Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
23 Aprili 2020 20:12:54
Repaglinide
Repaglinide ni dawa ya inayotumika katika matibabu ya kisukari aina ya pili, iliyo kundi la meglitinide.
Sifa ya kipekee ya Repaglinide
Sifa ya repaglinide kufyozwa kwa upesi na kuanza kufanya kazi muda mfupi mara baada ya kumezwa.
Majina ya kibiashara
Majina ya kibiashara ya Repaglinide ni;
Prandin
GlucoNorm
NovoNorm
Fomula ya kisayansi
Fomula ya kikemikali ya Repaglinide ni C27H36N2O4
Jina la kisayansi
Repaglinide huwa na jina la kisayansi la 2-ethoxy-4-[2-[[(1S)-3-methyl-1-(2-piperidin-1-ylphenyl)butyl]amino]-2-oxoethyl]benzoic acid
Fomu na uzito wa Repaglinide
Dozi inaweza kupatikana katika kidonge chenye;
Miligramu 0.5
Miligramu 1
Miligramu 2
Namna ya kutumia Repaglinide
Meza kadri ulizoelekezwa na daktari wako.
Meza dakika 15 kabla ya kula.
Usimeze kama huto kula.
Ufanyaji kazi wa Repaglinide
Huchochea seli bita za kongosho kuzalisha insulini ambayo ndiyo hushusha sukari ya damu.
Nusu maisha ya Repaglinide
Huanza kufanya kazi dakika 15 hadi 60 baada ya kumeza. Hufanya kazi mwilini kwa saa 4 hadi 6.
Utoaji taka za Repaglinide mwilini
Huchakatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondoa sumu.
Takanwili za mabaki yake hutolewa kwenye kinyesi (90%) na mkojo (8%).
Muingiliano wa Repaglinidena dawa zingine
Dawa hizi huongeza ufanisi wa Repaglinide: -
Celecoxib
Diclofenac
Etodolac
Fenoprofen
Flurbiprofen
Ibuprofen
Indomethacin
Ketoprofen
Ketorolac
Meclofenamate sodium
Meloxicam
Nabumetonea
Naproxen
Oxaprozin
Piroxicam
Rofecoxib
Sulindaca
Tolmetin
Phenelzine (Nardil)
Tranylcypromine (Parnate)
Isocarboxazid (Marplan)
Aspirin
Buffered aspirin
Choline n salicylate
Diflunisal
Magnesium salicylate
Salsalate
Sodium salicylate
Sodium thiosalicylate
Dawa hizi hupunguza ufanisi wa Repaglinide: -
Bendroflumethiazide
Benzthiazide
Chlorothiazide
Hydrochlorothiazide
Hydroflumethiazide
Methyclothiazide
Polythiazide
Trichlormethiazide
Chlorthalidone
Indapamide
Metolazone
Betamethasone
Budesonide
Dexamethasone
Dexone,
Hydrocortisone
Sodium phosphate
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Repaglinide
Marufuku kutumiwa kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye mzio na Repaglinide.
Wagonjwa wenye kisukari aina ya kwanza
Wagonjwa wenye dayabetiki ketoasidosisi
Angalizo
Tahadhari ya matumizi ya Repaglinide huchukuliwa kwa sababu ya uwezekano wa kushusha kiwango cha sukari kwenye damu kupita kiasi ni mkubwa kwa wagonjwa wa kisukari wenye hali zifuatazo:-
Wagonjwa wenye matatizo kwenye ini
Wagonjwa wenye matatizo ya figo
Maambukizi na homa kali
Majeraha makubwa
Upasuaji mkubwa
Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha
Wazee
Wagonjwa wenye upungufu wa lishe (utapiamlo)
Maudhi madogo ya Repaglinide
Maumivu ya kichwa (9%-11%)
Maumivu ya mgongo (5%-6%)
Maumivu ya viungo (3%-6%)
Kuharisha (4%-5%)
Matatizo kwenye njia ya hewa(bronchitis) (2%-6%).
Maumivu ya kifua (2%-3%)
Kutopata choo (2%-3%)
Madhara makubwa ya Repaglinide
Kushusha sukari kupita kiasi (10%-16%)
Madhara megnine ya Repaglinide
Madhara mengine ambayo hutokea kwa kiwango cha chini ya 1% ni:-
Upungufu wa damu
Matatizo ya kuona
Matatizo ya kongosho
Repaglinidewakati wa kunyonyesha
Nivyema kuepuka dawa hii wakati wa ujauzito na kunyonyesha. Hakuna tafiti za kutosha juu ya madhara yake wakati wa ujauzito na kunyonyesha.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:24:39
Rejea za mada hii:-