top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

30 Oktoba 2021, 11:53:48

Kuvimba miguu kwa mjamzito husababishwa na nini?

Kuvimba miguu kwa mjamzito husababishwa na nini?

Mabadiliko ya vichochezi na ongezeko la shinikizo kwenye mishipa inayorejesha damu moyoni husababisha mkusanyiko wa maji chini ya kifundo cha mguu unaoonekana kama uvimbe.


Kuna visababishi vingine?


Ndio!


Mgandamizo wa mishipa ya damu na mabadiliko ya homon si sababu pekee ya kuvimba kwa miguu wakati wa ujauzito. Kuna visababishi vingine vinavyoweza kusababisha uvimbe wa miguu chini ya kifundo cha mguu unaoweza kuvuka kifundo kwenda juu. Visababishi hivyo ni vimeorodheshwa katika Makala ya miguu kuvimba na makala ya mjamzito kuvimba miguu.


Namna ya kupunguza uvimbe wakati wa ujauzito


  • Epuka kukaa kwa muda mrefu, ukiweza kaa huku umeweka miguu yako juu ya kiti kingine kilicho karibu ili kusaidia damu kurudi kwenye moyo.

  • Wakati umekaa na miguu yako ipo juu ya kiti, hakikisha unaifanyia mazoezi kwa kuizunguka kwenye maungio ya kiwiko cha mguu pia kuipeleka juu na chini. Hii itasaidia pia kurudisha damu moyoni

  • Unapokuwa umelala kitandani au chini, weka mto kwenye miguu ili kuifanya iwe juu na kusaidia kurejesha maji moyoni.

  • Vaa soksi za kusinyaza miguu iliyovimba wakati wa mchana, epuka kuvaa soksi zinazobana maeneo ya kifundo cha mguu au misuli nyuma ya mguu

  • Fanya mazoezi au jishughulishe kwa kutembea tembea kila siku

  • Vaa nguo zisizobana ili kuepuka kupunguza mzunguko wa admu maeneo ya miguuni au kiunoni

  • Unaweza fanya masaji ya miguu, masikio na mikono kunaweza punguza tatizo hili pia, hii imeonekana kwenye tafiti mbalimbali za reflexoloji.


Mambo ya kuzingatia


  • Usiache kunywa maji kama huna tatizo la moyo au hujashauriwa na daktari wako.

  • Kama unapata uvimbe wa ghafla kwenye kanyagio unaoambatana na maumivu na kwenye mguu mmoja haswa, inaweza kuwa ishara ya kuganda damu ndani ya mishipa na hivyo unapaswa kuwasiliana na daktari haraka kwa vipimo na matibabu.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

30 Oktoba 2021, 18:18:06

Rejea za mada hii

  1. Bamigboye AA, et al. Interventions for varicose veins and leg oedema in pregnancy. Cochrane Database of Systematic Reviews. http://onlinelibrary.wiley.com/wol1/doi/10.1002/14651858.CD001066.pub3/abstract. Imechukuliwa 30.10.2021

  2. Benninger B, et al. Anatomical factors causing oedema of the lower limb during pregnancy. Folia Morphologica. 2013;72:67.

  3. Merck Manual Professional Version. Lower-extremity edema during late pregnancy. http://www.merckmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/symptoms-during-pregnancy/lower-extremity-edema-during-late-pregnancy. Imechukuliwa 30.10.2021

  4. American College of Obstetricians and Gynecologists. Frequently asked questions. Pregnancy FAQ0119. Exercise during pregnancy. http://www.acog.org/~/media/For%20Patients/faq119.pdf?dmc=1&ts=20140619T1702280658. Imechukuliwa 30.10.2021

  5. Merck Manual Consumer Version. Swelling during late pregnancy. http://www.merckmanuals.com/home/women-s-health-issues/symptoms-during-pregnancy/swelling-during-late-pregnancy. Imechukuliwa 30.10.2021

  6. Health and Medicine Division of the National Academies Press Water. Dietary Reference Intakes for water, potassium, sodium, chloride and sulfate.. https://www.nap.edu/download/10925. Imechukuliwa 30.10.2021

bottom of page