Mwandishi;
Mhariri:
Jaza jina na cheo cha mwandishi
Jumanne, 2 Machi 2021
Presha ya kupanda -Huduma ya kwanza
Kurasa hii imezungumzia kuhusu huduma ya kwanza kwa mgonjwa mwenye shinikizo la juu la damu au presha ya kupanda. Mtu mwenye presha ni yule ambaye ana shinikizo la damu la sistoliki linazoanzia 140 milimita za mercury na kuendelea na lile la diastoliki la 90 milimita za mercury na kuendelea. Mahitaji ya huduma ya dharura hutegemea aina ya mgonjwa na endapo anatumia dawa au la.
Shinikizo la damu la damu linalohitaji matibabu ya dharura hutakiwa tibiwa na daktari au mtaalamu wa afya aliyefunzwa tu. Shinikizo hilo huweza kuwa linaambatana na dalili za hatari au linaloambatana na dalili za hatari. Kwa shinikizo linaloleta dalili za hatari kama zilivyoorosheshwa hapa chini, ni vema ukampigia daktari wako ili kupata matibabu ya dharura, kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Shinikizo la damu la dharura ni lipi?
Shinikizo la dhalura ni lile ambalo lipo au linazidiviwango vifuatavyo;
Shinikizo la sistoliki 180 milimita za mercury (180mmHg) na
Shinikizo la dayastoliki 110 yaani (110mmHg)
Au kwa pamoja ni shinikizo linaloanzia au kuzidi 180/110mmHg
Dalili za shinikizo la juu la damu
Shinikizo la juu la damu mara nyingi huwa halionyeshi dalili yoyote ile, hata hivyo endapo dalili zimeonekana huweza kuwa dalili za kawaida au dalili za hatari. Dalili za hatari huashiria madhara ambayo yameshatokea kwenye mwili wako
Dalili za kawaida na za hatari
Dalili za kawaida
Kizunguzungu
Kutokwa jasho
Madhaifu ya hali ya moyo (kuwa mkali, kuwa na huzuni, kukanganyikiwa)
Kifua kubana
Kuhisi mapigo ya moyo yanaenda kasi
Kupata haja kubwa ngumu
Dalili za hatari
Maumivu au mgandamizo kwenye Kifua, mgongo, taya, shingo, mabega, mikono
Kutapika
Maumivu ya kichwa
Kupumua haraka haraka
Degedege
Kuzimia
Kutopata mkojo
Kubadilika uono (upofu)
Kupata ganzi ya ghafla
Kupooza sehemu yoyote ya mwili
Kutopata mkojo au mkojo kidogo
Namna ya kumpa huduma ya kwanza mgonjwa mwenye shinikizo la juu la damu
Kama una mgonjwa ana shinikizo la juu la damu kwa kupima, fanya mambo yafuatayo ili kumsaidia;
Mpatie dawa ambazo alikuwa anatumia kushusha shinikizo la juu la damu na anywe dozi ambayo alishauriwa na daktari wake
Piga simu mara moja kwa wataalamu wa huduma za dharura ili waje kumpatia huduma, kama ukiweza pia mkimbize hospitali
Kumbuka
Dawa zinazoshusha shinikizo la damu hutolewa kwa cheti kilichoandikwa na daktari, mtumizi ya dawa hizo huhitaji uwe na ujuzi nazo ambao wanao wataalamu wa afya tu
Shinikizo la damu lililo juu sana linapaswa kushushwa na dawa za kunywa au kuchoma kwenye mishipa kwa utaratibu maalumu, kushusha shinikizo la damu kwa ghafla huweza kuleta matatizo mengine makubwa kuliko kuwa na shinikizo la juu la damu
Mfikishe hospitali mgonjwa haraka iwezekanavyo kupata huduma sahihi na kwa wakati ili kuepuka madhara ya shinikizo la juu la damu kupita kiasi
Malengo ya matibabu ya shinikizo la juu la damu la dharura ni, kushusha shinikizo la damu kwenda kwenye kiwango kinachotakiwa ndani ya masaa 2 hadi 6 kwa wagonjwa wenye dalili za hatari, na kushusha shinikizo la damu kwenye kiwango kinachokubalika ndani ya siku 2 hadi 3 kwa wagonjwa wasio na viashiria vya hatari.
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri zaidi kabla ya kuchukua thatua yoyote baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa suhauri zaidi kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
1 Oktoba 2021 08:12:16
Rejea za mada:
Anna K Goodhart . Hypertension from the patient’s perspective. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5072901/#. Imechukuliwa 02.03.2021
Suzanne Oparil, et al. Hypertension. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6477925/. Imechukuliwa 02.03.2021
Frei SP, et al. Frequency of serious outcomes in patients with hypertension as a chief complaint in the emergency department. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/24005086/. Imechukuliwa 02.03.2021
Phillip D Levy, et al. Blood pressure treatment and outcomes in hypertensive patients without acute target organ damage: a retrospective cohort. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/26087706/. Imechukuliwa 02.03.2021
Wolf SJ, et al. American College of Emergency Physicians Clinical Policies Committee. Clinical policy: critical issues in the evaluation and management of adult patients in the emergency department with asymptomatic elevated blood pressure. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/23842053/. Imechukuliwa 02.03.2021
Watson K, et al. Focused Update on Pharmacologic Management of Hypertensive Emergencies. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/29884955/. Imechukuliwa 02.03.2021