top of page
Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD

Dawa ya uchafu unaotoka ukeni

7 Juni 2021 14:53:18
Image-empty-state.png

Uchafu ukeni mara nyingi husababishwa na maambukizi ya fangasi au magonjwa ya zinaa. Kutambua nini kinasababisha uchafu ukeni ni lazima kufahamu dalili zinazoambatana na kutokwa na uchafu ukeni ikiwa pamoja na rangi ya uchafu.


Visababishi vya uchafu ukeni


Matatizo yanayoweza kusababisha kutokwa na uchafu ukeni ni pamoja na;


  • Maambukizi ya fangasi ukeni

  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa

  • oKisonono

  • oMaambukizi ya Chlamydia

  • Trichomoniasis

  • Vaginosis ya bakteria

  • Pelvic inflammatory disease (PID)

  • Maambukizi ya virusi vya Human papillomavirus (HPV) au

  • Saratani ya shingo ya kizazi


Wapi unapata taarifa zaidi ya dawaza uchafu unaotoka ukeni?


Kufahamu matibabu ya kila ugonjwa tafuta dawaya ugonjwa huo kweye kiboksi cha tafuta chochote hapa.' juu ya tovuti hii kwa kuandika mfano, dawa ya kisonono, au dawa za fangasi ukeni kisha bofya kitufe cha kutafuta na chagua uchaguzi ambao unaendana na unachotafuta.


Majina mengine ya dawa za uchafu ukeni


Baadhi ya watu hutumia majina mengine kumaanisha kutokwa na uchafu ukeni kama vile,


  • Dawa ya kukausha uchafu ukeni,

  • Dawa ya kuzuia uchafu ukeni,

  • Dawa ya majimaji yanayotoka ukeni,

  • Dawa ya harufu mbaya ya uke

  • Dawa ya kukata uchafu ukeni, n.k


ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
10 Julai 2023 10:16:39
1. CDC. Vaginal Candidiasis. https://www.cdc.gov/fungal/diseases/candidiasis/genital/index.html. Imechukuliwa 06.06.2021

2. Peter G. Pappas, et al. Clinical Practice Guideline for the Management of Candidiasis: 2016 Update by the Infectious Diseases Society of America. https://academic.oup.com/cid/article/62/4/e1/2462830. Imechukuliwa 06.06.2021

3. Vulvovaginal Candidiasis. https://www.cdc.gov/std/tg2015/candidiasis.htm. Imechukuliwa 06.06.2021

4. Pelvic Inflammatory Disease (PID). https://www.cdc.gov/std/tg2015/pid.htm. Imechukuliwa 06.06.2021

5. @uly clinic Vaginal discharge syndrome treatment
bottom of page