Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kutibu Vaginosis ya bakteria
7 Juni 2021 15:46:39
Bacterial vaginosis au vaginosis ya bakteria ni moja yaugonjwa wa zinaa unaoambukizwa kwa kujamiana. Endapo umepimwa na kukutwa na ugonjwa huu ni vema ukatumia dawa wewe na mpenzi wako kila mtu dozi yake, isipofanyika hivyo, utapata maambukizi upya kutoka kwa mpenzi wako ambaye hajatibiwa. Endapo una wapenzi wengi, wote wanabidi kutibiwa ili kuepuka kupata maambukizi utakaposhiriki nao tena.
Dawa za kutibu Bacterial vaginosis
Dawa za kutibu Bacterial vaginosis au vaginosis ya bakteria zinajumuisha;
Dawa za kunywa
Dawa za kupaka au vidonge vya kuweka ukeni
Dawa za kunywa
Metronidazole
Tinidazole
Clindamycin
Dawa za kupaka
Clindamycin
Metronidazole
Majina mengine ya dawa ya kutibu bakteria vaginosis ni nyapi?
Baadhi ya watu hutumia majina yafuatayo kumaanisha dawa za matibabu ya maambukizi ya bakteria vaginosis;
Dawa za kutibu uchafu wa kahawia ukeni
Dawa za kutibu kutokwa na uchafu wenye harufu ya samaki ukeni
Dawa za kuondoa harufu mbaya ukeni
Dawa za kuzuia uchafu wa kahawia ukeni