Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
24 Machi 2025, 12:49:00

Je, mimba huonekana kwenye kipimo cha mimba kuanzia siku ngapi?
Kipimo cha Mkojo
Huonyesha:
Uwepo wa mimba ikiwa kuna homoni ya ujauzito (human chorionic gonadotropin).
Huwezi kuona kiinitete au mfuko wa ujauzito.
Kinaweza kugundua mimba lini?
Kuanzia siku 7-14 baada ya upvuleshaji (au siku 1-5 baada ya kukosa hedhi).
Kipimo cha Damu
Huonyesha:
Kiwango sahihi cha homoni ya mimba, ambacho kinaweza kutumika kukadiria umri wa ujauzito.
Homoni ya ujauzito inaweza kusaidia kuthibitisha ujauzito hata kabla ya kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound.
Kipimo kinaweza kugundua mimba lini?
Kuanzia siku 6-8 baada ya uovuleshaji (kabla ya kukosa hedhi).
Kipimo cha Ultrasound
Kuna aina kadhaa za vipimo vya Ultrosound kwa ajili ya kutambua mimba ambavyo ni;
Ultrasound ya Uke
Huonyesha kulingana na umri wa ujauzito:
Wiki ya Ujauzito | Kinachoonekana kwenye Ultrasound ya Uke |
Wiki 4-5 (Siku 28-35) | Gestational sac (mfuko wa ujauzito) unaweza kuanza kuonekana. |
Wiki 5-6 (Siku 35-42) | Yolk sac (mfuko wa lishe kwa kiinitete) huanza kuonekana. |
Wiki 6-7 (Siku 42-49) | Kiinitete (embryo) na mapigo ya moyo yanaweza kuonekana kwa mara ya kwanza. |
Wiki 8-9 (Siku 56-63) | Kiinitete kinakuwa na umbo dhahiri, vichipukizi vya mikono na miguu vinaweza kuonekana. |
Wiki 10-12 | Mtoto anaonekana akiwa na viungo vyake vikiwa vimeanza kuunda. |
Mimba inaweza kuonekana lini?
Kuanzia wiki ya 4-5 na kuendelea.
Ultrasound ya Tumbo
Huonyesha mimba kulingana na umri wa ujauzito kama ifuatavyo;
Wiki ya Ujauzito | Kinachoonekana kwenye Ultrasound ya Tumbo |
Wiki 5-6 | Inaweza kuanza kuonyesha gestational sac, lakini si mara zote. |
Wiki 6-7 | Yolk sac na kiinitete (embryo) vinaweza kuonekana. |
Wiki 7-8 | Mapigo ya moyo ya mtoto yanaweza kuonekana kwa uwazi. |
Wiki 9-12 | Mtoto anaonekana kwa uwazi zaidi, na viungo vikuu vinaweza kutofautishwa. |
Mimba inaweza kuonekana lini?
Katika kipimo cha ultrosound ya tumbo, mimba huanza kuonekana kuanzia wiki ya 5-6 na kuendelea.
Hitimisho
Mimba inaweza kuthibitishwa kwenye kipimo cha mkojo au damu kabla ya kuonekana kwenye ultrasound. Mfuko wa ujauzito (gestational sac) huanza kuonekana wiki ya 4-5, kiinitete (embryo) huanza kuonekana wiki ya 5-6 wakati mapigo ya moyo huonekana kwa mara ya kwanza wiki ya 6-7. Kwa kutumia ultrasound ya tumbo, mimba huonekana baadaye kidogo kuliko ultrasound ya uke.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
24 Machi 2025, 12:49:00
Rejea za mada hii
Montagnana M, Trenti T, Aloe R, Cervellin G, Lippi G. Human chorionic gonadotropin in pregnancy diagnostics. Clin Chim Acta. 2011 Aug 17;412(17-18):1515-20.
Fromm C, Likourezos A, Haines L, Khan AN, Williams J, Berezow J. Substituting whole blood for urine in a bedside pregnancy test. J Emerg Med. 2012 Sep;43(3):478-82.
Igarashi S. [Clinical significance of early pregnancy factor]. Nihon Sanka Fujinka Gakkai Zasshi. 1986 Jun;38(6):896-902.
Ku CW, Allen JC, Lek SM, Chia ML, Tan NS, Tan TC. Serum progesterone distribution in normal pregnancies compared to pregnancies complicated by threatened miscarriage from 5 to 13 weeks gestation: a prospective cohort study. BMC Pregnancy Childbirth. 2018 Sep 05;18(1):360.
Stephenson JN. Pregnancy testing and counseling. Pediatr Clin North Am. 1989 Jun;36(3):681-96.
Gnoth C, Johnson S. Strips of Hope: Accuracy of Home Pregnancy Tests and New Developments. Geburtshilfe Frauenheilkd. 2014 Jul;74(7):661-669.
Griffey RT, Trent CJ, Bavolek RA, Keeperman JB, Sampson C, Poirier RF. "Hook-like effect" causes false-negative point-of-care urine pregnancy testing in emergency patients. J Emerg Med. 2013 Jan;44(1):155-60.
Fontenot HB, George ER. Sexually transmitted infections in pregnancy. Nurs Womens Health. 2014 Feb-Mar;18(1):67-72.
Silasi M, Cardenas I, Kwon JY, Racicot K, Aldo P, Mor G. Viral infections during pregnancy. Am J Reprod Immunol. 2015 Mar;73(3):199-213.
Whitworth M, Bricker L, Mullan C. Ultrasound for fetal assessment in early pregnancy. Cochrane Database Syst Rev. 2015 Jul 14;2015(7):CD007058.