top of page
Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, M.D
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD

Dawa za kichefuchefu na kutapika

11 Julai 2023 08:15:57
Image-empty-state.png

Dawa hizi hufanya kazi kwa kuzuia kichefuchefu na kutapika kusababishwa na matatizo mbalimbali ndani ya mwili yanayoweza kuwa ya hatari au yasiyo ya hatari.  Endapo mtu ana kichefuchefu na kutapika, kitiba huashiria kuna shida fulani inaendelea ndani ya mwili inayosababisha dalili hizi (mfano maambukizi ndani ya mfumo wa chakula-minyoo, amoeba, kipindupindu,homa ya matumbo-typhoid, maambukizi kwenye mfumo wa fahamu n.k)


Kupata ushauri wa daktari ni lazima kabla ya kutumia dawa yoyote ya kuzuia kichefuchefu na kutapika. Wakati mwingine kutapika ni bora kuliko kuzuia kutapika kwa sababu huondoa tatizo ndani ya mwili,mfano mtu amekunywa sumu au ana maambukizi ndani ya tumbo ambapo mwilikwa asili yake unataka kuyatoa nje ya tumbo kwa njia ya kutapika. Lakini pia kutapika kupita kiasi kunaweza kusababisha mtu kuishiwa nguvu na kulegea, figo kuferi ghafla, mapigo ya moyo kutokueleweka na hata kifo hii ni kwa sababu kupoteza madini muhimu na maji mwilini.


​Orodha ya dawa

Dawa zinazoweza kuzuia kutapika ni pamoja na;
  • Promethazine (phenergan)

  • Prochlorperazine(compazine)

  • Metoclopramide(reglan)

  • Diphenhydramine


Dawa zilizoorodheshwa hapa chini huzuia kupata kichefuchefu na kutapika;
  • Ondasetron

  • Promethazine

  • Prochlorperazine

  • Prochlorperazine

  • Cyproheptadine

  • Diphenhydramine

  • Amitriptyline

  • Propanol

  • Phenobarbital

  • Topiramate

  • Zonisamide

  • Erythromycin

  • Sumatriptan

  • Lorazepam

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
11 Julai 2023 08:15:57
BNF 2021
bottom of page