• Daktari ni dawa gani nzuri zaidi ya UTI?
• Dawa gani ni nzuri katika kutibu UTI
• Nimeambiwa dawa nzuri ya UTI ni AZUMA je ni kweli?
• Ninasumbuliwa na UTI je nitumie dawa gani nzuri?
Utangulizi wa muhimu
Haya ni baadhi ya maswali yamekuwa yakiulizwa sana na wagonjwa haswa wale wanaotumia huduma za matibabu mtandaoni. Wengi pia wamekuwa wakitafuta kuhusu dawa nzuri ya U.T.I kwenye tovuti hii. Makala hii inajibu maswali hayo kwa ufasaha. Kila asomaye na asaidie kumtaarifu mwingine ili kupata elimu na kuepusha usugu wa dawa kwenye vimelea. Inakadiliwa kuwa vimelea wanaosababisha U.T.I wametengeneza usugu wa asilimia 100 kwenye dawa zinazotumika sana kwenye matibabu ya UTI ikiwa pamoja na dawa jamii ya penicilin na cephalosporin kizazi cha tatu.
Dawa nzuri ya UTI ni ipi?
Kiukweli kwa sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi yasiyo sahihi ya dawa, baadhi ya wagonjwa wenye maambukizi kama U.T.I na wataalamu wa afya hutumia mazoea tu kutumia au kutoa dawa bila kujua kwamba vimelea hao hubadilika kiasi cha kupoteza mwitikio kwenye dawa na kutoangamizwa kabisa na dawa.
Hata hivo pia, dawa inayoweza kuwa nzuri kwa mtu mmoja inaweza isiwe nzuri kwa mwingine ikitegemea hali ya usugu wa vimelea iliyojengwa kwenye dawa inayotumika.
Kutibiwa mara kwa mara UTI
Endapo umekuwa ukiambiwa kuwa na UTI baada ya kufanyiwa kipimo cha mkojo kila unapokwenda hospitali na kutibiwa na dawa mbalimbali pasipo mafanikio, hii ni ishara kuwa dawa hizo hazina uwezo wa kufanya kazi kwako. Kama umekuwa ukitumia dawa vema bila kukosa dozi, na dawa bado haijamaliza muda wake wa kazi hii inaweza maanidha kuwa dawa hiyo haina tena uwezo w akuua vimelea waliosababisha U.T.I kwako.
Nini cha kufanya kama vimelea nilionao wapo sugu kwenye dawa?
Kama umetibiwa UTI mara kwa mara pasipo dalili kuondoka, unapaswa kufanya kipimo cha kufahamu ni dawa gani yenye uwezo wa kuua aina ya vimelea ambavyo vinasababisha UTI kwako.
Kipimo gani cha kuonyesha dawa yenye uwezo wa kuua vimelea wa UTI wanaonisumbua?
Kipimo pekee cha kufahamu dawa yenye uwezo wa kuua vimelea wa UTI wanaokusumbua ni kipimo cha kupima uwezo wa dawa kwenye vimelea waliooteshwa kutoka kwenye mkojo kwa jina la kizungu ni urine culture and sensitivity Kama unasumbuliwa na UTI zingatia kufanya kipimo hicho na acha kudanganyika.
Je dawa yenye uwezo wa kuitbu U.T.I kwangu inaweza kutibu mtu mwingine?
Jibu linawez akuwa ndio asu sio, hii inategemea aina ya vimelea ambao wamekuathiri, na mwitikio wa vimelea kwenye dawa. Kama vimelea waliokuathiri wanafanana na wale waliomwathiri na wana mwitikio sawa kwneye dawa, dawa hiyo inaweza kukutibu.
Mambo gani mengine ya kufahamu kuhusu dawa nzuri ya kutibu UTI
Ni vema kufahamu kuwa, U.T.I ni maambukizi katika via vya mfumo wa mkojo, inaweza kuwa figo, mirija ya ureta, mrija wa urethra, au kiboofu cha mkojo. Pia U.T.I inaweza kusabaishwa na bakteria, virusi, fangasi au kemikali. Bakteria ni kisababishi kikuu cha UTI kwa watu walio na kinga nzuri ya mwili. Wapo bakteria wa aina mbalimbali lakini wakuu ni Staphylococcus aureus, Escherichia coli na Klebsiella pneumoniae
Wakati wa matibabu, mtaalamu wa afya na mgonjwa ni muhimu kuzingatia ni nini kinachosababisha U.T.I ili kupata matibabu ya uhakika pasipo kuleta madhara au kutengeneza usugu wa vimelea kwenye dawa kwa matumizi ya dawa yasiyo sahihi.
Rejea za mada hii;
1. Sangeda RZ, et al. National Antibiotics Utilization Trends for Human Use in Tanzania from 2010 to 2016 Inferred from Tanzania Medicines and Medical Devices Authority Importation Data. Antibiotics (Basel). 2021 Oct 15;10(10):1249. doi: 10.3390/antibiotics10101249. PMID: 34680829; PMCID: PMC8532727.
2. Five-day nitrofurantoin is better than single-dose fosfomycin at resolving UTI symptoms. Drug Ther Bull. 2018 Nov;56(11):131.
3. Long B, et al. The Emergency Department Diagnosis and Management of Urinary Tract Infection. Emerg Med Clin North Am. 2018 Nov;36(4):685-710.
4. Tang M, e tal. Recurrent Urinary Tract Infections are Associated With Frailty in Older Adults. Urology. 2019 Jan;123:24-27.
5. Behzadi P, Behzadi E, Yazdanbod H, Aghapour R, Akbari Cheshmeh M, Salehian Omran D. A survey on urinary tract infections associated with the three most common uropathogenic bacteria. Maedica (Bucur). 2010 Apr;5(2):111-5.
6. Yamaji R, et al. A Population-Based Surveillance Study of Shared Genotypes of Escherichia coli Isolates from Retail Meat and Suspected Cases of Urinary Tract Infections. mSphere. 2018 Aug 15;3(4)
7. Li R, et al. StatPearls [Internet]. StatPearls Publishing; Treasure Island (FL): Jan 6, 2023. Cystitis.
8. Foxman B. Epidemiology of urinary tract infections:Incidence, morbidity, and economic costs. Dis Mon. 2003;49:53–70.
9. American College of Obstetricians and Gynecologists. ACOG practice bulletin no 91:Treatment of urinary tract infections in nonpregnant women. Obstet Gynecol. 2008;111:785–94.
10. Foxman B, et al. Risk factors for second urinary tract infection among college women. Am J Epidemiol. 2000;151:1194–205.
11. Nguyen HT. Smith's General Urology. 16th ed. New York (USA): Mcgraw-Hill Medical; 2004. Bacterial Infections of the Genitourinary Tract; p. 220.
12. Momoh A, et al. The antibiogram types of Escherichia coli isolated from suspected urinary tract infection samples. J Microbiol Biotech Res. 2011;1:57–65.
13. Schnarr J, Smaill F. Asymptomatic bacteriuria and symptomatic urinary tract infections in pregnancy. Eur J Clin Invest. 2008;38(Suppl 2):50–7.
14. Spellberg B, Bartlett JG, Gilbert DN. The future of antibiotics and resistance. N Engl J Med. 2013;368:299–302.
15. McQuiston Haslund J, et al. Different recommendations for empiric first-choice antibiotic treatment of uncomplicated urinary tract infections in europe. Scand J Prim Health Care. 2013;31:235–40.
16. Goossens H, et al, Elseviers M ESAC Project Group. Outpatient antibiotic use in Europe and association with resistance:A cross-national database study. Lancet. 2005;365:579–87.
17. Warren JW, et al. Guidelines for antimicrobial treatment of uncomplicated acute bacterial cystitis and acute pyelonephritis in women. Infectious diseases society of America (IDSA) Clin Infect Dis. 1999;29:745–58.