top of page

Maana

​

Aina na visababishi

​

Degedege na Kifafa

​

Imeandikwa na daktari wa ULY clinic

​

Degedege ni mijongeo ya ghafla, mikali, isiyo ya hiari  na mpangilio maalumu inayotokea kwenye mwili inayosababishwa na kujongea kwa misuli  kama matokea ya kuharibika kwa mfumo wa fahamu wa ubongo kwa kutoa taarifa pasipo mpangilio.

 

Kwa kawaida Ubongo hutoa taarifa za kuamrisha viungo vingine kufanya kazi, taarifa hizi husafiri kama umeme kupitia mishipa ya fahamu na kufika sehemu ambayo imeamuriwa kufanya kazi. Umeme unapofika sehemu husika ya mwili, mwili huitikia kwa kufanya ile kazi iliyoamriwa. mfano wa baadhi ya kazi ni kama vile  kutembe kushika kitu, moyo kufanya kazi, kutoa haja kubwa n.k.

 

Mfuo huu wa  ubongo ukitoa umeme pasipo mpangilio, mtu hupata dalili za mijongeo isiyo ya hiari na kuonekana kama degedege

​

Kifafa ni hali inayotokea endapo mtu atapata degedege mara mbili ama zaidi ndani ya masaa 24 bila kuwa na kisababishi chochote.

​

imeboreshwa 29/03/2020

bottom of page