top of page
Uvimbe-kwenye-ulimi-ulyclinic-compressor
ulimi-ulyclinic.jpg
Uvimbe-kwenye-ulimi-ulyclinic

Imeandikwa na daktari wa ULY clinic

 

Uvimbe kwenye ulimi

 

Uvimbe kwenye ulimi unaweza kusababishwa na hali au magonjwa mbalimbali ambayo yameorodheshwa hapa chini.

 • Kuvimba kwa tezi za ulimi mfano kuvimba papilla za ulimi, kuna aina mbalimbali za papilla kwenye ambazo ni ulimicircumvallate (or vallate), fungiform, filiform na foliate. Papilla zote kwenye ulimi huwa na tezi za kuhisi radha ya chakula isipokuwa papilla za foliate. Angalia kwenye picha kuona maeneo ambayo kuna tezi hizi za papilla.

 • Fibroma

 • Papilloma

 • Uvimbe maji wa lymphangioma

 • Ranula

 • Mucocele

 • Kuvimba kwa mishipa ya damu ya ulimi

 • Saratani

 • Lympangioma

 

Makala hii imezungumzia uvimbe wa fibroma.

 

Uvimbe wa fibroma ni uvimbe usio saratani, hutokea sana na hutokana na mwitikio wa mwili dhidi ya uchokozi kwenye kinywa. Kwa jina jingine huitwa uvimbe wa majeraha, au polipu kwenye ulimi. Huweza kutokea kwenye ulimi/ kuta za ndani ya mashavu au kwenye fizi.

 

Vihatarishi vya kupata fibroma ni nini?

 • Uvimbe wa fibroma hutokea sana kwa watu wazima lakini hata hivyo hutokea kwenye umri wowote ule

 • Hudhuru asilimia 2 ya watu wazima

 

Visababishi

 

Husababishwa mara nyingi  na uchokozi kwenye ulimi unaosababishwa na kujing’ata ulimi, kujikwangua na jino lililopasuka au kutobolewa na vifaa mbalimbali vinavyovaliwa kinywani.

 

Dalili

 • Ulimi huwa na nyororo na mgumu kama vile unavyohisi ukishika kilele cha pua

 • Huwa na rangi inayofanana na sehemu zingine za ulimi lakinipia huweza kuwa na rangi iliyopauka au rangi nyeusi

 • Kuta za kipele zinaweza kupata vidonda hvyo kupata makovu

 • Huweza kupata umbo kama la kipele mshikizo au kuwa kama kipele kilicho sehemu ya ulimi kama inavyoonekana kwenye picha

 • Hutokea sana pembezoni mwa ulimi kwenye usawa ambapo meno ya chini na juu yanapokutana, maeneo mengine ni pamoja na ndani ya kuta za mashavu, kwenye fizi na mdomo wa chini

 • Huwa hazisababishi dalili zozote zile

 • Huweza kukua ndani ya wiki au miezi kadhaa ili kufikia ukubwa wa kipenyo cha sentimita 1, hata hivyo huweza kukuwa zaidi ya hapa

 • Uvimbe wa fibroma huwa haubadiliki kuwa saratani

 

Namna gani ya kutambua tatizo

 

Ugonjwa utatambuliwa kwa daktari kuangalia uvimbe huo na kuushika, pamoja na kukuuliza historia ya tatizo hilo. Kinyama kinaweza kukatwa ili kupimwa ili kutofautisha uvimbe wa fibroma na vimbe zingine au kuuondoa uvimbe kabisa.

 

Je uvimbe wa fibroma ndani ya kinywa unaweza kupotea bila tiba?

 

Jibu ni hapana, uvimbe hauwezi kupotea bila matibabu

 

Matibabu ya fibroma

 

Matibabu endapo yatahitajika, uchaguzi wa pekee ni kuondoa kwa njia ya upasuaji. Uvimbe unaweza kutokea tena baada ya upasuaji endapo chanzo cha uchokozi wkenye ulimi kitaendelea.

Imeboreshwa mara ya mwisho, 24.06.2020

Endapo umesoma na kuona kuwa una tatio hili, ni vema ukawasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile.

Pata ushauri na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC kwa kubonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Oral fibromas and fibromatoses. Medscape Reference. https://emedicine.medscape.com/article/1080948-overview. Imechukuliwa 24.06.2020

 2. Periodontics. AAP.  https://aap.onlinelibrary.wiley.com/doi/abs/10.1902/cap.2012.120069. Imechukuliwa 24.06.2020

 3. RDH. Fibroma. https://www.rdhmag.com/pathology/oral-pathology/article/14173234/oral-pathologythe-fibroma-breaking-a-chronic-habit. Imechukuliwa 24.06.2020

 4. Stoopler ET, Alawi F. Clinicopathologic challenge: a solitary submucosal mass of the oral cavity. Int J Dermatol 2008; 47: 329–331.

bottom of page