top of page

Mwandishi:

WAMJW

Mhariri:

ULY CLINIC

9 Oktoba 2021 10:57:06

Lockdown kudhibiti Corona

Je, lockdown inasaidia kudhibiti Corona? Nchi zilizofanya hivyo zimefanikiwa?

Kufunga shughuli za kijamii na kibiashara (Lockdown) ni moja ya njia ambazo zimekuwa zikitumika katika kudhibiti/kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona sehemu mbalimbali duniani. Lockdown ikitumika pamoja na njia nyingi (kunawa mikono kwa maji tiririka, kuvaa barakoa, nk) kwa pamoja vinasaidia kwa kiwango kikubwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.


Kabla hujaamua kuanzisha lockdown inabidi kuangalia mambo mengi kwa mapana yake, ikiwa ni pamoja wananchi watakavyoweza kupata na kufikia mahitaji yao ya kila siku ya msingi hasa kwa jamii ya watu wa kipato cha chini. Hata hivyo, tathmini ya kisayansi inahitajika ili kusema kwa uhakika ni kwa namna gani lockdown imesaidia au kuchangia punguza maambukizi na kwa kiasi gani.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

9 Oktoba 2021 12:28:02

Rejea za mada hii

bottom of page