top of page

Majadiliano na Wataalamu

Public·804 members

Ni nini husababisha maumivu ya jicho?

Hili ni swali niloulizwa leo na mgonjwa wangu kuhusu visababishi vya maumivu ya jicho, na nilimjibu kama ifuatavyo;Maumivu ya jicho ni ile hali inayotokea endapo kuna tatizo katika kuta za nje au ndani ya jicho. Kuwa na maumivu makalai ya jicho kunaweza kumaanisha kuna shuda kubwa kwenye jicho inayoweza kupelekea kupoteza kuona au kuwa una shida kubwa inayohitaji tiba ya haraka. Maumivu ya jicho huweza kuelezewa kama hali ya jicho kuwasha, kuungua, au ya kuchoma choma.Mara nyingi maumivu ya jicho hutokana an kuingia kwa kitu kigeni kwenye macho ambacho husabaisha kuamka kwa chembe hai za mwili ili kupambana na kumwondoa mgeni huyo, matokeo yake huwa ni uzalishaji wa kemikali zinazosababisha kuhisi maumivu na kubadilika kwa hali ya jicho ikiwa pamoja na rangi, kwa pamoja inaitwa michomo kwenye macho. Maumivu yanayotoka ndani ya jicho huwa na sifa za kuchoma au kuuma Sababu zinazoweza kusababisha maumivu ya jicho huwa pamoja;

  • Aleji/Mzio na kitu fulani

  • Michomo ya kwenye kope

  • Kuziba kwa mrija wa machozi

  • kuota kwa kifuko cha maji kwenye macho

  • Maumivu ya kichwa

  • Matumizi ya lensi za kuvaa

  • Mikwaruzo kwenye kuta ya konea

  • Macho kuwa makavu

  • Kitu kigeni kwenye macho

  • Tatizo la glaukoma

  • Majera, au kujigonga kwenye macho au kuungua

  • Michomo kwenye sehemu ya jicho yenye rangi nyeupe

  • Michomo kwenye konea

  • Michomo kwenye sehemu nyekundu ya konea

  • Michomo ya mshipa wa fahamu wa optic

  • Michomo kwenye kuta ya konjuctiva

  • Michomo kwenye ukuta w akatikati wa macho

  • Uvimbe mwekundu unauuma iliyo karibu na kingo za kope ya jicho

  • Kugeuza kope kwa ndani au nje kwa nje


Unamaumivu ya jicho? Kutana na daktari wako kwa tiba au tumia application ya uly clinic kupata tiba na daktari wako

32 Views

Kuhusu kundi

Uliza swali pamoja na kusoma majibu ya maswali yaliyoulizwa,...

bottom of page