top of page
Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Imeboreshwa:
5 Desemba 2025, 08:00:00
Image-empty-state.png

Dawa ya uchafu ukeni kutokana na fangasi

Dawa za kutibu maambukizi ya fangasi ambao husababisha kutokwa na uchafu mweupe ukeni usio na harufu ambao huambatana na muwasho zimeorodheshwa kwa kina kwenye makala hii kama dawa za kunywa na dawa za kupaka.


Dawa za kunywa kwa fangasi wa ukeni
  • Fluconazole


Dawa za kupaka kwa fangasi wa ukeni
  • Boric acid

  • Nystatin

  • Flucytosine

  • Clotrimazole

  • Butoconazole

  • Terconazole

  • Fluconazole

  • Miconazole

  • Tioconazole


Majina mengine ya dawa za fangasi ukeni ni nini?

Baadhi ya watu hutumia majina yafuatayo kumaanisha dawa za fangasi ukeni. Dawa za muwasho ukeni, dawa za uchafu mweupe ukeni, dawa ya utokwa na maziwa ukeni, dawa ya kuzuia muwasho wa uke. Hata hivyo ni vema ukasoma kuhusu visababishi vya muwasho ukeni kisha kufahamu ni shida gani inayokusumbua.


Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara



Maswali yaliyoulizwa mara kwa mara


1. Je, fangasi wa ukeni hupona bila dawa?

Kwa baadhi ya wanawake, dalili ndogo zinaweza kupungua zenyewe, lakini mara nyingi fangasi huhitaji dawa za kupaka au kunywa ili kupona kikamilifu.

2. Je, ninaweza kutumia dawa hizi nikiwa mjamzito?

Wanawake wajawazito wanapaswa kutumia dawa za kupaka tu kama clotrimazole au miconazole. Dawa za kunywa kama fluconazole hazipendekezwi bila usimamizi wa daktari.

3. Je, fangasi ukeni huambukizwa kwa partner wangu?

Kawaida fangasi si ugonjwa wa zinaa, lakini wanaume wanaweza kupata muwasho au wekundu kwenye uume baada ya kujamiiana na mwanamke aliye na fangasi.

4. Je, ni dalili zipi tofauti kati ya fangasi na UTI?

Fangasi: muwasho, uchafu mweupe, wekundu.UTI: maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara nyingi, mkojo kunuka. Hakuna uchafu mweupe.

5. Je, naweza kupata fangasi kwa kutumia pedi au sabuni nyingi?

Ndiyo. Pedi zenye harufu kali, sabuni nyingi, na kujisafisha ndani ya uke huongeza hatari ya fangasi.

6. Je, fangasi hurudia mara kwa mara?

Ndiyo, hasa kwa wanawake wenye kisukari kisichodhibitiwa, wanaotumia antibiotics mara kwa mara, au wenye kinga dhaifu.

7. Ni muda gani dawa za fangasi huchukua kufanya kazi?

Dawa za kupaka hufanya kazi ndani ya siku 1–7 kulingana na aina yake. Fluconazole ya kumeza mara nyingi huanza kupunguza dalili ndani ya saa 24–48.

8. Je, ninaweza kujamiiana nikiwa na fangasi?

Inashauriwa kuepuka ngono hadi dalili zipone ili kuepuka maumivu na kuzuia kusambaza muwasho kwa mwenza.

9. Je, chakula kinaweza kuongeza au kupunguza fangasi?

Vyakula vyenye sukari nyingi huongeza uwezekano wa kurudia kwa fangasi. Ulaji wa mtindi wenye vimelea rafiki unaweza kusaidia kuweka usawa wa vijidudu ukeni.

10. Ni wakati gani ni lazima nione daktari?

Mwone daktari ikiwa:

  • Dalili hazipungui baada ya kutumia dawa

  • Unapata fangasi mara zaidi ya 4 kwa mwaka

  • Una maumivu makali au una ujauzito

  • Hujawahi kupata uchunguzi wa kitaalamu kabla

Majina mengine ya dawa za fangasi ukeni

Watu hutumia majina mbalimbali kurejelea dawa hizi, kama vile:

  • Dawa za muwasho ukeni

  • Dawa za uchafu mweupe ukeni

  • Dawa ya uchafu mweupe ukeni

  • Dawa ya kutokwa na maziwa ukeni

  • Dawa ya kuzuia muwasho wa uke


Ni muhimu kufahamu chanzo cha tatizo kwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu. Tumia dawa baada ya kupata ushauri wa daktari ili kuhakikisha zinawiana na tatizo na hali yako ya afya.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeandikwa
7 Juni 2021, 15:01:42
1. CDC. Vaginal Candidiasis. https://www.cdc.gov/fungal/diseases/candidiasis/genital/index.html. Imechukuliwa 06.06.2021

2. Peter G. Pappas, et al. Clinical Practice Guideline for the Management of Candidiasis: 2016 Update by the Infectious Diseases Society of America. https://academic.oup.com/cid/article/62/4/e1/2462830. Imechukuliwa 06.06.2021

3. Vulvovaginal Candidiasis. https://www.cdc.gov/std/tg2015/candidiasis.htm. Imechukuliwa 06.06.2021
bottom of page