top of page

Mwandishi:

Dkt. Peter A, MD

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

30 Oktoba 2021 14:51:40

Image-empty-state.png

Mjamzito kuvimba miguu

Kuvimba chini au juu ya usawa wa kifundo cha mguu wakati wa ujauzito ni hali ya kawaida kama itatokea na kuongezeka taratibu. Karibia wanawake wote wajawaziti hupata dalili hii na huzidi kipindi cha tatu cha ujauzito. Kama uvimbe wa miguu unatokea kwa haraka au kuwa namaumivu, wasiliana na daktari kwa uchunguzi.


Wakati gani uwasiliane na daktari haraka?


Ukiwa na dalili ya kuvimba miguu wakati wa ujauzito pamoja na zifuatazo unapaswa kuwasiliana nadaktari haraka;


 • Ongezeko la kasi la uvimbe usoni, mikono au kwenye kanyagio

 • Maumivu makali ya kichwa

 • Matatizo ya kuona ( mfano kutoona vema au vitu kuwa vimefifia)

 • Maumivu makali chini ya mbavu

 • Kutapika pamoja na dalili za hapo juu


Kwanini miguu huvimba wakati wa ujauzito?


Kuna njia mbalimbali zinazofahamika kuchangia miguu kuvimba wakati wa ujauzito ambazo ni;


 • Wakati wa ujauzito wa kawaida, mwili wa mama mjamzito hupata ongezeko la lita 6 hadi 8.

 • Mwili huongeza utunzaji wa chumvi (sodium) kwa takribani milimol 950 wakati huu wa ujauzito. Chumvi hii hutunza maji mwilini na kuweza pelekea uvimbe.

 • Kupungua kwa uwezo wa mwili kudhibiti kiwango cha maji cha nje na ndani ya chembe hai hupungua pia wakati wa ujauzito.

 • Mabadiliko ya kiwango cha maji kwenye tishu zinazozunguka chembe hai wakati wa ujauzito husababisha kuhama kwa maji na kwenda nje ya chembe hai na hivyo kupelekea mwonekano wa uvimbe.


Hapo awali dalili ya kuvimba miguu ilitumiwa kuwa kigezo cha kuwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu la kifafa cha mimba, dalili hii kwa sasa haipaswi kutumika kutambua na haina msaada wowote kwani


Matibabu


Kuvimba miguu kutokana na mabadiliko ya kawaida wakati wa ujauzito huwa hakuhitaji matiabu yoyote ya dawa. Matumizi ya dawa za kupunguza maji mwilini yamehifadhiwa kutumika kwa wajawazito walio na dalili za kuvia kwa maji kwenye tishu za mapafu au wenye dalili za hatari za kupata shinikizo la juu la damu la kifafa cha mimba.


Matibabu ya kawaida ya kunyanyua miguu usawa wa moyo na kufanya mazoezi au kuvaa soksi hushauriwa zaidi kwa miguu iliyovimba kwenye usawa wa kifundo cha mguu.


Tiba isiyo dawa

 • Acha kukaa au kusimama kwa muda mrefu

 • Vaa viatu vinavyokuacha huru kwenye miguu na acha kuvaa viatu vinavyobana miguu yako

 • Ukiwa umekaa, weka miguu yako kwenye usawa wa moyo, mfano iweke kwenye kiti ukiwa umekaa

 • Kunywa maji ya kutosha ili kusaidia mwili wako kutoa maji ya ziada

 • Fanya mazoezi ya miguu ili kuongeza kasi ya kutoa maji miguuni


Mazoezi ya kufanya

 • Mazoezi yafuatayo husaidia kupunguza uvimbe miguuni wakati wa ujauzito

 • Kunja na nyoosha kanyagio ili kuitumikisha misuli ya miguu na kuongeza mzunguko wa damu. Fanya miendo 30 ya kukunja na kunyoosha miguu na mara mbili au zaidi kwa siku.

 • Fanya zoezi linalotengeneza mzunguko wa duara kwa kifundo, fanya miduara nane na mara nane kwa siku


Wapi utapata taarifa zaidi?


Pata taarifa zaidi kuhusu kuvimba na namna ya kukbiliana na tatizo la kuvimba miguu kwenye linki zifuatazo;


ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

21 Mei 2023 12:34:27

Rejea za dawa

 1. Davison JM. Edema in pregnancy. Kidney Int Suppl. 1997 Jun;59:S90-6. PMID: 9185112.

 2. Mohaupt MG. Odeme in der Schwangerschaft--banal? [Edema in pregnancy--trivial?]. Ther Umsch. 2004 Nov;61(11):687-90. German. doi: 10.1024/0040-5930.61.11.687. PMID: 15605462.

 3. Swollen ankles, feet and fingers in pregnancy. https://www.nhs.uk/pregnancy/related-conditions/common-symptoms/swollen-ankles-feet-and-fingers/. Imechukuliwa 29.10.2021

 4. Bamigboye AA, et al. Interventions for varicose veins and leg oedema in pregnancy. Cochrane Database of Systematic Reviews. http://onlinelibrary.wiley.com/wol1/doi/10.1002/14651858.CD001066.pub3/abstract. Imechukuliwa 30.10.2021

 5. Benninger B, et al. Anatomical factors causing oedema of the lower limb during pregnancy. Folia Morphologica. 2013;72:67.

 6. Merck Manual Professional Version. Lower-extremity edema during late pregnancy. http://www.merckmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/symptoms-during-pregnancy/lower-extremity-edema-during-late-pregnancy. Imechukuliwa 30.10.2021

 7. American College of Obstetricians and Gynecologists. Frequently asked questions. Pregnancy FAQ0119. Exercise during pregnancy. http://www.acog.org/~/media/For%20Patients/faq119.pdf?dmc=1&ts=20140619T1702280658. Imechukuliwa 30.10.2021

 8. Merck Manual Consumer Version. Swelling during late pregnancy. http://www.merckmanuals.com/home/women-s-health-issues/symptoms-during-pregnancy/swelling-during-late-pregnancy. Imechukuliwa 30.10.2021

 9. Health and Medicine Division of the National Academies Press Water. Dietary Reference Intakes for water, potassium, sodium, chloride and sulfate.. https://www.nap.edu/download/10925. Imechukuliwa 30.10.2021

bottom of page