Je, wamsaidiaje daktari kutambua ugonjwa kwa dalili?
Ili kutengeneza mawasiliano mazuri ya kutambua, kuchunguza na kukupa matibabu yanayoendana na shida yako, unapaswa kuelezea vema dalili kuu na dalili ambata.
PID hutibika na kuisha kabisa endapo itagunduliwa mapema na kutibiwa kwa dawa sahihi. Hata hivyo matibabu hayaondoi madhara na uharibifu wowote uliokwisha tokea kwenye mfumo wa uzazi kutokana na ugonjwa.
Kunguni ni mdudu anayejipatia chakula kwa kufyonza damu ya binadamu. Japokuwa hana madhara makubwa mwili, huweza kusababisha mzio kwenye ngozi kwa baadhi ya watu.
Unaweza kuambukizwa VVU kwa kung'atwa na mwathirika?
Maambukizi ya VVU yanaweza kutokea endapo kidonda cha kung'atwa kimekutana na majimaji, damu, shahawa, ute wa uke, uume au njia ya haja kubwa kutoka kwa mwathirika.
Vipo visa vichache vilivyoripotiwa kusababishwa na njia hii kiasi cha kuonekana kuwa na hatari kidogo ya maambukizi. Uambukizaji kwa njia hii hutegemea mambo mbalimbali baina ya mwathirika na anayeambukizwa
PEP ni dawa ya dharura ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI ndani ya masaa 36 lakini zi zaidi ya masaa 72 baada ya kukutana na kihatarishi cha maambukizi ya UKIMWI.
PEP yenye tenofovir DF/FTC (Truvada) ikitumika kwa siku siku 7 au zaidi, inaweza kinga maambukizi mengine ya VVU kutokana na ngono zembe. Kinga hutegemea aina ya virusi na mwitikio wake kwenye dawa.