Huduma ya kwanza
Katika sehemu hii utajifunza kuhusu huduma ya kwanza kwenye matukio mbalimbali ili uweze kuwa msaada pale itakapohitajika kabla wataalamu wa afya hawajafika kwenye tukio
Kumwagikiwa na kemikali machoni- Huduma ya kwanza
Kumwagikiwa na kemikali kwenye macho inapaswa kuchukuliwa kama tukio la kupata matibabu ya dharura na endapo hatua zisipochukuliwa mapema, inaweza pelekea kuharibika kwa umbo la jicho/macho, matatizo ya uono, ukavu, presha na hata upofu wa macho. Ukubwa wa jeraha na athari zinazoweza kujitokeza hutegemea aina ya kemikali, kiwango kilichomwagikia na muda wa kemikali kuwa katika jicho/macho.
Kujifungulia nyumbani- Huduma ya kwanza
Kujifungua nyumbani inatafsiriwa kuwa ni kujifungua eneo lolote nje ya kituo cha afya, na mama hupatiwa huduma kutoka kwa wakunga wa jadi au ndugu na jamaa. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha kujifungu nyumbani hata hivyo kuna athari pia za kujifungulia nyumbani kama vile vifo kwa wajawazito na vichanga hasa katika nchi zinazoendelea.
Kutapika na kuharisha- Huduma ya kwanza
Kuharisha na kutapika ni miongoni mwa dalili zinazoonekana na huashiria magonjwa ya mfumo wa tumbo, au kushiria shida katika mifumo mingine ya mwili. Kuharisha na kutapika husababisha mwili kupoteza maji na chumvi chumvi muhimu za sodium , potassium, bicarbonate na chloride. Watoto na wazee huwa katika hatari zaidi ya kupungukiwa na maji kuliko watu wazima.