top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Charles W, MD

20 Novemba 2021 17:40:59

Je, ni nani hapaswi kutumia vidonge vya majira?

Je, ni nani hapaswi kutumia vidonge vya majira?

Kwa kawaida, unashauriwa kutotumia majira yenye vichocheo viwili kama una hali zifuatazo;


  • Hunyonyeshi na upo chini ya miezi mitatu tangu umejifungua

  • Unanyonyesha na upo kati ya wiki 6 na miezi 6 tangu umejifungua

  • Umri wako ni miaka 35 au zaidi na unavuta chini ya sigara 15 kwa siku

  • Una shinikizo la juu la damu (shinikizo la damu sistoliki kati ya 140 na 159 mm Hg au shinikizo la damu diastoli kati ya 90 na 99 mm Hg)

  • Una shinikizo la juu la damu linalodhibitika, ambapo inawezekana kulifanyia uchunguzi wa kina

  • Una historia ya kuwa na shinikizo la juu la damu na shinikizo la juu la damu la ujauzito

  • Una sirosisi kidogo ya ini au umeshawahi kuungua umanjano wakati ukitumia majira yenye vichocheo viwili siku za nyuma

  • Una ugonjwa wa kibofu cha nyongo (kwa sasa au uliokwishatibiwa)

  • Una umri wa miaka 35 au zaidi na una kipandauso bila aura

  • Una umri mdogo chini ya miaka 35 na unapata kipandauso bila aura ambacho kimeendelea au kimezidi kuongezeka wakati umeanza kutumia majira yenye vichocheo viwili siku za nyuma

  • Umewahi kuwa na saratani ya matiti zaidi ya miaka mitano iliyopita, na haijajirudia

  • Unatumia barbiturates, carbamazepine, oxcarbazepine, phenytoin, primidone, topiramate, au rifampicin.

  • Una kisukari kwa zaidi ya miaka 20 au madhara yake kwenye ateri, macho, figo, au mfumo wa neva

  • Una magonjwa mengine yanayoongeza hatari ya ugonjwa wa ateri na mishipa ya damu kama vile uzee, kuvuta sigara, ugonjwa wa kisukari, na shinikizo la juu la damu.


Kumbuka

Katika hali ya kipekee, iwapo hakuna njia nyingine salama zaidi au haziwezekani kwako kutumia njia hiyo, mtoa huduma mwenye utaalamu ambaye anaweza kuchunguza kwa makini matatizo maalum na hali yako hiyo anaweza kuamua kama unaweza kutumia majira yenye vichocheo viwili au la. Mtoa huduma atafikiria ukubwa wa tatizo lako na madhara yanayoweza kutokea katika kuamua kuwa utumie njia hii au la na ufutiliaji unapaswa kufanyika kwa karibu.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

20 Novemba 2021 17:50:54

Rejea za mada hii

  1. Baird DT, et al. Hormonal contraception. N Engl J Med. 1993 May 27;328(21):1543-9.

  2. Maguire K, et al. The state of hormonal contraception today: established and emerging noncontraceptive health benefits. Am J Obstet Gynecol. 2011 Oct;205(4 Suppl):S4-8. 

  3. Committee on Gynecologic Practice. ACOG Committee Opinion Number 540: Risk of venous thromboembolism among users of drospirenone-containing oral contraceptive pills. Obstet Gynecol. 2012 Nov;120(5):1239-42.

  4. Shulman LP. The state of hormonal contraception today: benefits and risks of hormonal contraceptives: combined estrogen and progestin contraceptives. Am J Obstet Gynecol. 2011 Oct;205(4 Suppl):S9-13. [PubMed]

  5. ACOG Practice Bulletin No. 110: noncontraceptive uses of hormonal contraceptives. Obstet Gynecol. 2010 Jan;115(1):206-218.

  6. Simmons KB, et al. Drug interactions between non-rifamycin antibiotics and hormonal contraception: a systematic review. Am J Obstet Gynecol. 2018 Jan;218(1):88-97.e14.

  7. Weerasinghe M, et al. Overdose of oral contraceptive pills as a means of intentional self-poisoning amongst young women in Sri Lanka: considerations for family planning. J Fam Plann Reprod Health Care. 2017 Apr;43(2):147-150.

bottom of page