumia dozi uliyosahau siku inayofuata ukiamka tuu kisha endelea na dozi inayofuata kwa muda sahihi. Usitumie zaidi ya dozi moja ndani ya siku saba. Kama umesahau kutumia dozi na dozi inayofuata ni chini ya siku saba usitumie dozi hiyo uliyosahau.
13 Juni 2023, 19:18:46
Dawa Risedronate
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021, 07:10:45
Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.
Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.
Rejea za mada hii:
Bäck SE, et al. Age dependence of renal function: clearance of iohexol and p-amino hippurate in healthy males. Scand J Clin Lab Invest. 1989 Nov;49(7):641–646.
Bax RP, et al. The pharmacokinetics of meropenem in volunteers. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):311–320.
Burman LA, et al. Pharmacokinetics of meropenem and its metabolite ICI 213,689 in healthy subjects with known renal metabolism of imipenem. J Antimicrob Chemother. 1991 Feb;27(2):219–224.
Christensson BA, et al. Pharmacokinetics of meropenem in subjects with various degrees of renal impairment. Antimicrob Agents Chemother. 1992 Jul;36(7):1532–1537.
DAVIES DF, SHOCK NW. Age changes in glomerular filtration rate, effective renal plasma flow, and tubular excretory capacity in adult males. J Clin Invest. 1950 May;29(5):496–507.
Douglas JG, et al. The pharmacokinetics of cefuroxime in the elderly. J Antimicrob Chemother. 1980 Jul;6(4):543–549.
Granerus G, et al. Reference values for 51Cr-EDTA clearance as a measure of glomerular filtration rate. Scand J Clin Lab Invest. 1981 Oct;41(6):611–616.
Harrison MP, et al. The disposition and metabolism of meropenem in laboratory animals and man. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):265–277.
Jones RN, et al. In-vitro studies of meropenem. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):9–29.
Krutzén E, et al. Plasma clearance of a new contrast agent, iohexol: a method for the assessment of glomerular filtration rate. J Lab Clin Med. 1984 Dec;104(6):955–961.
Ljungberg B, et al. Pharmacokinetics of antimicrobial agents in the elderly. Rev Infect Dis. 1987 Mar-Apr;9(2):250–264.