Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya minyoo
18 Juni 2021 13:58:42
Minyoo huitwa kwa jina jingine la helminthis ni vimelea wenye uwezo wa kuingia na kufanya makazi ndani ya mwili na pia kusababisha maradhi. Minyoo ina uwezo wa kuishi tumboni, kwenye ngozi, Mishipa ya damu, ini na hata kwenye moyo. Dawa zinazotumika kutibu minyoo hufanya kazi yake kwa kuzuia minyoo kupata chakula au kuwafanya wapooze na hivyo kufa. Dawa nyingi haziwezi kuua mayai ya minyoo yaliyopo mwilini.
Orodha ya dawa za minyoo
Miongoni mwa dawa zinazotumika kutibu minyoo ni;
Levamisole
Niclosamide
Praziquantel
Albendazole
Diethylcarbamazine
Ivermectin
Tiabendazole
Maudhi ya dawa za minyoo
Dawa za minyoo huwa na maudhi kiasi ambayo ni;
Maumivu ya tumbo
Kuendedha
Kichefuchefu
Hisia za kuumwa
Wapi unaweza kupata taarifa zingine zaidi kuhusu dawa za minyoo?
Kupata maelezo ya ziada ya kila dawa ya minyoo, itafute kwenye makala za uly clinic kupitia kiboksi cha 'Tafuta chochote hapa...' juu ya tovuti hii
Majina mengine ya dawa ya minyoo
Majina mengine yanayomaanisha dawa za minyoo ni;
Dawa za kutibu minyoo
Dawa ya minyoo kwa watoto
Dawa ya kutibu minyoo wakati wa ujauzito