top of page
Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD

Dawa za kutumia baada ya kupata kiharusi

16 Juni 2021 18:33:59
Image-empty-state.png

Kiharusi huchangiwa kwa asilimia zaidi ya 80 na kuzibwa kwa mishipa ya damu inayolisha sehemu fulani ya ubongo. Asilimia zilizobaki ni kutokana na kupasuka kwa mshipa wa damu unaolisha sehemu fuoani ya uvongo. Kuziba kwa mishipa ya damu ya ubongo htokana na mabonge ya damu yaliyofanyika katika mishipa mikubwa kutokana na sababu mbalimbali.


Tafiti za zinaendelea kufanyika ili kugundua dawa mbalimbali za kisasa ambazo zitatumika katika matibabu ya kiharusi haswa kwa wagonjwa ambao wameshelewa kupata matibabu. Makala hii imeelezea dawa zinazotumika ili kuharakisha uponyaji wa haraka na kuzuia uwezekano wa kupata kiharusi wakati ujao. Dawa kama tPA ikitolewa mapema zaidi kwa wagonjwa wa kiharusi, huharakisha uponyaji wa mishipa ya fahamu na sehemu ya ubongo iliyokufa kwa wagonjwa wenye kiharusi cha iskimia.



Makundi ya dawa


Makundi ya dawa zinazotumika baada ya kupata kiharusi ni;


  • Dawa za kuyeyusha damu

  • Dawa za kupunguza shinikizo la damu

  • Dawa za kuchochea ukarabati wa ubongo na mishipa ya fahamu

  • Vyakula na dawa asili zenye kampaundi za kuchochea uzalishaji chembe za ubongo na neva


Dawa hizi huzuia damu kuganda kirahisi na hutumika kwa wagonjwa waliopata kiharusi cha iskemia.


Dawa zinazozuia damu kuganda

  • Warfarin (Coumadin, Jantoven).

  • Dawa za kuzuia chembe sahani kukusanyika kama Clopidogrel (Plavix) na Aspirin

  • tPA

  • Dawa za kushusha lehemu kwenye damu kama jamii ya statin kama vile Atorvastatin (Lipitor), Fluvastatin (Lescol), Lovastatin (Altoprev), Pitavastatin (Livalo), Pravastatin (Pravachol), Rosuvastatin (Crestor) na Simvastatin (Zocor).


Dawa za kupunguza shinikizo la damu

Hutumika endapo mtu ana shinikizo la juu la damu, dawa hizo ni;


Dawa jamii ya ACE

  • Benazepril (Lotensin)

  • Captopril,

  • Enalapril (Vasotec),

  • Fosinopril,

  • Lisinopril (Prinivil, Zestril),

  • Moexipril

  • Erindopril

  • Quinapril (Accupril)


Beta-bloka

  • Acebutolol (Sectral),

  • Atenolol (Tenormin),

  • Bisoprolol (Zebeta),

  • Metoprolol (Lopressor, Toprol XL),

  • Nadolol (Corgard),

  • Nebivolol (Bystolic)

  • Propranolol (Inderal, InnoPran XL)


Calcium channel bloka

  • Norvasc (amlodipine)

  • Plendil (felodipine)

  • DynaCirc (isradipine)

  • Cardene (nicardipine)

  • Procardia XL,

  • Adalat (nifedipine)

  • Cardizem

  • Dilacor, Tiazac, Diltia XL (diltiazem)


Dawa za kuchochea ukarabati wa ubongo na mishipa ya fahamu


Dawa hizi hufanya kazi ya kuchochea uzalishaji wa neva na chembe mpya za ubongo ili kurejesha sehemu zilizokufa kutokana na kiharusi cha iskimia. Dawa hizi kwa sasa bado zipo kwenye majaribio ya tafiti, na inatia moyo kwamba zitakapokuwepo sokoni zitasaidia sana wagonjwa wa kiharusi kurejesha hisia za mwili;


  • Pifithrin-α (PFT-α)

  • Protini za Morphojenetiki 7 kutoka kweye mifupa

  • Neurotrophic factor (BDNF)

  • Damu ya kitovu cha mtoto

  • Kokeini na amphetamine


Kumbuka

Kokeini na amphetamine zinapatikana madukani lakini zipo katika makundi ya dawa ambazo haziruhusiwi kutumika pasipo kuandikiwa na daktari na ni miongoni mwa dawa za kulevya.


Vyakula na dawa asili


Vyakula na vitu halisi vya vyenye kampaundi za kuchochea uzalishaji chembe za ubongo na neva

Kuna vyakula kutoka kwenye mazingira yetu ambavyo vimeonekana katika tafiti kuwa na kampaundi zinazochochea uzalishaji wa chembe mpya za ubongo na neva ili kurekebisha sehemu zilizokufa kutokana na kiharusi. Vyakula hivi vinaonekana pia kuwa na faida zaidi vikitumika kabla ya kutokea wa kiharusi. Kampaundi muhimu kutoka kwenye vyakula hivo ni;


Polyphenol kutoka kwenye matunda madogo ya rangi ya bluu (kama blueberi) na majani ya chai ya kijani, unga wa kokoa, wine nyekundu, zabibu nyekundu, mbegu za siha, mboga za majani, mafuta ya mzeituni, kahawa


Amino asidi kama carnosine inayopatikana kwenye vyakula kana bata mzinga, kuku, nyama ya nguruwe na ngombe. Vyakula kama mayai, maziwa na siagi ya ng’ombe huwa na kiasi kidogo sana cha carnosine.


Dawa zilizotengenezwa kutoka kwenye matunda yenye polyphenol


Kuna dawa nyingi ambazo zimetengenezwa kutoka kwenye viini vya matunda yaliyotajwa hapo juu. Mfani wa dawa hizo ni kama Stem cell n.k.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
10 Julai 2023 10:16:39
1.Kuo-Jen Wu, et al. Improving Neurorepair in Stroke Brain Through Endogenous Neurogenesis-Enhancing Drugs. https://journals.sagepub.com/doi/10.1177/0963689717721230. Imechukuliwa 16.06.2021

2.Arnett DK, et al. (2019). 2019 ACC/AHA guideline on the primary prevention of cardiovascular disease. DOI: 10.1016/j.jacc.2019.03.010. Imechukuliwa 16.06.2021

3.Ischemic stroke treatments.strokeassociation.org/en/about-stroke/treatment/ischemic-stroke-treatment. Imechukuliwa 16.06.2021

4.Medications.
stroke.org/we-can-help/survivors/stroke-recovery/first-steps-to-recovery/preventing-another-stroke/medications. Imechukuliwa 16.06.2021

5.Stroke.nhlbi.nih.gov/health-topics/stroke. Imechukuliwa 16.06.2021

6.Stroke treatments. stroke.org/we-can-help/survivors/just-experienced-stroke/stroke-treatments. Imechukuliwa 16.06.2021

7. Healthy Foods High in Polyphenols. https://www.webmd.com/diet/foods-high-in-polyphenols#/. Imechukuliwa 16.06.2021

8. The top food sources of carnosine. https://www.carnosyn.com/carnosine-guide/#.Imechukuliwa 16.06.2021
bottom of page