top of page

Ugonjwa na dawa

Kurasa hii utajifunza kuhusu dawa na ugonjwa unaotibiwa na dawa hiyo. Wasiliana na daktari wako kabla ya kutumia dawa yoyotee ile ili kuepuka madhara na usugu wa dawa mwilini mwako. Kumbuka siku zote kuwa dawa ni sumu kwenye mwili wako endapo haitatumika bila ushauri wa daktari

Dawa za fangasi usoni

Dawa za fangasi usoni

Fangasi wa usoni kwa wanawake na watoto hutokea sana kwenye mdomo wa juu. Kwa mwanaume maambukizi yakitokea kwenye maeneo ya ndevu huitwa Tinea Barbae, matibabu huhusisha matumizi ya viuaji fangasi.

Dawa za kutibu haja ngumu

Dawa za kutibu haja ngumu

Konstipesheni hutibiwa kwa dawa za kuongeza nyuzinyuzi kwenye mlo na kulainisha haja ngumu ambayo tayari ipo kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

Dawa za maumivu ya U.T.I

Dawa za maumivu ya U.T.I

Phenazopyridine hutumika baada ya kula chakula, kutibu maumivu ya mkojo wakati wa kukojoa kwa wagonjwa weye UTI.

Dawa za maumivu ya majeraha

Dawa za maumivu ya majeraha

Hufanya kazi kwa kuzuia mfumo wa kinga ya mwili kuzalisha kemikali zinazosababisha maumivu. Dawa hizi ni za kuzuia dalili tu na hazitibu tatizo.

Dawa za fangasi wa ulimi

Dawa za fangasi wa ulimi

Matibabu ya fangasi wa mdomoni na kwenye ulimi huhusisha matumizi ya dawa za kuua fangasi zinazoitwa antifangus. Uchaguzi wa dawa hutegemea aina ya fangasi na mwitikio wake kwenye dawa.

bottom of page