Imeandikwa na Daktari wa ULY-clinic
Demataitiz
​
Demataitiz ni neno la kitiba ambalo limetoholewa na ULY CLINIC kutoka kwenye neno tiba Dermatitis ambalo pia lilitokana na neno la Kigiriki “dermat” ikimaanisha “Ngozi” na “-its” ni neno la kiingereza.
​
Hivyo demataitiz ni neno tiba linalomaanisha michomo kenye Ngozi, ambapo mtu mwenye dalili hii huwa na Ngozi kavu, iliyovimba, enye kuwa nyekundu na wakati mwingine enye vipele. Hata hivyo dalili zake hutegemea na aina ya demataitiz. Tatizo hili huweza kusababisha miwasho kenye Ngozi inayoweza kuwa ya wastani au mikali.
​
Baadhi ya aina za za demataitiz huweza kudumu kwa muda kidogo na wakati mwingine kukaa muda wa siku kadhaa kisha kutoweka na baadhi hutokea kwa watoto na zingine hutokea kwa watu wakubwa. Hata hivyo demataitiz huweza kutulizwa kwa dawa za kupaka au kumeza.
Dalili za demataitis
-
Vipele kwenye Ngozi
-
Malenge kwenye Ngozi
-
Ngozi iliyokauka na kupasuka
-
Miwasho ya Ngozi
-
Maumivu ya kuchoma na kama ya kung’atwa na mdudu
-
Ngozi kuwa nyekundu
-
Kuvimba
​
Aina za demataitis
Pumu ya Ngozi- kwa jina jingine huitwa ezima, hurithiwa na huanza utotoni. Soma Zaidi hapa.
​
Demataitis ya kugusana- demataitis aina hii hutokana na kuguswa kwa Ngozi na kitu kigeni, hivyo Ngozi huitikia kwa kutoa kemikali zinazosababisha demataitiz
​
Demataitis ya dishindrotiki- hutokana na ngozi kupoteza uwezo wa kujilinda yenyewe. Husababisha Ngozi kuwa kavu, kuwasha na huambatana mara nyingi na malenge lenge kwenye Ngozi.
​
Demataitis ya seboreiki.- Hutokea kwa Watoto na haswa maeneo ya kichwani ingawa inaweza kutokea kwenye maeneo ya uso au kifuani. Husababisha makovu, Ngozi kuwa nyekundu na m’mba.
​
Demataitiz ya Folikula. Aina hii hudhuru mashina ya vinyweleo vya ngozi na kufanya ngozi iwe nene na kuwa na uvimbe kwenye shimo la ngozi. Tatizo hili hutokea sana kwa watu asili ya Afrika na watuwenye rangi ya ngozi ya maji ya kunde.
​
Visababishi vya demataitis ni kama vile;
Visababishi hutegemea aina ya demataitis. Visababishi vya demataitiz aina ya dishindroiki haifahamiki
​
Demataitis ya kugusana
Huweza kuamshwa na vichokoza Ngozi endapo vitagusana na Ngozi ambavyo ni
-
Madawa jamii ya detegenti
-
Mafuta ya urembo
-
Madini ya niko
-
Sumu ya ivy na oak
Pumu ya Ngozi- huamshwa na mambo kama Ngozi kavu, mazingira na maambukizi ya bakteria kwenye Ngozi. Pumu ya Ngozi ni tatizo la kijeni na hutembea kwenye familia, huambatana na mzio na pumu ya kifua(asma).
​
Demataitis ya seboreiki
Husababishwa na maambukizi ya fangazi kwenye tezi za Mafuta ya ngozi. Huamka Zaidi kipindi cha baridi na mvua.
​
Vitu vinavyoweza kuamsha tatizo la demataitizi ni;
-
Msongo wa mawazo
-
Mabadiliko ya homoni
-
Mazingira
-
Kemikali chokozi wkenye Ngozi
Matibabu ukiwa nyumbani
​
Matibabu ya demataitiz hutegemea kisababishi, baadhi ya dalili huweza kupotea siku kadhaa hadi wiki kadhaa bila tiba.
Endapo dalili hazijapotea unaweza kufanya mambo haya ukiwa nyumbani
-
Kutumia dawa za kupunguza mzio na miwasho kwenye Ngozi- dawa jamii ya anthistamine kama diphenyhydramine
-
Kuanika eneo lenye tatizo kwenye mwanga wa jua - weka eneo ambalo limepata madhara kwenye mwanga wa jua kwa dakika chache. Yaache maeneo yenye tatizo kupigwa na mwanga wa jua ukiwa unatembea. Kumbuka
-
Tumia krimu ya Ngozi yenye mchanganyiko wa steroid kama hydrocortisone kuondoa miwasho ya Ngozi na miunguzo
-
Tumia krimu kulainisha Ngozi endapo Ngozi yako ni kavu
-
Kuoga maji yenye shayiri.
Kujikinga
-
Onga kwa muda mfupi – tumia dakika 5 hadi 10 tu na tumia maji ya uvuguvugu badala ya baridi. Unaweza kutumia Mafuta ya kuogea pia
-
Tumia nguvu kidogo na sabuni ambayo haikaushi Ngozi
-
Jikushe kwa kutumia nguvu kiasi
-
Fanya Ngozi yako iwe na unyevu nyevu kwa kutumis Mafuta
Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba
​
​
Imeboreshwa 12.03.2020
​