Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
23 Aprili 2020, 12:28:19

Nateglinide
Utangulizi
Nateglinide ni dawa inayotumika kushusha kiwango cha sukari katika damu kwa wagonjwa wenye kisukari aina ya pili. Dawa hii ipo kwenye kundi la dawa linaloitwa meglitinide, hufanya kazi kwa haraka na ndani ya muda mfupi.
Majina mengine
Nateglinide-phenyl-d5
Fomula ya kikemikali
C19H27NO3
Jina la kisayansi (IUPAC)
(2R)-3-(2,3,4,5,6-pentadeuteriophenyl)-2-[(4-propan-2-ylcyclohexanecarbonyl) amino]propanoic acid.
Muonekano
Ni dawa ya kidonge. Umbo na rangi vinaweza kutofautiana kutegemeana na kiwanda kinachozaliza.
Dozi zinazopatikana
Mara nyingi hupatikana katika vidonge vyenye;
• Miligramu 60
• Miligramu 120
Namna ya kutumia
• Meza kama utakavyo elekezwa na daktari wako.
• Unashauriwa kumeza dakika 30 kabla ya kula chakula.
• Usimeze kama hutokula chakula.
• Inaweza kutumiwa pamoja na metformin kama akiamua daktari wako.
Namna inavyofanya kazi mwilini
• Huchochea seli beta kongosho kuzalisha insulin ambayo ndio hususha kiwango cha sukari kwenye damu.
Mwili unachofanya kwa dawa hii
• Hufyonzwa upesi kutoka kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwenda kwenye damu.
• Huanza kufanya kazi dakika 15 baada ya kumezwa.
• Hufikia kilele cha ufanisi wa utendaji kazi baada ya saa 1 hadi 2.
• Huchakwata na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kupunguza sumu.
• Takamwili za dawa hii zinazobaki mwilini hutolewa nje ya mwili kwa njia ya mkojo (asilimia 83) na kinyesi (asilimia 10).
Maudhi madogo madogo
• Maumivu ya kichwa
• Maambukizi ya njia ya hewa
• Dalili za mafua
• Kuharisha
• Kichefuchefu
Madhara makubwa
Kushusha sukari kupita kiasi (asilimia 2 ya wagonwa)
Marufuku kutumiwa na wagonjwa wafuatao;
• Wenye mzio na dawa ya Nateglinide.
• Wenye kisukari kinachotibika na dawa ya insulin pekee (kisukarisukari aina ya kwanza).
• Wagonjwa wenye historia ya kupata dayabetiki ketoasicosisi
• Wagonjwa wenye matatizo ya ini
Tahadhari wakati wakutumia dawa hii
Tahadhari huchukuliwa kwa sababu dawa inaweza kushuka sukari mara dufu kwa wagonjwa wa kisukari wenye hali zifuatazo:-
• Isitumiwe na dawa nyingine inachochea uzalishaji wa insulin.
• Wagonjwa wenye matatizo ya figo.
• Maambukizi na homa kali
• Majeraha makubwa
• Wanaohitaji Upasuaji mkubwa
• Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha
• Wazee
• Wagonjwa wenye upungufu wa lishe (utapiamlo).
• Isitumiwe pekee yake kana kwamba ni badala ya metformin bali itumike pamoja na metformin ili kuhakikisha kwango cha sukari kinarekebishwa kwa usahihi.
Matumizi wakati wa ujauzito na kunyonyesha
Ni vyema kuiepuka wakati wa ujauzito na wakati wakunyonyesha kwani inaweza kuleta madhara kwa mtoto.
Kundi la dawa kwenye ujauzito
Dawa hii ipo kwenye kundi C la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:27:06
Rejea za mada hii:-