Mwandishi:
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD

Tiludronate ni dawa ya kizazi cha kwanza cha bisphosphonate inayofanana na etidronic acid na clodronic acid, hutumika kutibu ugonjwa wa Paget kwenye mifupa.
Majina mengine ya Tiludronate
Majina mengine ya Tiludronate ni;
Skelid
Dawa zilizo kundi moja na Tiludronate
Dawa zilizo kundi moja na Tiludronate ni ;
Alendronate
Ibandronate
Etidronate
Pamidronate
Zoledronate
Fomu na uzito wa Tiludronate
Dawa hii ipo katika fomu ya kidonge chenye uzito wa 200mg
Tiludronate hutibu nini?
Hutumika kutibu ugonjwa wa mifupa kwa mgonjwa mwenye kiwango cha alkaline phosphatase zaidi ya ≥2 mara mbili ya kiwango cha juu cha kawaida kinachoweza kuleta madhara ya hapo mbeleni
Namna Tiludronate inavyoweza kufanya kazi
Dawa jamii ya Bisphosphonates kama ikiwa pamoja na tiludronate hufyonzwa na chembe na mifupa kisha kujishikiza kwenye hydroxyapatite. Kujishikiza huku husababisha kutengeneza mazingira ya utindikali na kuzalishwa kwa bisphosphonate inayosaidia chembe za osteoclast kuzuia kufyonzwa kwa kwa madini kalisiamu yaliyo kwenye mifupa.
Ufozwaji wa dawa
Asilimia 2 hadi 11 ya dawa hufyonzwa na kuingia kewnye damu kwa ajili ya kuleta madhara ya kitiba kama mtu atatumia kidonge chenye uzito wa 400mg
Mwingiliano wa Tiludronate na chakula
Dawa hii inatakiwa kutumika mtu akiwa hajala kwani chakula kinapunguza ufozwaji wa dawa.
Utoaji taka wa Tiludronate mwilini
Asilimia 60 ya dawa hutolewa kwa njia ya mkojo bila kufanyiwa umetaboli.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Tiludronate
Wagonjwa wenye mzio wa Tiludronate.
Wagonjwa ambao kalisium ipo chini (Hypocalcemia).
Dawa zenye muingiliano na Tiludronate
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Tiludronate;
Hakuna orodha ya dawa yenye mwingiliano mkali na Tiludronate hivyo kufanya zisitumike kwa pamoja.
Dawa zinazoweza kutumika na Tiludronate chini ya uangalizi;
Aluminum hydroxide
Calcium acetate
Calcium carbonate
Calcium chloride
Calcium citrate
Calcium gluconate
Deferasirox
Magnesium supplement
Selenium
Sodium bicarbonate
Sodium citrate/citric acid
Sodium sulfate/?magnesium sulfate/potassium chloride
Sodium sulfate/potassium sulfate/magnesium sulfate
Trimagnesium citrate anhydrous
Voclosporin
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Tiludronate;
Aspirin
Aspirin rectal
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Foscarnet
Indomethacin
Teriparatide
Matumizi ya Tiludronate kwa mama mjamzito
Tahadhari inatakiwa wakati mama anatumia dawa hii hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama mjamzito na mtoto.
Matumizi ya Tiludronate mama anayenyonyesha
Hakuna tafiti zinazoonesha madhara ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha, kwa mtoto na katika uzalishwaji wa maziwa hivyo taadhari inatakiwa ichukuliwe wakati mama anatumia dawa hii.
Maudhi ya Tiludronate
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya mifupa, misuli na viungio vya mwili
Shinikizo la dawa kuwa juu
Harara kwenye ngozi
Kichefuchefu
Haja kubwa kuwa ngumu
Kuharisha
Mafua
Kutapika
Kupata msongo wa mawazo
Kifua kuuma
Kizunguzungu
Sinusaitiz
Rinaitiz
Tumbo kujaa gesi
Kutokwa jasho
Ufanye nini kama umesahau kutumia dozi yako?
Ni muhimu sana kutumia dozi yako kwa wakati sahihi. Kama umesahau kutumia dozi yako kwa wakati sahihi muulize daktari wako muda sahihi wa kutumia dozi inayofuata.
13 Juni 2023 19:18:46
Dawa Tiludronate
Imeboreshwa,
25 Septemba 2021 07:35:06
Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.
Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.
Rejea za mada hii:
Bäck SE, et al. Age dependence of renal function: clearance of iohexol and p-amino hippurate in healthy males. Scand J Clin Lab Invest. 1989 Nov;49(7):641–646.
Bax RP, et al. The pharmacokinetics of meropenem in volunteers. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):311–320.
Burman LA, et al. Pharmacokinetics of meropenem and its metabolite ICI 213,689 in healthy subjects with known renal metabolism of imipenem. J Antimicrob Chemother. 1991 Feb;27(2):219–224.
Christensson BA, et al. Pharmacokinetics of meropenem in subjects with various degrees of renal impairment. Antimicrob Agents Chemother. 1992 Jul;36(7):1532–1537.
DAVIES DF, SHOCK NW. Age changes in glomerular filtration rate, effective renal plasma flow, and tubular excretory capacity in adult males. J Clin Invest. 1950 May;29(5):496–507.
Douglas JG, et al. The pharmacokinetics of cefuroxime in the elderly. J Antimicrob Chemother. 1980 Jul;6(4):543–549.
Granerus G, et al. Reference values for 51Cr-EDTA clearance as a measure of glomerular filtration rate. Scand J Clin Lab Invest. 1981 Oct;41(6):611–616.
Harrison MP, et al. The disposition and metabolism of meropenem in laboratory animals and man. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):265–277.
Jones RN, et al. In-vitro studies of meropenem. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):9–29.
Krutzén E, et al. Plasma clearance of a new contrast agent, iohexol: a method for the assessment of glomerular filtration rate. J Lab Clin Med. 1984 Dec;104(6):955–961.
Ljungberg B, et al. Pharmacokinetics of antimicrobial agents in the elderly. Rev Infect Dis. 1987 Mar-Apr;9(2):250–264.