Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kutibu dutu ya sehemu za siri (Genital warts)
7 Juni 2021, 18:28:36

Chunjua au dutu inafahamika pia kwenye tovuti hii kama 'maoteo sehemu za siri' ni aina mojawapo ya ugonjwa wa zinaa . Nusu ya wanaojihusisha na ngono mara kwa mara haswa isiyo salama hupata maambukizi haya kwenye muda fulani katika maisha yao na wanawake wanaathiriwa sana na haya kuliko wanaume.
Matibabu ya dutu sehemu za siri (Genital warts) ni ya aina gani?
Matibabu ya dutu ni yale ya kutumia dawa au upasuaji.
Matibabu ya dutu kwa kutumia dawa
Imiquimod
Podofilox
Sinecatechins
Trichloroacetic acid (TCA)
Bichloroacetic acid (BCA)
Matibabu ya dutu kwa upasuaji
Matibabu ya dutu kwa njia ya upasuaji huhusisha
Upasuaji wa kukata dutu
Upasuaji wa kugandisha dutu (Cryotherapy)
Chanjo ya maambukizi ya Virusi vya HPV
Endapo bado hujaanza kushiriki ngono, ni vema ukapata chanjo. Chanjo zinazopatikana ni;
Chanjo ya Cervarix (HPV Bivalent)
Gardasil (HPV Quadrivalent)
Gardasil 9 (HPV Nonavalent)
Recombinant (HPV) Bivalent Vaccine
Recombinant (HPV) Nonavalent Vaccine
Recombinant (HPV) Quadrivalent Vaccine