top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

24 Aprili 2020 11:48:51

Miglitol

Miglitol

Utangulizi


Miglitol ni dawa inayotumika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu na kuhakikisha inabaki kwenye kiwango cha kawaida. Dawa hii iliyo kwenye kundi la dawa la alfa glukosidazi inhibita, hutumika pamoja na lishe sahihi na mazoezi ili kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na kisukari aina ya pili.


Miongoni mwa faida za dawa hii ni kuwa haichangii ongezeko uzito kwa mgonjwa wa kisukari na haina madhara kwenye ini.


Majina mengine


• Glyset

• Diastabol

• Plumarol


Fomula ya kikemikali


• C8H17NO5


Jina la kisayansi (IUPAC)


• (2R,3R,4R,5S)-1-(2-hydroxyethyl)-2-(hydroxymethyl)piperidine-3,4,5-triol


Muonekano


• Mara nyingi huwa ni kidonge kidogo cheupe cha mvringo, ingawa umbo na rangi vinaweza kubadilika kutegemeana na kiwanda kinacho itengeneza.


Dozi inayopatikana


Hupatikana kama vidonge vyenye;


• Miligramu 25

• Miligramu 50

• Miligramu 100


Namna ya kutumia


• Meza dawa hii kadri ulivyo elekezwa na daktari wako.

• Meza dawa hii punde kabla ya kula.

• Dawa hii huweza kutumiwa pamoja na dawa nyingine kama vile metformin, kama akipendekeza daktari wako.


Inavyofanya kazi mwilini.


Dawa ya miglitol hufanya kazi ya kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu kwa kuchelewesha mmeng'enyo wa vyakula vya wanga. Kuchelewa kwa mmeng'enyo wa vyakula vya wanga husababisha sukari kutofanyika upesi na kutoingia kwenye damu kwa kiwango kikubwa.


Kwa kuchelewesha mmeng'enyo wa vyakula vya wanga, pia huchelewesha ufyonzwaji wa sukari ya glukosi kutoka kwenye mfumo wa chakula kwenda kwenye damu hivyo kuzuia kuongezeka kwa kiwango cha sukari ya damu.


Mwili unchofanya kwa dawa hii


Dawa hii haichakatiwi mwilini bali hufanya kazi bila kubadilishwa na hufyonzwa na kutolewa kupitia njia ya mkojo.


Madhara madogo madogo


• Maumivu ya tumbo

• Tumbo kujaa hewa

• Kujamba

• Kuharisha

• Vipele kwenye ngozi


Marufuku kwa wagonjwa wafuatao


• Wenye mzio na dawa hii

• Wagonjwa wa kisukari aina ya kwanza

• Wagonjwa ambao figo zimeshindwa kufanya kazi.

• Wagonjwa waliowahi kupata dayabetiki ketoasidosisi

• Wagonjwa waliopata tatizo la kuziba kwa utumbo wa chakula

• Wagonjwa wenye magonjwa ya infamatori baweli


Kundi la dawa katika ujauzito


Dawa hii ipo kundi B la usalama wa dawa kipinid cha ujauzito


Matumizi wakati wa ujauzito na kunyonyesha


• Inaweza kutumiwa kwa mama mjamzito ila hakuna tafiti za kutosha juu mdahara yake.

• Epuka kwa kipindi cha kunyonyesha.

• Ni vyema kufuata muongozo wa wizara ya afya kwa nchi husika. Mfano kutumia insulini wakati wa ujauzito.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:28:26

Rejea za mada hii:-

1.FDA. Miglitol. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2012/020682s010lbl.pdf. Imechukuliwa 24/04/2020.

2.Goodman & Gilman’s The Pharmacological Basis of THERAPEUTICS twelfth edition ISBN: 978-0-07-176939-6 ukurasa wa 1264

3.Madescape: https://reference.medscape.com/drug/glyset-miglitol-342716#6. Imechukuliwa 24/04/2020.

4.Pub Chem: https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Glyset. Imechukuliwa 24/04/2020.
bottom of page