Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya miguu kuwaka moto
9 Juni 2021 14:59:04
Miguu kuwaka moto katika Makala hii inajumuisha pia tatizo la kanyagio kuwaka moto, ambalo huelezewa kuwa ni hisia za joto, kuchomachoma kwa miguu, au kanyagio. Hali hii huweza kutokea wakati wa usiku au wakati wote haswa kwa watu wa makamo lakini haimaanishi kuwa haiwezi kutokea kwa watu walio na umri mdogo. Makala hii imezungumzia kuhusu dawa za tatizo la miguu kuwaka moto, kusoma zaidi kuhusu tatizo la miguu kuwaka moto, dalili na uchunguzi, nenda kwenye makala nyingine ndani ya tovuti ya ulyclinic.
Orodha ya dawa zinazotumika kutibu dalili za miguu kuwaka moto
Orodha ya dawa zinazotumika kwa ajili ya miguu kuwaka moto ambazo daktari wako anaweza kukuandikia (mojawapo) kulingana na kisababishi kilichofahamika kwako ni;
Amitriptyline
Carbamazepine (tegretol)
Desipramine (norpramin)
Duloxetine (cymbalta)
Gabapentin (neurontin)
Pregabalin (lyrica)
Topiramate (topamax)
Venlafaxine (effexor xr)
Neuroton
Kumbuka
Miguu kuwaka moto ni dalili/kiashiria cha tatizo fulani ndani ya mwili, upatapo dalili hii hakikisha unaonana na daktari wako kwa uchunguzi ili kupata tiba halisi. Dawa nyingi zilizoorodheshwa hapo juu huficha dalili kwa muda mfupi bila kutibu tatizo tatizo.
Visababishi vya miguu kuwaka moto
Miguu kuwaka moto husababishwa sana na Kisukari au matumizi ya kupindukia ya pombe. Visababishi vingine ambavyo kila kimoja kinamatibabu yake ni;
Uremia kutokana na ugonjwa sugu wa figo
Magonjwa ya mishipa midogo ya fahamu
Upungufu wa vitamin haswa vitamin B6 na B12)
Upungufu wa homon za tezi shingo
Ugonjwa wa lyme
UKIMWI
Maudhi ya dawa kama dawa za saratani, UKIMWI, isoniazid, amiodarone, isoniazid, metformin na zingine
Kunywa dozi kubwa ya vitamin B6,
Amyloid polyneuropathy
Erythromelalgia
Sumu kutokana na madini ya risasi, zebaki na aseniki
Michomo kwenye mishipa ya damu kutokana na maambukizi
Sarcoidosis
Sindromu ya Guillain-Barre (GBS)
Madhaifumengine ya mishipa ya fahamu
Unapata wapi maelezo zaidi kuhusu miguu kuwaka moto?
Soma kwa kubofya linki zinazofuata
Majina mengine ya dawa za miguu kuwaka moto
Majina mengine yanayomaanisha shida ile ile ya miguu kuwaka moto ni;
Dawa ya Kanyagio kuwaka moto
Dawa ya Miguu kuchoma choma
Dawa ya Miguu kuwa ya moto