Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
ULY CLINIC
9 Oktoba 2021, 11:31:30
Watu gani hawatakiwi kupewa chanjo ya COVID-19?
Chanjo kama zilivyo dawa nyingine zina vigezo katika utolewaji wake. Chanjo nyingi zilizopo kwa sasa zinaoneka kuwa salama kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea. Tafiti bado zinaendelea kubaini usalama na ufanisi wa hizi chanjo kwa watoto.
Watu wasopswa kutumia chanjo ni;
Wenye mzio/ aleji na moja ya kiambata ndani ya chanjo
Pia watu wenye visa vya kuganda damu hawashauriwi kupata baadhi ya chanjo kama vile AstraZeneca, Janssen and Sputnik V.
Watu chini ya umri wa miaka 18
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021, 15:17:35
Rejea za mada hii