Matibabu
​
Imeandikwa na madaktariwa ULY-Clinic
​
Matibabu kuzuia maambukizi baada ya kujihatarisha
Kama unajua umejihatarisha na maamukizi ya kirusi cha hepatitis B, mpigie daktari wako haraka. Kama hujawahi kupata chanjo au huna uhakika kama ushawahi kupata chanjo au kama mwili wako haukuitikia kwenye chanjo basi mwone daktari ambaye atakupa chanjo ya sindano dhidi ya kirusi huyu. Ndani ya masaa 12 ya kukutana na kirusi huyu itakayokusaidia kutopata ugonjwa huu. Na kisha utapacha chanjo hapo hapo pia.
​
Matibabu ya maambukizi ya mda mfupi
Kama daktari akitambua kama una maambukizi ya mda mfupi unaweza usihitaji matibabu kwa sababu ugonjwa utaisha wenyewe. Unatakiwa kupumzika, kula vizuri mlo kamili, kunywa maji ya kutosha wakati mwili wako unapambana na virusi.
Maambukizi sugu
Kama ukikutwa unamaambukizi sugu ya kirusi cha hepatitis B, unahitaji matibabu ili kupunguza hatarishi ya ugonjwa wa ini na kuzuia kuwaambukiza watu wengine. Matibabu huwa pamoja na;
Dawa za kupambana na virusi- lamivudine, adefovir, telbivudine na entecavir husaidia kupambana na kirusi huyu na kuzuia uwezo wao wa kuharibu ini.
Interferone alfa 2b- hutumika kwa watu wadogo(watoto) ambao hawataki matibabu ya mda mrefu au wanatarajia kupata ujauzito ndani ya mda mfupi. Huchomwa na huwa na madhara yasiyotakiwa kama huzuniko kuu, kushindwa kpumua na kubana kwa kifua.
Kubadilishiwa ini- kama ini lako likiwa limeathiriwa kwa kiwango kikubwa basi utabidi kuwekewa ini jingine kutoka kwa mtu mweingie endapo itawezekana. Wakati wa upasuaji daktari huondoa ini lililoathirika na kukuwekea jinngine. Ini la kuwekewa hutoka kwa watu waliokufa mara nyingi au kutoka kwa mtu mzima ambaye anatoa sehemu tu ya ini lake
​
Madawa mengine ya kupambana na maambukizi ya kirusi cha hepatitis B bado yanagunduliwa na kutengenezwa.
​
Imechapishwa 3/3/2015